Daraja la Kilombero kuzinduliwa

Daraja la Kilombero kuzinduliwa

Mimi naipongeza serikali kwa kupeleka maendeleo kwa wananchi, japo nyuzi kama hizi hazipati wadau wa kutosha, ukilinganisha na zile za "watu wasiojulikana"
Kwanini waipongeza kwa kutimiza wajibu wake?
 
Hii ni platform kubwa kisiasa kwa Mzee Wa magogoni ,kwenye uzinduzi lazima aende na tukio lazima lirushwe live kwny TV na redio kila kona ya nchi wapate kushuhudia utendaji was serikali ya vi wonder
 
mmoja wa viongozi wakuu wa Serikali ambao ama ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, anatarajiwa kwenda kufanya uzinduzi huo.
hivi hata mataifa mengine ni lazima kila mradi kuzinduliwa na viongozi wa kitaifa? naona kama ni matumizi mabaya Ya Fedha za umma
 
yametimia sasa ..afathar limeisha watu wavuke bila wac wac wa kuzama na kale kakivuko
 
UZINDUZI wa Daraja la Mto Kilombero mkoani Morogoro, utafanyika wakati wowote kuanzia sasa baada ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 100.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa aliliambia HabariLeo jana kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Serikali ambao ama ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, anatarajiwa kwenda kufanya uzinduzi huo.

Kwandikwa alisema daraja hilo lenye urefu wa mita 384 na viwango vya kisasa, litakuwa na uwezo wa kupitisha magari ya aina zote na lilivyosanifiwa linafanana na Daraja la Kigamboni.

“Natambua changamoto ya kivuko waliyokuwa nayo wananchi wa Ulanga, Malinyi na Kilimbero, naamini kukamilika kwa daraja hili itakuwa msaada mkubwa kwao. Serikali tumejipanga kuhakikisha wananchi wa wilaya hizo wanaunganishwa vyema na wananchi wa wilaya nyingine za mikoa ya kusini,” alieleza Kwandikwa.

Alisema kuwa baada ya kuaminiwa na Rais katika nafasi hiyo ya Unaibu Waziri, atahakikisha anamsaidia vyema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa kufanya ukaguzi kwenye miradi mbalimbali. Alisema atakwenda kufanya ukaguzi kwenye daraja Oktoba 23.

Moja ya changamoto inayoikabili Wilaya ya Ulanga ni kutounganishwa na wilaya nyingine kwa upande mikoa ya kusini, hali iliyofanya wilaya hiyo kuwa kama kisiwa, lakini pia kuna changamoto ya barabara kwa wilaya zote za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Naibu Waziri alisema kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi haraka ili kuwasaidia wananchi. Wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi maarufu kwa kilimo cha mpunga na ufugaji, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi na mazao yatokayo na mifugo.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana mwezi Januari kivuko cha Mto Kilombero ‘MV Kilombero ll’ kilipinduka baada ya kusukumwa na upepo mkali ambapo watu 30 kati 31 waliokuwemo waliokolewa. Tukio hilo la kuzama kwa kivuko Mto Kilombero lilikuwa la pili baada ya mwaka 2003 pia kuzama na kuua watu kadhaa.

View attachment 608365

View attachment 608367
Bravo!
 
Halafu bado kuna ' Mijitu ' itasema Serikali ya Chama Tawala ya CCM iliyo chini ya Jemedari na Mwanamume wa Shoka Rais Dkt. Magufuli haifanyi Kazi. Acheni tu CCM izidi kuwa ' Madarakani ' kwani inafanya ' Maendeleo ' ya dhati na kweli ambayo yanaonekana na ' Majungu ' tumewaachia ' Wapuuzi ' wanaojijua ambao Wao wanadhani ' Propaganda ' za ' Kuichafua ' CCM na Serikali yake ndiyo ngazi yao kuzidi kuwepo na kuaminika na wale wasiojua ' Kufikiri ' vizuri.

Akhsante sana CCM
Akhsane sana Rais wa JMT Dkt. Magufuli
Mungu ibariki CCM na Walaani wale wote ambao wanaichukia CCM na wape adhabu kali kabisa popote pale walipo
 
Sasa ni kanyaga twende, mambo ya kivuko tupa kule. Ila naishauri serikali kwa kweli maeneo ya kilombero, mahenge, malinyi, ulanga watilie mkazo kwenye miundo mbinu ya barabara ni aibu mpaka sasa miaka 56 ya uhuru miji hii muhimu kwa fursa za kilimo na ufugaji mpaka leo bado ina changamoto ya barabara mbovu.
Kuna madini sana kule. Graphite and germstones
 
Kilichobaki ni kuweka lami katika barabara ya kuelekea Huko Mahenge...sehemu ambayo inasemekana hata mwalimu Nyerere hakuwahi kufika
 
image1-jpg.608365


Hiyo daraja mtoto kwa chini kabisa kando ya hilo kubwa ilijengwa kwa dhumuni gani
 
Back
Top Bottom