Dar: Polisi waua majambazi watano

Jeshi la police kuna shida pale.mm binafsi sina imani nao.risasi za mguu mtuhumiwa anakufa.is it?
 
Risasi za miguu na wakafariki wakiwa njiani kuelekea hospital... Huu msemo hauna mbadala? Kila mara ni hivo hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unaongea haya kwa kuwa hujawahi hata kupigwa ngeta na majambazi. Ila ugewahi kuona waathirika wa matukio ya ujambazi, wala usingekuwa na huruma. Juzi tulikuwa na mzee mmoja ukimwangalia kichwani kumebondeka na sehemu nyingine za mwili zimejaa makovu. Alivamiwa na majambazi na kunyang'anywa pesa. Wakati tukiwa wadogo tunakaa mkoani Mza, tulivamiwa na majambazi. Mzee wangu alichezea kichapo sijawahi ona. Majambazi sio watu. Ni bora ukutane na simba kuliko kukutana na jambazi.
Hongera kwa jeshi la polisi kwa weledi wa kuny'ang'anya majambazi silaha haraka haraka kabla hayajaleta madhara makubwa kwa jamii.
 
Mkuu usibishane nami!!
Policeman always shot not to kill, na tageti yao ni kuanzia kiunoni kushuka chini. Ila akua lazima atoe utetezi(mfano RPC's hujitetea kwamba huwapiga majambazi risasi za miguuni ila wanakufaga njiani wakiwa wana wahishwa hospital)
Soma sheria mkuu usikariri

5/5
Niambie range gani hufundishwa majeshi yetu kuanzia kiunoni kushuka chini ukijibu hilo swali nitajua unaelewa kitu. Na pia kwa mujibu was sheria zako hakuna jeshi lolote lina ruhusiwa kuua.na ukijifanya unajua sana sheria lazima utakuwa mpumbavu mana sheria hufunga vitu vyenye msingi na tija ili tuwe wajinga tusiweze songa mbele
 
Risasi za miguu na wakafariki wakiwa njiani kuelekea hospital... Huu msemo hauna mbadala? Kila mara ni hivo hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app


Sasa jambazi akipigwa risasi ya mguu, ukavunjika vibaya, unafikiri wakati anakimbizwa kwenda hosp kuna guarantee afike akiwa hai? Sometimes sio ya mguu, unaweza kuta imepiga ya moyo kwa sbb wanakimbizana, sasa ya moyo ukiwa hata kabla ya kufika hosp unatangulia mbele za haki, ndio hivyo yaani..!! Tii sheria bila shuruti
 
Uongo mtupu, risasi za miguu tu Halafu wote wakafa? Nakumbuka kuna kauli iliwahi kutolewa "Ukimkamata Jambazi mmalize Hakuna haja ya kesi.... "


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua majambazi watano na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne, kukamata silaha nne na risasi 59 katika matukio matatu tofauti.

Marchi 3 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni huko maeneo ya Kibaha Maili moja Jeshi la Polisi likiwa katika ufuatiliaji lilimkamata mtuhumiwa moja aitwaye Friday Samson (29)askari wa JWTZ Kikosi cha 36KJ Kibaha Msangani na katika mahojiano ya kina alikiri kumiliki silaha mbili kinyume cha sheria na kwamba huzihifadhi silaha hizo nyumbani kwa mke mdogo mtaa wa Muheza Kibaha Pwani na hufanyia matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Baada ya mahojiano Jeshi la Polisi pamoja na mtuhumiwa huyo walifika kwenye nyumba hiyo na kufanikiwa kukamata silaha aina ya AK 47 yenye namba NM174844 ikiwa na risasi 20 ndani ya magazine, boksi moja likiwa na risasi 27,bastola moja yenye namba 3249 ikwa na risasi 7 ndani ya magazine na risasi 3 za silaha ya G3.

Mtuhumiwa alikubali kuwaonyesha wenzake watatu anaoshirikiana nao katika matukio hayo na askari walipofika kwenye nyumba wanayoishi watuhumiwa hao walianza kukimbia kupitia mlango wa nyuma na hatimaye askari walirusha risasi hewani kuwaamuru wasimame lakini walikaidi na ndipo walipowafyatulia risasi za miguu ambazo ziliwajeruhi na walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom