Dar: Polisi yaua Majambazi 6 na kukamata silaha kadhaa zikiwemo AK 47 tatu na Risasi 217

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Habari wakuu,

Muda si mrefu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa anazungumza na Waandishi wa habari.

Niwaletea kile atakachosema hapa hapa.

UPDATES:

Ndugu wanahabari karibuni katika kupata taarifa ya utendsji wa jeshi la polisi

AK47 tatu risasi 217 mabomu ya kivita 8 magazini 8 zimekamatwa maeneo ya Ubungo ufi. Jeshi la Polisi walifanikiwa kuwaua majambazi 6.

Kitambulisho cha OP 0216239 Theopili Manirakiza MKAZI WA RUKOMBO BURUNDI wa kikundi cha CNDD na FNDD.

Majambazi hao waliuawa baada ya mtego wa Polisi. Walitaka kuvamia bank za hapa mjini katikati.

Tulipata taarifa kuna majambazi wengine.

Willey Ilakozes(Mrundi) , Omary Nassor(Mtanzania) ndio Walipanga kumvamia mwanabiashara.

Kuna gari walivamia, tulikuta lilikuwa na Sh. Mil 50 maeneo ya Mabibo. Tegeta walivamia mchina na kumpora Sh. mil 10.

Huyu Irakoze ni Komando. Alishaua Polisi wawili, Kahama walishawahi kuua askari 2 na kutoroka na AK 47 MBILI.

Mwaka 2012 Irakoze alishawahi kuvamia mgodi na maduka ya Zanzibar.

Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri. Watanzania wanaotegemea kupata kipato kwa kuvunja sheria, wataishia mikononi mwa Polisi. Ni wakati wa kubadilika, wenye kufanya matendo hayo hawatabaki salama.

Yeyote atakayejaribu kupambana na jeshi la Polisi, hatabaki salama

======
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA

Ofisi ya:Kamanda wa Polisi, Kanda maalum ya Polisi, S.L.P.9140,
DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUUWAWA KWA MAJAMBAZI SITA NA KUPATIKANA KWA SILAHA AINA AK 47 TATU, MAGAZINE 08, RISASI 217 ZA AK 47 NA MABOMU YA KUTUPA KWA MKONO 08.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam mnamo tarehe 29 Nov 2018 huko maeneo ya Ubungo UFI kupitia kikosi kazi maalum cha kupambana na ujambazi lilifanikiwa kuwaua majambazi sita na kukamata silaha moja aina ya AK 47, risasi 11, kitambulisho chenye namba OP 0216239 kwa jina la THEOPHILI MANIRAKIZA mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo la Theopili Manirakiza katika majibizano ya risasi.

Majambazi hao waliuwawa baada ya mtego uliowekwa na askari kufuatia taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa(WILLY IRAKOZES@Commando raia wa Burundi, JEAN MUGISHA raia wa Burudi na mtanzania OMARY NASSORO) waliokuwa na bunduki tatu aina ya AK47 na magazine 08, risasi 217 na mabomu ya kutupa kwa mkono 8,ambao walipanga tarehe 29/11/2018 majira ya saa 10 :30 alfajiri kufanya tukio la kumpora mfanyabiashara aliyekuwa akisafiri kuelekea Morogoro akisadikiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa matukio ya uhalifu yaliyotokea huko Mabibo External tarehe 03 Nov 2018 ambapo mfanyabiashara wa TIGOPESA/MPESA aliporwa Tshs. 50 milioni na huko Tegeta tarehe 15 Nov 2018 mfanyabiashara raia wa China ambaye aliporwa Tshs. 10 milioni.

Aidha jambazi huyu WILLY IRAKOZES@Commando amekuwa akitafutwa kwa kufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha hasa katika tukio la kuvamia Benki ya NMB Temeke ambapo aliua askari wawili (02) na raia.

Tarehe 15 March 2011 akiwa anashikiliwa kituo cha Polisi Kagongwa Kahama kwa makosa mbalimbali yeye na wenzake walitoroka baada ya kuwaua askari polisi 02 na kutoroka na silaha mbili aina ya AK47.

Aidha matukio mengine waliyoshiriki ni pamoja na kuteka mgodi wa Tulawaka Geita mwaka 2011, kuvamia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni huko Zanzibar, Mwaka 2012 walivamia kituo cha mafuta huko Kagera na kufanya mauaji, Pia walivamia maduka yaliyopo karibu na kituo cha Polisi Chato na hivyo kukishambulia kituo ili kurahisisha uporaji ambapo walipora Tshs,3 milioni na mwaka 2010 walivamia mgodi wa Nyamongo na kufanya mauaji ya askari 01 na kujeruhi wengine.

LAZARO B. MAMBOSASA-SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

29/11/2018
 
Huwa siamini kama hao majambazi ni kweli majambazi...maaana ni kama huwa wanajitega wapigwe risasi bila wao kurusha hata moja.....
Niwe na AK47 na risasi 200 afu nife kizembe?
Ni bomu nife kizembe ?
Polisi wetu ni wahuni sana, wanaua watu kijinga afu wanawapandikizia risasi
 
Sometimes but not always

Leta ushaidi juu ya ulichosema,kuwa polisi sio kazi nyepesi mkuu.Policemen are well trained cops.
 
Huwa siamini kama hao majambazi ni kweli majambazi...maaana ni kama huwa wanajitega wapigwe risasi bila wao kurusha hata moja.....
Niwe na AK47 na risasi 200 afu nife kizembe?
Ni bomu nife kizembe ?
Polisi wetu ni wahuni sana, wanaua watu kijinga afu wanawapandikizia risasi
Hjakutana na jambazi mzee
Wakikudhuru hpo ndipo utawaelewa
Kwann na wao wanafanyiziwa

Ova
 
Habari wakuu,

Muda si mrefu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa anazungumza na Waandishi wa habari.

Niwaletea kile atakachosema hapa hapa.

UPDATES:

Ndugu wanahabari karibuni katika kupata taarifa ya utendsji wa jeshi la polisi

AK47 tatu risasi 217 mabomu ya kivita 8 magazini 8 zimekamatwa maeneo ya Ubungo ufi. Jeshi la Polisi walifanikiwa kuwaua mabajambazi 6.

Kitambulisho cha OP 0216239 Theopili Manirakiza MKAZI WA RUKOMBO BURUNDI cha CNDD na FNDD.

Majambazi hao waliuawa baada ya mtego wa Polisi. Walitaka kuvamia bank za hapa mjini katikatika.

Tulipata taarifa kuna majambazi wengine.

Willey Ilakozes, Omary Nassor(Mtanzania) ndio Walipanga kumvamia mwanabiashara.

Kuna gari tulikuta lilikuwa na Sh. Mil 50 maeneo ya Mabibo. Tegeta walivamia mchina na kumpora Sh. mil 10.

Huyu Irakoze ni Komando. Alishaua Polisi wawili, Kahama walishawahi kuua askari 2 na kutoroka na AK 47 MBILI.

Mwaka 2012 Irakoze alishawahi kuvamia mgodi na maduka ya Zanzibar.

Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri. Watanzania wanaotegemea kupata kipato kwa kuvunja sheria, wataishia mikononi mwa Polisi. Ni wakati wa kubadilika, wenye kufanya matendo hayo hawatabaki salama.

Yeyote atakayejaribu kupambana na jeshi la Polisi, hatabaki salama

======
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA

Ofisi ya:Kamanda wa Polisi, Kanda maalum ya Polisi, S.L.P.9140,
DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUUWAWA KWA MAJAMBAZI SITA NA KUPATIKANA KWA SILAHA AINA AK 47 TATU, MAGAZINE 08, RISASI 217 ZA AK 47 NA MABOMU YA KUTUPA KWA MKONO 08.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam mnamo tarehe 29 Nov 2018 huko maeneo ya Ubungo UFI kupitia kikosi kazi maalum cha kupambana na ujambazi lilifanikiwa kuwaua majambazi sita na kukamata silaha moja aina ya AK 47, risasi 11, kitambulisho chenye namba OP 0216239 kwa jina la THEOPHILI MANIRAKIZA mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo la Theopili Manirakiza katika majibizano ya risasi.

Majambazi hao waliuwawa baada ya mtego uliowekwa na askari kufuatia taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa(WILLY IRAKOZES@Commando raia wa Burundi, JEAN MUGISHA raia wa Burudi na mtanzania OMARY NASSORO) waliokuwa na bunduki tatu aina ya AK47 na magazine 08, risasi 217 na mabomu ya kutupa kwa mkono 8,ambao walipanga tarehe 29/11/2018 majira ya saa 10 :30 alfajiri kufanya tukio la kumpora mfanyabiashara aliyekuwa akisafiri kuelekea Morogoro akisadikiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa matukio ya uhalifu yaliyotokea huko Mabibo External tarehe 03 Nov 2018 ambapo mfanyabiashara wa TIGOPESA/MPESA aliporwa Tshs. 50 milioni na huko Tegeta tarehe 15 Nov 2018 mfanyabiashara raia wa China ambaye aliporwa Tshs. 10 milioni.

Aidha jambazi huyu WILLY IRAKOZES@Commando amekuwa akitafutwa kwa kufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha hasa katika tukio la kuvamia Benki ya NMB Temeke ambapo aliua askari wawili (02) na raia.

Tarehe 15 March 2011 akiwa anashikiliwa kituo cha Polisi Kagongwa Kahama kwa makosa mbalimbali yeye na wenzake walitoroka baada ya kuwaua askari polisi 02 na kutoroka na silaha mbili aina ya AK47.

Aidha matukio mengine waliyoshiriki ni pamoja na kuteka mgodi wa Tulawaka Geita mwaka 2011, kuvamia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni huko Zanzibar, Mwaka 2012 walivamia kituo cha mafuta huko Kagera na kufanya mauaji, Pia walivamia maduka yaliyopo karibu na kituo cha Polisi Chato na hivyo kukishambulia kituo ili kurahisisha uporaji ambapo walipora Tshs,3 milioni na mwaka 2010 walivamia mgodi wa Nyamongo na kufanya mauaji ya askari 01 na kujeruhi wengine.

LAZARO B. MAMBOSASA-SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

29/11/2018
Duh kama ni kweli huyu jamaa ni yule wa stanbic Nyamongo, ni hatari sana. Wenzake waliuwa karibu wote ila yeye aliondoka anatembea kama anaenda kuhemea sokoni.
 
Back
Top Bottom