Dar miaka ya nyuma ilikuwa tamu sana

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,582
Nakumbuka miaka ya 2001 kuja mpaka 2014 hivi Dar ilikuwa tamu mno. Maeneo ya Sinza na Mwenge ilikuwa maeneo matamu sana kuishi. Dah! Jamani Sinza ilikuwa tamu balaa, watoto wa Sinza walikuwa wakali balaa, hata sehemu zingine za uswazi nako watoto walikuwa wazuri balaa ila Sinza ndio ilikuwa maeneo matamu sana kuishi.

Yaani ukisimama kwenye vituo vyote vya Sinza watoto wanaokuja kupanda daladala kwenda maeneo mbalimbali walikuwa wazuri balaa. Njoo posta mpya kipindi cha jioni watu wanaposubiria daladala kurudi nyumbani utafurahi mwenyewe maana wadada wote walikuwa warembo. Hadi watoto wa shule za sekondari wa enzi hizo walikuwa warembo hatari. Nakumbuka enzi hizo mambo ya internet kafee ndio yalikuwa yamepamba moto.

Ukitaka kutuma email lazima uende internet cafe, basi huko full kupishana na watoto wazuri. Enzi hizo watoto walikuwa wanapenda sana miziki ya kimarekani, vijana wote walikuwa na swaga za kimarekani. Miziki kama in the club, dilema, babe boy na nyingine nyingi ilikuwa inabamba kweli. Bongo flavor nayo ilikuwa at its peak.

Wakina Juma nature na songi la ugali na sonia, Ferouz na nyimbo yake ya starehe, mwana FA, Ray c, Gangwe mob, uswahilini matola na wengine wengi walikuwa the talk of the town. Siku ya Valentine barabarani kila mtu na mtu wake, wamevalia nguo nyekundu. Enzi hizo mapenzi hayakuwa ya kitapeli kama sasa hivi.

Bar zilikuwa zinafurika kuanzia asubuhi, watu walikuwa na pesa, watu walikuwa wanatumia pesa. Asilimia kubwa ya wakazi wa Dar walikuwa na furaha, sio sasa hivi kila mtu ana majonzi ya ukata. Jamani zamani Dar ilikuwa tamu sana. Zamani Dar ilikuwa tamu sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom