Tatizo la Tanzania ni Uongozi na Siasa

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Hatimaye yametimia Rais Samia amekiri kuwa kuna tatizo kubwa la viongozi. Wananchi tuliowengi tulilisemea hili lakini watawala wakatupuuza. Hayati Baba wa Taifa aliwahi kusema ili nchi yeyote iendelee lazima iwe na;

1. Watu
2. Ardhi
3. Siasa safi
4. Uongozi Bora

Tanzania ina watu mil. 60, ardhi yenye milima na mabonde mito maziwa na bahari, lakini inakwama kuendelea kwa sababu ya mambo 2 nayo ni uongozi na siasa safi.

Suala la uongozi limekuwa tatizo sugu, kwani upatikanaji wa viongozi wetu ni kwa teuzi tu. Kiongozi anateuliwa kisiasa bila kujali ana sifa na ujuzi gani na anakabidhiwa taasisi kubwa kuiongoza kama vile Halmashauri n.k.

Pili kuna viongozi wengi sana ambao Rais ndio anawateua, kwa mujibu wa Katiba iliyopo anateua kuanzia Waziri Mkuu mpaka DAS kule wilayani na wote hawa sifa kuu ni chama anachotoka ambacho ni CCM.

Ushauri
Kwanza tupate Katiba Mpya iweke utaratibu wa kuwapata viongozi, ikiwa ni pamoja na nafasi zote zitangazwe kila Mtanzania mwenye sifa aombe, na baada ya mchujo orodha ipelekwe kwa Rais kwa teuzi ila sio nje ya hao waliochujwa.

Pia kuwe na viongozi waliochujwa ambao sio lazima Rais awateua, bali waajiriwe moja kwa moja na mamlaka husika.

Yote haya yatawezekana endapo tu tutakuwa na Katiba Mpya na tuache kuteua viongozi kwa milengo ya chama; yaani CCM.

Tanzania ni yetu sote na maendeleo ya nchi hayataki chama, kwani kila mwananchi ana haki ya kushiriki shughuli za kimaendeleo kwa nchi yake kama anavyolipa kodi bila kujali chama atokacho.

millardayo_1677821598689879.jpg
 
Back
Top Bottom