Daraja la Kilombero kuzinduliwa

Daraja la Kilombero kuzinduliwa

Nilifika hapo Mwaka jana afadhali ndugu zangu watapita pale bila shida Ifoza ipo vizuri sana na daraja litaongeza thamani za bidhaa toka upande wa pili. Na ile barabara ya mikumi to namtumbo iliisha daaah kwetu kutakuwa pazuri sana
 
UZINDUZI wa Daraja la Mto Kilombero mkoani Morogoro, utafanyika wakati wowote kuanzia sasa baada ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 100.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa aliliambia HabariLeo jana kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Serikali ambao ama ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, anatarajiwa kwenda kufanya uzinduzi huo.

Kwandikwa alisema daraja hilo lenye urefu wa mita 384 na viwango vya kisasa, litakuwa na uwezo wa kupitisha magari ya aina zote na lilivyosanifiwa linafanana na Daraja la Kigamboni.

“Natambua changamoto ya kivuko waliyokuwa nayo wananchi wa Ulanga, Malinyi na Kilimbero, naamini kukamilika kwa daraja hili itakuwa msaada mkubwa kwao. Serikali tumejipanga kuhakikisha wananchi wa wilaya hizo wanaunganishwa vyema na wananchi wa wilaya nyingine za mikoa ya kusini,” alieleza Kwandikwa.

Alisema kuwa baada ya kuaminiwa na Rais katika nafasi hiyo ya Unaibu Waziri, atahakikisha anamsaidia vyema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa kufanya ukaguzi kwenye miradi mbalimbali. Alisema atakwenda kufanya ukaguzi kwenye daraja Oktoba 23.

Moja ya changamoto inayoikabili Wilaya ya Ulanga ni kutounganishwa na wilaya nyingine kwa upande mikoa ya kusini, hali iliyofanya wilaya hiyo kuwa kama kisiwa, lakini pia kuna changamoto ya barabara kwa wilaya zote za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Naibu Waziri alisema kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi haraka ili kuwasaidia wananchi. Wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi maarufu kwa kilimo cha mpunga na ufugaji, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi na mazao yatokayo na mifugo.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana mwezi Januari kivuko cha Mto Kilombero ‘MV Kilombero ll’ kilipinduka baada ya kusukumwa na upepo mkali ambapo watu 30 kati 31 waliokuwemo waliokolewa. Tukio hilo la kuzama kwa kivuko Mto Kilombero lilikuwa la pili baada ya mwaka 2003 pia kuzama na kuua watu kadhaa.

View attachment 608365

View attachment 608367
Safi sana.Nakumbuka nilipita hapo na kapantoni uchwara huku nikiwa nimeshika roho!Hongera sana Magufuli.Watanyamaza tu.Chanja mbuga.
 
Sasa ni kanyaga twende, mambo ya kivuko tupa kule. Ila naishauri serikali kwa kweli maeneo ya kilombero, mahenge, malinyi, ulanga watilie mkazo kwenye miundo mbinu ya barabara ni aibu mpaka sasa miaka 56 ya uhuru miji hii muhimu kwa fursa za kilimo na ufugaji mpaka leo bado ina changamoto ya barabara mbovu.
Aisee nilifika huko hali ya Barabara maeneo tajwa hapo juu ni mbaya sana... Kwasasa wateweza kuvuka kwa usalama lakini safari iliyopo mbele yao ni jasho na damu....
 
Safi sana awamu hii haina blabla, serikali ijikite sasa kujenga barabara ya lami kutoka Kidatu hadi Songea.
 
Nichumu Nibebike

Toka Moro mjini hadi Kilombero ni tsh ngapi?
Mwaka 2015 nililipa nauli ya tsh10000 kutoka moro hadi ifakara halafu nikalipa 10000 kutoka ifakara hadi malinyi, kutoka ifakara hadi daraja lilipo ni pafupi sana nafikiri nauli ni jero
NB: kutoka ifakara kwenda malinyi na mahenge lazima uvuke hilo daraja ila kipindi napita daraja lilikuwa bado tulitumia kivuko hatarishi cha pantoni, kilombero itakuwa less than tsh10000
 
Sisi tunataka kujua nani aliyemtwanga risasi Lissu sio daraja lenu, litatusaidia nini sisi.

We utakuwa shoga who is Lisu compared na Daraja. Unajua walikufa Watu wangapi 2001-2002. na miaka ya Karibuni kwa kivuko kibovu kule. Shut Nenda nairobi. Hizi ndo siasa za maji kunya.
 
Mimi hata sielewi! Hayo maji ndiyo pantoni lilizama? Mbona panaonekana pafupi sana, mwendo wa dakika 1 tu safari imeisha! Au kuna sehemu pana zaidi Ilikuwa inatumika kwa pantoni?
 
Kusema ukweli Daraja la Kilombero ni mkombozi mkubwa sana kwa hizi wilaya mbili yaani Kilombero na Ulanga.

Kile kivuko nakikumbuka sana toka wakati ule kinapita katika rolling wire mpaka kivuko mpaka sasa ni Daraja imara aisee Serikali inajitahidi sana.

Kutoka Ifakara Lipangalala mpaka ng'ambo Lupiro nasikia barabara ni level moja
 
Mimi hata sielewi! Hayo maji ndiyo pantoni lilizama? Mbona panaonekana pafupi sana, mwendo wa dakika 1 tu safari imeisha! Au kuna sehemu pana zaidi Ilikuwa inatumika kwa pantoni?
Ndio hapo hapo mkuu, pantoni halikuzama ila lilisombwa na maji then likapinduka
 
nguvu

Majaruba yanakodishwa kwa tshs ngapi?

Na kutoka Moro mjini hadi huko ni mwendo wa saa ngapi?
 
Thank you for the news but where are the photos?
================================================
Nimeokoteza picha huko mtandaoni. Sijui litakuwa ni lenyewe!

images


Au ngoja niiweke hii ambayo najua watu wa Ufipa hawataifurahia...
ZeLGynduYk3S08q5k66BVXRTssEkVTf_LNJH28B-w7I2lQBn-nf9PtlQn_gMMAn2lphliHD0gyoNuCx7lnwP2_F5K9ZdU9LaXEruu08lMlxIu3f9YqYZDxmKew=w1200-h630-p-k-no-nu




image1.JPG

HILI DARAJA NANI ASIYEJUA NI MOJA YA KAZI ZA HESHIMA KWA KIKWETE PAMOJA NA LILE LA MALAGARASI...
 
Hongera awamu iliyopita kuleta maendeleo hilo daraja ni moja ya matunda

Wanajaribu kuwahadaa watanzania lakini tunafahamu hilo daraja ni moja ya project za KIKWETE.. FLY OVER UBUNGO,TAZARA NA SGR JK alishatafuta mpaka wafadhili..
 
Back
Top Bottom