Dar: Polisi waua majambazi watano

Risasi za miguu na wakafariki wakiwa njiani kuelekea hospital... Huu msemo hauna mbadala? Kila mara ni hivo hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hawa inatakiwa wapewe mwezi mzima(au hata miwili na zaidi ikibidi) wa kuangalia series(true event based) za jinsi ya kufanya intelijensia kama FBI files waone wenzao ilivyo ni muhimu kiasi gani kumkamata mtuhumiwa akiwa hai, na jinsi ilivyo "embarassment" kwa polisi kuua mtuhumiwa na pia hata siku moja huwezi kumwita mtuhumiwa ni "jambazi".. polisi sio mahakama!!!
 
Next time polisi wawe wanawalenga WATUHUMIWA risasi za tumbo tu! Maana za miguuni huwa daima zinapelekea vifo vyao na kuwanyima nafasi ya kujitetea ambayo ni ya msingi kwa wote! Au angalau wawe wanalenga vichwa!!

Police wa Bongo ni pathetic
 
Mambo Sasa katika ubora wake,mmewafyatulia miguuni na kufariki njiani kuelekea hospitalini hamjui hata kudanganya!!
Ungekuwa umesomea sheria usinge laumu huo msemo wa polisi. Polisi hawaruhusiwi kuuwa hivyo kama ikitokea kaua, lazima atoe utetezi.

5/5
 
Nan kakwambia polisi hawarushusiwi kuua? Kwa mhalifu ambae unapiga risas tatu hewani akishindwa kusimama unapiga ya mguu na hakuna mafundisho ya range wanayofundishwa kupiga mguu Bali Target ni kichwa nenda dunian kote katika mafunzo ya majeshi yote range ni kichwa tu kupiga mguu ni kumkammata mwalifu akiwa hai ili kuweza kupata ABC.

Tatizo tunapenda kudanganyana sana
Ungekuwa umesomea sheria usinge laumu huo msemo wa polisi. Polisi hawaruhusiwi kuuwa hivyo kama ikitokea kaua, lazima atoe utetezi.

5/5
 
wanawasingizia, siwezi kuamini lolote awamu hii! Polisi akiua asishitakiwe apandishwe cheo ma mshahara! Imani itoke wapi? We need an independent verification!
Siku majambazi wakikuingilia na kukushuhulikia mtazamo wako katika jambo hili unaweza kubadilika. Muulize mzee Yusuf na mke wake
 
Mmmh risasi za miguu zinaua? Tena wote kwa pamoja wanafia njiani
Mambosasa rais kasema watanzania si wajinga


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua majambazi watano na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne, kukamata silaha nne na risasi 59 katika matukio matatu tofauti.

Marchi 3 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni huko maeneo ya Kibaha Maili moja Jeshi la Polisi likiwa katika ufuatiliaji lilimkamata mtuhumiwa moja aitwaye Friday Samson (29)askari wa JWTZ Kikosi cha 36KJ Kibaha Msangani na katika mahojiano ya kina alikiri kumiliki silaha mbili kinyume cha sheria na kwamba huzihifadhi silaha hizo nyumbani kwa mke mdogo mtaa wa Muheza Kibaha Pwani na hufanyia matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Baada ya mahojiano Jeshi la Polisi pamoja na mtuhumiwa huyo walifika kwenye nyumba hiyo na kufanikiwa kukamata silaha aina ya AK 47 yenye namba NM174844 ikiwa na risasi 20 ndani ya magazine, boksi moja likiwa na risasi 27,bastola moja yenye namba 3249 ikwa na risasi 7 ndani ya magazine na risasi 3 za silaha ya G3.

Mtuhumiwa alikubali kuwaonyesha wenzake watatu anaoshirikiana nao katika matukio hayo na askari walipofika kwenye nyumba wanayoishi watuhumiwa hao walianza kukimbia kupitia mlango wa nyuma na hatimaye askari walirusha risasi hewani kuwaamuru wasimame lakini walikaidi na ndipo walipowafyatulia risasi za miguu ambazo ziliwajeruhi na walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku majambazi wakikuingilia na kukushuhulikia mtazamo wako katika jambo hili unaweza kubadilika. Muulize mzee Yusuf na mke wake
Nasema kweli ni majambazi? Awamu hii lolote linawezekana, unielewe!
 
Vipi kuhusu huyo mtuhumiwa (askari wa jwtz)aliyekwenda kuwaonesha hao polisi, wenzake walipojificha; je yupo mikono salama au na yeye alipofika eneo la tukio na yeye alijaribu kutaka kutoroka na hivyo akajeruhiwa mguuni na kufia njiani alipokua akiwahishwa hospitali pamoja na hao majeruhi wenzake?

Mbaya zaidi wamenyimwa haki yao ya kujitetea! Sifurahishwi na matukio ya ujambazi, lakini pia sifurahii vifo vilivyojaa utata vinavyofanywa na vyombo vya dola kwa kisingizio cha huo ujambazi.
 
Ukiona MTU anatetea mhalifu ujue hajapigwa hata roba ya mbao au hajawah ibiwa alafu cha kwanza kwenda kwa sharfu haaaaaaaaaa central police
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom