Daraja la kati ni wale waendesha ma-baloon - Dr. Jakaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daraja la kati ni wale waendesha ma-baloon - Dr. Jakaya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigTime, Jan 20, 2011.

 1. BigTime

  BigTime Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari TBC nikamuona Mh.Dr.Dr.Kikwete akizindua rasmi awamu ya pili ya mpango wa elimu ya sekondari katika kutekeleza MDGs.

  Katika hotuba yake alisisitiza kuwa ili nchi yeyote ile duniani iendelee kimaendeleo inahitaji watu wa daraja la pili...na kwa Tanzania watu hao ni wale waendesha ma-baloon na wenye elimu ya sekondari.....

  Kweli naamini kabisa kuwa mheshimiwa haelewi kwa nini Tanzania ni maskini, ishu hapa sio waendesha ma-baloon bali ni uongozi mmbaya wenye rushwa na usioheshimu demokrasia (siasa safi).

  Ili nchi yeyote ile iendelee inahitaji Ardhi, Watu na uongozi bora (siasa safi), TZ tuna Ardhi ya kumwaga, watu kibwena ila tatizo ni Uongozi....

  Mheshimiwa wake up, tabaka la kati sio waleta maendeleo, bali sera safi, na uongozi bora ndo kitu muhimu kwa sasa...hayo mabaloon yasikufanye uamini kuwa Wa-Tz wameendelea, zaidi ya asilimia 87 ya Watanzania wanaganga njaa kupindukia.
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mabaloon, mmmmmmmmmmmh, sijui; maana ni ya mikopo tu hayo!!!!
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  is he serious ..au mmemkariri vibaya.....kweli mtu ambaye alishawahi kusomaga uchumi miaka ya 70 anaweza kusema hayo???????....hivi mnajuwa magari yote nchi hii hayazidi milioni moja......au mnadanganyika na hayo magari ambayo hayana mahali pa kupita????.....na kufikiri hao ndio watanzania ...nchi bado maskini,watu maskini ..kwa viwango vyetu hata mmiliki wa boda boda anastahili kuitwa mwenye uwezo....wachache wenye magari hao ni mamilionia...hawajafika hata asilimia 5% ya wananchi......bila shaka tabaka la kati tena lenye nguvu ni muhimu...tatizo bado hatuna tabaka la kati lenye nguvu ...
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli ra(H)is tumempata!
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  I hope kuna watu watakuwa wameirekodi... Hata hivyo hainishtui!!!
   
 6. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,498
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  uchumi wenyewe ndio huo wa kupata gentleman/pass degree!
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  No wonder!
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkwere huyooo kazini. Anawashangaa mnaomshangaa!
   
 9. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Alikuwa sahihi. Nchi yoyote kuendelea inahitaji kujenga "middle class" ambayo "definition" yake inatofautiana nchi moja hadi nyingine. Lakini kwa Tanzania ni ukweli kuwa daraja la kati (middle class) ni hao wanaoendesha ma-"baloon". Inawezekana ni ya mikopo, lakini ukweli ni kuwa hawa wana kipato kiasi kwamba mabenki yamewaona wanakopesheka.

  Hawa watu wa aina hii "proportion" yao inapokuwa kubwa katika nchi, ni ukweli kuwa hiyo inakuwa ishara ya mafanikio kwa nchi. Tanzania tukifikia level ambapo asilimia 80% ni hawa waendesha mabaloon, basi tumetoka. Serikali inatakiwa ijenge mkakati madhubuti wa kuhakikisha hili tabaka linakuwa kwani hawa ndo consumers. Uchumi ukiwa na consumers, viwanda vitajengwa kwani soko ni kubwa.

  Hapa rais kasema ukweli. Tunaweza kutofautiana maoni ya jinsi gani ya kufikia kiwango cha kuwa na majority ya watu wetu katika daraja hili la kati, lakini ukweli ni kuwa tunahitaji kuwa na "strong middle class" kwa wingi.
   
 10. T

  Tofty JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kusema ukweli naombea hapa mheshimiwa awe amekuwa "misquoted". Kama ni ukweli basi we are in deep trouble.......he could have put his economics degree into practice in this matter........but again no comments on that front...
   
 11. BigTime

  BigTime Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, Dr. Kikwete alitamka hayo maneno kama yalivyonukuliwa hapo juu, tena cha kushangaza zaidi alikuwa anasoma; design hotuba yake iliandaliwa hivyo, taarifa ya habari jana TBC walirusha hii makitu.
   
 12. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Ni kweli alisema hivyo,akisistiza umuhimu wa kuwa na middle class kubwa,akasema duniani pote middle class ndo nguzo ya kunyanyuka kwa uchumi,majority wanapokuwa lower class ni ngumu sana,tunabaki chini............Its not surprising at all when it come sfrom him,he was very confident whe talking!!!:smile-big:
   
 13. C

  Chesty JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,348
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Aliandikiwa akasoma, nothing more. And i guess it doesn't mean anything to him. Kikwete hana political will ya kuona watanzania wanaondokana na umaskini, he is busy kufanya madili yake.
   
 14. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  kaka nakubaliana na wewe kabisa.......mabaloon haya watu wengi wamekopeshwa na mabenk yameona kwamba wanakopesheka, hivyo watu hawa wakiwa wengi kuweza kukopa uchumi utakua kwani uwekezaji utapanuka na ajira kuwa nyingi nchini....nakubaliana na mheshimiwa rais asilimia 100...ila kwa watu wenye upeo mdogo ni vigumu kumuelewa.
   
 15. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ......mabaloon haya watu wengi wamekopeshwa na mabenk yameona kwamba wanakopesheka, hivyo watu hawa wakiwa wengi kuweza kukopa uchumi utakua kwani uwekezaji utapanuka na ajira kuwa nyingi nchini....nakubaliana na mheshimiwa rais asilimia 100...ila kwa watu wenye upeo mdogo ni vigumu kumuelewa.....alitolea mfano kwa wenye mabaloon na sio kwamba wenye mabaloon ndio haswa middle classes, kuna middle class wengine ambao wana businesses na hawana mabaloon
   
 16. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nafikiri lengo lake lilikuwa kutaka kuonyesha jinsi ambavyo middle class la tanzania lilivyo na uwezo, tabaka hili ndio linauwezo wa kufanya kazi na kuzalisha na pia ndio walaji wakuu wa vitu vinavyozalishwa. Tabaka hili likiwa kubwa ni dhahiri hali ya uchumi inaboreka.
   
 17. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Robo tatu ya hayo ma-baloon ni ya mikopo jamani. pia msisahau mengi yanapark kwenye ofisi za ccm.
  :plane:
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,450
  Trophy Points: 280
  Ni uchumi gani ambao "luxury expenditures" zinajenga mhimili wa kukua "exponent domestic growth"? Kwa nini asiwaze viwanda vya kati, uzalishaji wa kati nk. Tz pick-up car ina ushuru mkubwa sana (import duties) kulinganisha na baloons, pengine ndio sera ya maendeleo ya Tz.

  Tabaka la kati, katika nchi mathalan US, ni tabaka lenye diversity na resources kubwa ndio maana ni segment kubwa ya labour market and economy. Mazingira, sera na sheria za uchumi lazima zielekezwe kuzaa kundi hilo. Sio sera za kindugu, ukiritiimba, rushwa na ufisadi maana wakizaliwa na mfumo mbovu kama huo itakuwa balaa tu; ni sawa na kutoa uchumi mikononi mwa mafisadi fulani na kuwakabidhi wengine.
   
 19. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 565
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Naombeni kuuliza Political Economy imefanana per se na Economics? Nauliza hivi kwasababu nilishawahi kuopt course ya political economy na haikuwa ngumu kiviiile....PE ndio Economics yenyewe?
   
 20. I

  Ibinzamata Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kikwete anachefua na Lugha zake za mitaani. He is the head of state lkn kauli zake nyingine utafikiri muhuni fulani hivi. Ma-baloon, ukizoea kula nawe utaliwa, mambo mswano, changanya na za kwako, watoto wanakiherehere, leo hakuna mchawi hapa, oooops............
   
Loading...