Dar: Watuhumiwa 56 Wakamatwa kwa wizi wa magari 12 na pikipiki 28

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 56 KWA WIZI WA MAGARI NA PIKIPIKI, MAGARI 12 YA WIZI NA PIKIPIKI 28.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam katika kipindi cha kuanzia Mwezi Machi hadi Aprili 2021 limefanya oparesheni ya kupambana na wahalifu vinara wanaojihusisha na wizi wa magari na pikipiki katika jiji la Dar es salaam.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam, Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata watuhumiwa hao kama ifuatavyo;
1. SELEMAN SEIF Miaka 52, Mkazi wa Toangoma Mbagala
2. DICKSON KALIKILA Miaka 47, Mkazi wa Kyela Mbeya
3. JAFETH MWAIPOPO Miaka 57, Mkazi wa Kivule
4. PETER PHILIPO Miaka 32, Mkazi wa Sinza
5. OMARI KOMBA Miaka 32, Mkazi wa Kilungule Kimara
6. ABDALLAH ISSA Miaka18, Mkazi wa Kibada kigamoni
na watuhumiwa wengine 7 ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

Watuhumiwa hawa walikamatwa na magari ya wizi kama ifuatavyo;
1. T 387 CKD Suzuki
2. T 775 APA Toyota Carina
3. T 949 BRF Toyota Prado
4. T.627 DJY Toyota IST
5. T459 DGP Toyota Ractus
6. T 373 DMR Toyota Crown
7. T920 DRY aina ya Nissan na Magari mengine 05 ambayo uchunguzi wake bado unaendelea hatutaweza kuyataja namba zake za usajili kwa sababu za kiupelelezi.

Watuhumiwa wote pamoja vielelezo wamekamatwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Mikoa mingine.

Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na majalada yatapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua za kisheria.

Aidha katika oparesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 41 walikamatwa wakiwa na pikipiki 28 zidhaniwazo kuwa za wizi.

Katika oparesheni hiyo tulifanikiwa kumkamata mwizi maarufu wa pikipiki anayefahamika kwa ajina la HAMISI BEATUS aka masai miaka 27, mkazi wa Manzese DSM na IFAKARA Morogoro ambaye ndiye kinara wa wizi pikipiki katika mikoa ya Dar es salaam na Morogoro, ambapo mtuhumiwa huyu alihojiwa na kukiri kuhusika kushiriki kuiba na kupokea pikipiki mbalimbali za wizi kutoka kwa washirika wake waliopo jijini Dsm na Mkoa wa Morogoro.

WITO kwa jamii, wananchi wanatakiwa kuwa makini na magari yao hasa maeneo ya kuegesha ambayo hayana uangalizi au ulinzi wa kutosha.

JESHI LA POLISI LAFANYA UCHUNGUZI SAKATA LA MSANII RAJABU ABDUL KAHAL (HARMONIZE)

Jeshi la Polisi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu za msanii wa Muziki wa kizazi kipya anayefahamika kwa jina la RAJABU ABDUL KAHAL@HARMONIZE.

Hadi sasa wamehojiwa watuhumiwa watano akiwemo msanii FRIDA KAJALA MASANAJA miaka 36, PAULA PAUL PETER miaka 18, RAYMOND SHABANI MWAKYUSA@RAY VANN miaka 27, CLAITON REVOCATUS@BABA LEVO miaka 34, CATHERINE JOHN CHARLES na JUMA HAJI miaka 32. Watuhumiwa wote wamehojiwa na wapo nje kwa dhamana.

LAZARO B. MAMBOSASA - SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM.
20/04/2021
 

Attachments

  • PRESS 20,April 2021N.pdf
    220.8 KB · Views: 11
Back
Top Bottom