Dar: Samaki wa kichina tani 11 wateketezwa

Dar: Samaki wa kichina tani 11 wateketezwa

Tunaomba uthibitisho wa picha kwa haya uandikayo [emoji41][emoji41]
Hiyo hapo mkuu
itvtz-20190311-0001.jpeg
 
Hivi waafrika tumelaaniwa? Samaki wote tulionao bado watu wanaagiza samaki kutoka China? Wachina wenyewe hawana chakula cha kutosha na wanakula kitu chochote chenye miguu minne kasoro meza. Iwekwe adhabu ya kifungo cha maisha kwa wanaokamatwa.
Hahahaaa!meza na stuli ndo hawali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shehena ya samaki wenye sumu kutoka nchini China wateketezwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi Jijini Dar Es Salaam , zoezi lililosimamiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina.

Shehena ya samaki wenye sumu kutoka nchini China wateketezwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi Jijini Dar Es Salaam.

zoezi hilo lilofanyika leo Machi 11, 2019 limesimamiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina.

Samaki walioteketezwa wanafikia Tani 11 ambapo inaelezwa thamani yake ni zaidi ya TSh Milioni 60, ni baada ya kubainika kuwa samaki hao wana kemikali ya Zebaki yenye madhara kwa jamii na inaweza sababisha Saratani na kuharibu uzazi.
Aiseee,hivi Tz maziwa,bahari,mito yote hii bado tunaimport samaki? Aliyeturoga sisi alituweza sana
 
Marafiki zetu Wachina wana roho nzuri sana hawapendi kuona tunakosa kuĺa samaki
Wapima%20samaki.JPG
 
Attachments

  • Wapima%20samaki.JPG
    Wapima%20samaki.JPG
    67.9 KB · Views: 28
Miaka ya nyuma tulishawahi kulishwa samaki wa kwenye makopo tuliambiwa wanatoka Norway. Ukifungua kopo unawakuta samaki lakini hawana vichwa wala mikia vyote wametoa. Mpaka leo najiuliza hivi wale walilkuwa ni samaki au tulikuwa tunalishwa Nyoka bila kujua.

Democracy means that Domo kiasi
 
Samaki wa China mbona wengi tu, Indonesia n.k.
Halafu bei nafuu kuliko wa Ziwani Tanzania ila wakifika sokoni wanawekwa bei moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni suala la kujiuliza tuna bahari kubwa na samaki wengi inakuwaje samaki wanaagizwa kutoka nje? Kuna samaki vibua wanauzwa ktk viboksi kuanzia idadi ya 35 na 50 kina mama lishe ndio namba moja kununua tunaibiwa samaki ktk bahari yetu halafu wanakuja kutuuzia tena .nchi inakosa mapato makubwa kwa jinsi hii nchi haitaendelea tutapiga mguu upande mguu sawa siku zinaenda maisha ya wananchi yanakuwa magumu

Back
Top Bottom