Watu 7 wapata upofu kwa kutofuta Ushauri wa Kitabibu wakati wa kutibu Red Eyes

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Mratibu wa Huduma za Msingi za Macho kutoka Wizara ya Afya Visiwani Zanzibar, Dkt. Rajabu Mohamed Hilali amesema hadi kufikia Februari 1, 2024 watu 7 walikuwa wamepata upofu wa macho kutokana na kutofuata ushauri wa Kitabibu katika kukabiliana na Ugonjwa wa RedEyes.

Kufuatia taarifa hiyo Dkt. Hilali ametoa wito kwa Wagojwa kutibiwa na Madaktari wenye taaluma ya macho, kuacha kutumia kila dawa wanayoambiwa na wengine na kuosha macho kwa maji safi bila ya kuongeza Chumvi pindi wanapoambukizwa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya Tanzania, Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa kugusa Tongotongo au Machozi ya Mtu mwenye Maambukizi (kwa kugusa sehemu ambazo mtu mwenye maambukizi amezigusa) hauna Tiba Maalumu.


 
Back
Top Bottom