Dar: Mapokezi ya ndege ya pili ya ATCL aina ya AirBus A220-300(Ngorongoro) katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Rais Magufuli leo anatarajia kuongoza watanzania kupokea ndege nyingine ya sita aina ya Airbus A220-300, inayowasili hapa nchini ikitokea nchini Canada, na kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa katika kipindi cha awamu ya tano kufikia 6.


UPDATES; 1520hrs

=> Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 iliyonunuliwa na serikali yatua uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar muda huu. Rais John Magufuli, viongozi waandamizi, viongozi wa dini na wananchi wajitokeza kuipokea.

=> Askofu Kakobe: "Hata ungefanya kitu gani huwezi kusifiwa na Watu wote na MUNGU anasema kama utasifiwa na Watu wote basi ni ole wako, tumekusanyika kwa ajili ya ndege za ATCL ni jambo zito na kubwa lakini usitarajie Watu wote watakusifu, wengine watakusifu ukifa"

“Mheshimiwa mimi huwa ni mbishi kidogo…na ukiona nimekuja mahali kama hapa…ujue umenikosha,” – kauli ya Mchungaji wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe akikiri kukoshwa na Rais

Kakobe amsihi Rais Magufuli alale. “…Umewahi kutuambia unashindwa kulala kwa sababu kitanda kimejaa mafaili…lakini leo tunakusihi…hebu jipongeze ulale…” – kauli ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe.

Paul Makonda: Mh. Rais naomba niruhusu kwa leo nikupe salamu tu kwa kuwa furaha yangu imezidi

> Pokea salamu kutoka kwa Mwl. Christopher Mwakasege. Anakupongeza kwa jambo kubwa unalolifanya ila ameshindwa kuja yupo Tukuyu kwa jambo la kifamilia.

Paul Makonda: Nilipotoa tangazo la kuja hapa nilisema waje wale waliowahi kutoa ahadi na wakatekeleza.

> Tumekuja kukuunga mkono kwa kuwa ulitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na unatekeleza ikiwemo elimu bure

Paul Makonda: Hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama baba wa familia. Nikikua nataka niwe kama wewe

Akizungumza katika mapokezi ya ndege aina Airbus A220-300 hapa uwanja wa ndege, RC Paul Makonda amewataka viongozi wa Dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Dkt Magufuli.

Serikali imesema Ndege mpya iliyopokelewa leo aina ya AIRBUS A220-300 NGORONGORO itakuwa na safari za kila siku kwenda Dodoma kuanzia January 16 mwaka huu tofauti na ilivyo sasa ambapo ATCL hufanya safari 4 tu kwa wiki kwenda Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji ATCL Ladislaus Matindi: Ujazo wa ndege hizi 2 za Airbus unatuwezesha kutoa huduma kwa Mkoa wa Mtwara na mikoa yenye viwanja vidogo

> Ndege hizi zote zina uwezo wa kubeba tani 19 na tayari tumefanikiwa kuingia kwenye makubaliano ya kusafirisha nyama ya mbuzi

Matindi: Tayari tunashirikiana na ubalozi wa Uingereza ili kuwakutanisha wadau wa usafiri wa ndege kuweza kujadiliana na kukubaliana kuhusu fursa zilizopo kwenye shirika la ndege

Matindi: Baada ya kurudisha kwenye mfumo wa tiketi duniani kazi ya kuunganisha ATCL kwenyw mfumo huo inategemewa kuwa imekamilika Januari hii.

> Tunatazamia pia kutoa huduma kwa wateja kwa saa 24 kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo kwenye matengenezo

Matindi: Kufika kwa ndege hii kunahitimisha mkataba wa ununuzi wa ndege mbili za Airbus A220-300, ndege hizi zinatuwezesha kuwa na upanuzi wa mtandao wa safari zetu na kutoa huduma za kimkakati katika soko la Kusini mwa Afrika

Ladslaus Matindi: Katika safari ya ndege hii tulikuwa na Kapteni Khamisi, Kapteni Msingi na aliyeiteremsha ndege hapa nchini ni Kampteni Budodi na kiongozi wa safari alikuwa ni Kapteni Patric anayetoka kwenye kampuni iliyotuuzia ndege na atakuwa hapa kwa miezi 3 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana wetu

Waziri Mkuu Majaliwa: Jambo hili ni kubwa sana na tunaamini wafanyakazi mtafanya kazi kwa weledi na kuendelea kuliinua shirika letu na ukitaka usafiri mzuri safiri na Air Tanzania

Mhandisi Isack Kamwelwe: Nakupongeza Rais wangu kwamba uliweka nia na ukaagiza tununue ndege 7 na zimenunuliwa ambapo Oktoba mwaka huu inaingia ndege nyingine na juzi umeniambia tununue ndege nyingine tena

Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson: Sisi kama Bunge tunakupongeza Rais kwa kazi kubwa unayoendelea kuifanya, sote ni mashahidi kwa kinachoendelea, ulipokuja bungeni kusema utanunua ndege hatukuamini lakini kama matani tunazo ndege Sita

Mbona maaskofu wa madhehebu makubwa huwa haalikwi kwenye utoto huu?
 
Hahaaa hii nchi kwahiyo jiwe Ameshatubu !!!?

Jiwe kweli balaaa kamnyoosha mpaka kakobe leo hii mpaka yeye anatamani kuyameza maneno yake aliyo mwambia kuwa akatubu"

Ndugu zangu mkipata fursa za kupiga hela zitumieni faster mkijifanya kukaidi mtakufa kwakujifanya wazalendo " hii nchi bila unafiki maisha hayasongi "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemsikia Rais kama vile anasema Katibu Kiongozi Balozi Kijazi ndiye aliyeidhinisha pesa za kununua ndege ...... hii imekaaje!!?
 
Back
Top Bottom