Daraja la Kilombero kuzinduliwa

Daraja la Kilombero kuzinduliwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,709
Reaction score
9,030
UZINDUZI wa Daraja la Mto Kilombero mkoani Morogoro, utafanyika wakati wowote kuanzia sasa baada ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 100.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa aliliambia HabariLeo jana kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Serikali ambao ama ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, anatarajiwa kwenda kufanya uzinduzi huo.

Kwandikwa alisema daraja hilo lenye urefu wa mita 384 na viwango vya kisasa, litakuwa na uwezo wa kupitisha magari ya aina zote na lilivyosanifiwa linafanana na Daraja la Kigamboni.

“Natambua changamoto ya kivuko waliyokuwa nayo wananchi wa Ulanga, Malinyi na Kilimbero, naamini kukamilika kwa daraja hili itakuwa msaada mkubwa kwao. Serikali tumejipanga kuhakikisha wananchi wa wilaya hizo wanaunganishwa vyema na wananchi wa wilaya nyingine za mikoa ya kusini,” alieleza Kwandikwa.

Alisema kuwa baada ya kuaminiwa na Rais katika nafasi hiyo ya Unaibu Waziri, atahakikisha anamsaidia vyema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa kufanya ukaguzi kwenye miradi mbalimbali. Alisema atakwenda kufanya ukaguzi kwenye daraja Oktoba 23.

Moja ya changamoto inayoikabili Wilaya ya Ulanga ni kutounganishwa na wilaya nyingine kwa upande mikoa ya kusini, hali iliyofanya wilaya hiyo kuwa kama kisiwa, lakini pia kuna changamoto ya barabara kwa wilaya zote za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Naibu Waziri alisema kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi haraka ili kuwasaidia wananchi. Wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi maarufu kwa kilimo cha mpunga na ufugaji, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi na mazao yatokayo na mifugo.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana mwezi Januari kivuko cha Mto Kilombero ‘MV Kilombero ll’ kilipinduka baada ya kusukumwa na upepo mkali ambapo watu 30 kati 31 waliokuwemo waliokolewa. Tukio hilo la kuzama kwa kivuko Mto Kilombero lilikuwa la pili baada ya mwaka 2003 pia kuzama na kuua watu kadhaa.

image1.JPG

unnamed.jpg
 
Sasa ni kanyaga twende, mambo ya kivuko tupa kule. Ila naishauri serikali kwa kweli maeneo ya kilombero, mahenge, malinyi, ulanga watilie mkazo kwenye miundo mbinu ya barabara ni aibu mpaka sasa miaka 56 ya uhuru miji hii muhimu kwa fursa za kilimo na ufugaji mpaka leo bado ina changamoto ya barabara mbovu.
 
UZINDUZI wa Daraja la Mto Kilombero mkoani Morogoro, utafanyika wakati wowote kuanzia sasa baada ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 100.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa aliliambia HabariLeo jana kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Serikali ambao ama ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, anatarajiwa kwenda kufanya uzinduzi huo.

Kwandikwa alisema daraja hilo lenye urefu wa mita 384 na viwango vya kisasa, litakuwa na uwezo wa kupitisha magari ya aina zote na lilivyosanifiwa linafanana na Daraja la Kigamboni.

“Natambua changamoto ya kivuko waliyokuwa nayo wananchi wa Ulanga, Malinyi na Kilimbero, naamini kukamilika kwa daraja hili itakuwa msaada mkubwa kwao. Serikali tumejipanga kuhakikisha wananchi wa wilaya hizo wanaunganishwa vyema na wananchi wa wilaya nyingine za mikoa ya kusini,” alieleza Kwandikwa.

Alisema kuwa baada ya kuaminiwa na Rais katika nafasi hiyo ya Unaibu Waziri, atahakikisha anamsaidia vyema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa kufanya ukaguzi kwenye miradi mbalimbali. Alisema atakwenda kufanya ukaguzi kwenye daraja Oktoba 23.

Moja ya changamoto inayoikabili Wilaya ya Ulanga ni kutounganishwa na wilaya nyingine kwa upande mikoa ya kusini, hali iliyofanya wilaya hiyo kuwa kama kisiwa, lakini pia kuna changamoto ya barabara kwa wilaya zote za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Naibu Waziri alisema kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi haraka ili kuwasaidia wananchi. Wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi maarufu kwa kilimo cha mpunga na ufugaji, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi na mazao yatokayo na mifugo.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana mwezi Januari kivuko cha Mto Kilombero ‘MV Kilombero ll’ kilipinduka baada ya kusukumwa na upepo mkali ambapo watu 30 kati 31 waliokuwemo waliokolewa. Tukio hilo la kuzama kwa kivuko Mto Kilombero lilikuwa la pili baada ya mwaka 2003 pia kuzama na kuua watu kadhaa.
Mkuu sisi tuko busy na kusaka mchawi wa aliyewanunua madiwan
 
Daraja limekamilika hata picha hamna?!!
 
Sisi tunataka kujua nani aliyemtwanga risasi Lissu sio daraja lenu, litatusaidia nini sisi.
 
Thank you for the news but where are the photos?
================================================
Nimeokoteza picha huko mtandaoni. Sijui litakuwa ni lenyewe!

images

Au ngoja niiweke hii ambayo najua watu wa Ufipa hawataifurahia...
ZeLGynduYk3S08q5k66BVXRTssEkVTf_LNJH28B-w7I2lQBn-nf9PtlQn_gMMAn2lphliHD0gyoNuCx7lnwP2_F5K9ZdU9LaXEruu08lMlxIu3f9YqYZDxmKew=w1200-h630-p-k-no-nu

image1.JPG
 
Watavuka bure tu? No, ni vizuri likatumika kama chanzo cha mapato; else ogelea.
 
JPM akazane amalizie lile daraja la Sibiti.

Maana likikamilika,barabara ya lami toka Korandoto to Singida via Manyara itakamilika.

Hivyo kufupisha umbali wa safari toka Mwanza kwenda Dar.

Kwani yatachepukia Kolandoto na kuingia Maswa-Meatu hadi Manyara.

Pia itasaidia kuiunganisha Arusha na Meatu na pia Meatu na Igunga.

Pia Meatu ikifunguka,hata Bariadi,Busega hadi Musoma kutafunguka.

Aongeze bidii.

Tuko bega kwa bega naye kwa maendeleo.
 
Serikali si wamegoma kuongeza madaraja!!!????sasa hili linatoka wapi!!
 
Mimi naipongeza serikali kwa kupeleka maendeleo kwa wananchi, japo nyuzi kama hizi hazipati wadau wa kutosha, ukilinganisha na zile za "watu wasiojulikana"
Kweli kabisa ingekuwa ya kisiasa ungeona wachangiaji wengi mkuu.
 
Sisi tunataka kujua nani aliyemtwanga risasi Lissu sio daraja lenu, litatusaidia nini sisi.
Mkuu we kama daraja halikusaidii piga kimya endelea kumtafuta aliyempiga risasi tundu lisu..huku utakuwa umekosea njia mkuu
 
Back
Top Bottom