Pamoja na kwamba hatua aliyochukua Lukuvi inaweza kuwa ndiyo dawa sahihi ya uozo uliopo kwenye Serikali ya CCM na watendaji kwa ujumla. Lakini, kwanza timing yake inatia mashaka kwamba ndio yaleyale ya kutaka kuwa-impress wapigakura waone kwamba Serikali ya CCM inafanya kazi.
Hata hivyo, ingekuwa ni faraja zaidi kama Lukuvi angelitutajia majina ya watu ambao wamewahi kupewa viwanja kwa njia za aina hiyo kwa sababu mpokea rusha na mtoa rushwa wote wanahesabiwa ni wakosaji. Hao watu wenye kwenda kuhonga maofisa ardhi ili wapate viwanja ni wahalifu wakubwa sawa na akina Magesa wanaopokea hiyo rushwa na kutoa viwanja isivyo halali.Pia tusisahau kwamba kuna 'vigogo' ambao wanatumia nafasi zao na majina yao makubwa kupata viwanja. Matumizi hayo mabaya ya nafasi zao nayo ni kosa linalohitaji kushughulikiwa kama watajavyoshughulikiwa wengine wanaoshawishi maafisa ardhi kutenda kosa la upendeleo katika ugawaji viwanja. Tunataka kusikia majina ya mameya akina Londa, Kimbisa n.k. yakitajwa kwa sababu Mameya na viongozi wa Halmashauri huwataka maafisa ardhi watoe viwanja kwa vigogo na matajiri kadha wa kadha nchini kwa manufaa yao hao viongozi husika. Mfano hai niliowahi kuusikia ni juu ya kiwanja kimoja cha wazi pale Msasani ambacho kiligawiwa kwa Meya, Afisa mmoja Mwandamizi Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na kwa Waziri wa Ulinzi kwa majina na si kwa ajili ya matumizi ya ofisi zao. Sasa viongozi kama hao wakianza kuvamia maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa matumizi ya umma, maafisa ardhi watashindwaje kuiga?