Dar: Uamuzi kuhusu rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Longido Onesmo Nangole

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Jana tar 14 .08.2017 mbele ya jopo la Majaji wa rufaa ikiongozwa na Jaji wa rufaa Musa Kipenka ilikuja kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya kupinga uamuzi wa Mahakama kuu wa kutengua ubunge wa longido uliompa ushindi Onesmo Nangole wa Chadema dhidi ya Steven Kiruswa wa CCM

Kabla ya usikilizwaji wa rufaa hiyo kulisikilizwa maombi ya pingamizi yaliyowasilishwa na Mawakili wa mjibu maombi yakiwa na hoja mbili

1.Wakili Lamwai aliiomba mahakama itupilie mbali rufaa hiyo kwa kuwa muda wake wa kusikilizwa umepita kwa upande wa mleta maombi (Onesmo Nangole) mawakili Tundu Lissu na Peter Kibatala walipinga hoja hiyo kwa kuwasilisha vifungu vya sheria ya rufaa za kesi ya uchaguzi kuwa rufaa hiyo bado ina muda na kwamba iliwasilishwa mahakamani mwezi wa 6 /2017 ambapo muda wa mahakamama kuisikiliza na kuitolea maamuzi ni miezi 12 tokea rufaa hiyo iwasilishwe mahakamani.

Hoja ya pili ya pingamizi ni kwamba katika kuwasilisha rekodi za rufaa mleta maombi ya rufaa hakujumuisha kielelezo/kizibiti cha simu ya mkononi uliyorekodi moja ya mikutano ya kampeni ya Onesmo Nagole ambayo maneno yaliyokuwemo inasemekana yalikuwa yakimbagua Ndugu Steven Kiruswa.

Upande wa utetezi ukiongozwa.na Wakili Peter Kibatala aliwasilisha hoja ya kupinga pingamizi hilo kwa kuainisha vifungu vya sheria na baadhi ya maamuzi yaliyowahi kutolewa na mahakama mbalimbali za rufaa katika nchi za Kenya,Uganda na ikiwemo Tanzania

Kwaupande wa Mwanasheria mkuu wa serikali uliokuwa unawakilishwa na mawakili David Kakwaya(senior state attoney) na Wakili wa serikali Fortunatus Muhalila hawakuwa na hoja ya kukubali wala kukataa.

Kesi hiyo imeahirishwa kwa mahakama kupitia hoja za pande zote mbili na itatoa notisi ya tarehe ya kutoa uamuzi kwa pingamizi zilizoainishwa.

IMG-20170815-WA0029.jpg
IMG-20170815-WA0030.jpg
 
Mawakili wa serikali hawakuwa na hoja ya kukubali wala kukataa.


Baadae utasikia, ''Upande wa jamhuri hauna nia ya kuendelea na shauri"
 
We unamleta lissu tena. Mkipigwa utasikia "agizo kutoka juu".

Hawa walishindwa kwa Lema baado mnawaamini?
 
Back
Top Bottom