Dar ni mji hovyo kabisa huwezi hata kuifikia Arusha

Yaani unailinganisha Dar na Arusha mkuu haupo serious.
Huyu naona alikuja Dar - Manzese uwanja wa fisi kwa shemeji yake na hakupata muda wa kulitembelea jiji. Hvi kweli chnagamoto za kumanage watu zaidi ya 5million( dsm) ni sawa na kumanage changamoto za watu laki 3 (Arusha). Bangi mbaya sana!
 
Wakazi wa Masaki na Mbezi hamuwezi feel pain, tabu ni kwa sie washika bomba mkuu! We unaishi kwenye beamer, nyumbani kitu cha Samsung

AC kinapumua kuweka hewa safi ndani ya dakika 20 tu imefukuza joto lote utaanzaje kuwaza. Ofisini 9-5 ni full pupwe maisha lazma yawe mepesi tu.
Niko uswazi nimeridhika tu
 
Kungekuwa kuna kifute cha kutoa Like zaidi ya moja ningeclick nikupe ..... Mtoa mada kazungumzia kero, wanadaslam wanapindisha mada na kufanya comparison
ni kweli kabisa mkuu...nafkiri hawajaelewa mada vizuri tu, ila kuhusu kero kati ya Dsm na Arusha..ipo wazi kabisa kwamba Dsm pakohovyo sana kulinganisha na Arusha

Hata kwenye upande wa maji tu, maji ya Arusha ni masafi, yana taste nzuri mara elfu ukilinganisha na ya Dsm ambayo hata upatikanaji wake ni wa shida katika sehemu nyingi za Dsm. Kiufupi Dsm kuna kero nyingi sana, tukisema tuziorezesha zote hapa..sizani kama tutazimaliza (nina experience na ninachokisema).

Kwa experience yangu ya kuishi Arusha..kero ninazo kutana nazo ni kidogo sana yaani ni kama hamna kero kabisa.
Ni jiji zuri sana aisee..
 
Mimi natokea Arusha.. Honestly speaking Hakuna mji wa kuufananisha na Dar Hapa Tanzania!
Wananchi wake wastaarabu. Mji upo kibiashara kabisa. Pesa zipo!
Arusha na Moshi napapenda sana kama nyumbani ila Dar ni Habari ingine!

Dar kamwe siondoki!
 
Hata kijengehuwezi linganisha Na buza. Hizo unga ltd, matejo,daraja mbili, mbauda, majengo sokon one, ngarenaro Tandale kwa tumbo kuna nafuu. Hakuna Arusha mtaa utakaoulinganisha na oysterbay, masaki, mbez beach ya chini, ununio, mbweni, mikocheni
Mbona mbez beach mnaanza kuimega eti mbezi beach ya chini. ..hebu funguka mbezi zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nafkiri wengi hamjamwelewa mleta mada vizuri..kero anazoziongele mleta mada ni kero ambazo zipo Dar kwa asilimia kubwa kuliko Arusha...kiukweli uwezi kufananisha hali ya uchafu wa dar na Arusha..Dar ni too much.

Au suala la usafiri, Dsm usafiri ni wa shida mno hasa wakati wa asubuhi na jioni mpaka mida ya tatu hivi za usiku.. unakuta kuna foleni,kugombania usafiri, kubanana kwenye usafiri wa uma ni kitu ambacho hakikwepeki katika mida hiyo. ila kwenye suala la usafiri wa uma Arusha huwezi kukutana na changamoto hizo haijalishi ni asubuhi au jioni..hakuna foleni (hutokea mara chache na huwa haichukui muda mrefu)..usafiri upo wakutosha, sio wa kugombania wala wakubanana

katika suala la hali ya hewa, nzuri Arusha ipo vizuri kuliko Dsm. Invutia hata kutembea kwa miguu muda wowote bila kuboeka..yaani unatembea huku unafurahia mandhari ya mazingira na hewa safi pia. Sio kama Dsm, ukiwa na mtoko wako ukaamua kwenda kwa miguu hasa mida ya mchana lazma ulowe jasho na pia unachoka sana kutokana na joto kali ( nafkiri kwa wenyeji wameshaizoea hii hali ya joto kwaio inakua sio changamoto sana kwao). Hata kwenye mida ya usiku sehemu nyingi za Dsm kuna kuwa na mbuu wengi sana kutokana na joto

Kwa upande wangu naungana na mtoa mada, Arusha hamna kero nyingi, hapaboi kama Dsm.
Arusha idadi ya watu ni ndogo na sio kwamba usafiri upo wa kutosheleza ...#pointofcorrection

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What a hell!
Yaani Dar es salaam ni mji wa hovyo sana. Vinyesi siku za mvua watu wanafungulia mikondo kila kona. Mito ya maji ni michafu. Maji ya kunywa ni machafu na yana ladha mbaya. Mji unanuka nuka uchafu tu. Joto la mji hadi kero. Mapipe ya maji mtaani yamechimbiwa juu kwa juu yamepasuka na mengine yanapita kwenye mabafu na vyoo vya watu.

Yaani Dar ni kuzimu tena jehanam. Mji umejaa mbu tu na inzi na harufu mbaya muda wote. Kibaya zaidi kuna joto. Huwezi kuifananisha Dar na hata kwa miji mitakatifu kama Arusha na Nairobi, Dar ni kuzimu kabisa. Aliyeweka wazo la Dar iwe mji wa kibiashara na makao ya serikali miaka ile alifanya makosa makubwa sana, hapafai kuitwa hata Manispaa huku pabaya sana

Joto mpaka kero. Maji machafu kila mtaa. Mipira ya maji ya kuchwa imepita juu kabisa imechanika chanika imefungwa na malboro. Majengo mabovu maji ya mvua kila mahali. Mji hauna mpangilio kabisa huu upo hovyo hovyo. Pabaya pananuka kama chooni. Mbu utadhani ni hospitali ya kuzalisha mbu, pabaya sana. Foleni kila mahali mji mbaya sana huu.

What is the hell?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kama unakaa Masaki, Osterbay, Mikocheni n.k we huendi mjini (posta & kkoo)
Unaishi Masaki then unataka ukaswim Sunrise Beach Resort huoni kama ule umbali ni kakero Fulani + jua linavyowaka, ukifika Ferry zile shombo hujisikiagi vibaya bado hujaweka mafoleni. Tuseme tu ukweli Dar itabaki kuwa Dar kwenye biashara na baadhi ya starehe ila inaboa sometimes.
Mtoa mada yuko sahihi ila kwa kuwa watz Ubishi ni kawaida yetu hatuna budi kubisha hata kwenye ukweli
Mama la mama kwenye Ubora wako😎😎😎
 
Back
Top Bottom