Unajuaje hadithi ya Kamanda Milanzi ni ya kweli?
Yani drug lord wa kimataifa uliyekuwa unamtafuta kwa miaka mingi unaenda kumshika kwa kidhibiti cha gramu 250 za unga za kum sachi? Hizo si ni kesi za kina Wema na Chidi?
Halafu, kama ilivyo ada, wameenda bila search warrant, jamaa akakataa wasije kumbambika. Polisi wakatumia "mbinu zao" kumsachi, mbinu gani za ku sachi ambazo polisi wa bongo wanazo FBI hawana? Maana hatujawahi kusikia kuna mbinu duniani kote ya kusachi nyumba ambayo mwenyewe hajakubali na yuko hapo hapo mlangoni. Uchawi?
Long and short of it ni kwamba hawana ushahidi wa kuridhisha na hawana credibility katika hako ka home searching kao kwamba hawajambambika vikete.