Brooklyn
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 1,459
- 284
Kweli naamini kabisa kuwa mheshimiwa haelewi kwa nini Tanzania ni maskini, ishu hapa sio waendesha ma-baloon bali ni uongozi mmbaya wenye rushwa na usioheshimu demokrasia (siasa safi).
Ili nchi yeyote ile iendelee inahitaji Ardhi, Watu na uongozi bora (siasa safi), TZ tuna Ardhi ya kumwaga, watu kibwena ila tatizo ni Uongozi....
.
Mkuu with all due respect for your views, hakuna tena nasisitiza HAKUNA uhusiano wowote kati ya nchi kuendeshwa kidemokrasia (siasa safi) na maendeleo ya kiuchumi. Hakuna tafiti yoyote iliyothibitisha kuwa democratic countries zinapata maendeleo ya kiuchumi zaidi ya zile nchi ambazo zinakandamiza demokrasia.
Mifano michache ya nchi zilizoendelea na demokrasia yake inatia shaka ni China, Singapole, Indonesia. Hata ukiangalia jirani zetu Ruanda wao wana record higher economic growth every year more than Tanzania wakati kidemokrasia tuko juu zaidi yao!!