Dar lands official arrested | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar lands official arrested

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Jun 17, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  This action has been long overdue. Or is it a prelude to the coming elections? Hope we see more of the likes of this!

  By Dominic Nkolimwa

  17th June 2010
  [​IMG] Linked to plot selling allegations
  [​IMG] 16 other staff suspended, unit closed  [​IMG]
  Dar es Salaam Regional Commissioner William Lukuvi

  Dar es Salaam Regional Commissioner William Lukuvi has ordered the Kinondoni Municipal Council Lands Unit closed and its head arrested following corruption and forgery allegations in plot allocations.

  The RC told journalists that he had ordered the arrest of the Head of the Lands Unit, Magesa Magesa and suspension of 16 of its staff for further investigation in relation to the allegations.

  The allegations are linked to the selling of two plots located at Msasani Peninsula in Dar es Salaam.
  The RC said that he decided to close down the Land Unit after a surprise visit to the office in which the lands officers failed to provide him with important documents, among them the title deeds for the plots which were to be issued with building permits.

  "It took about three hours to look for the files which had the title deeds of the two plots, an indication that something was wrong somewhere," he said.

  Lukuvi said after the three-hour search, the documents were brought to him and after going through them, he discovered that the documents relating to the sale of the plots had been forged. The signature and rubber stamp of the Kinondoni Municipal Director were forged, he said.

  He identified the plots as number 1,274 and 1,275 which all are open spaces according to the City Planning Map.

  Lukuvi said that according to the information from the Lands Unit the plots were sold since 2009. He said when questioned, Magesa allegedly admitted that he sold the plots under political pressure.
  Kinondoni municipality is leading in complaints of corrupt land deals, which include the sale of open spaces.

  Lukuvi said what he had done was just an administrative measure to arrest the situation, while other procedures will follow including thorough investigation of the allegations.

  Lukuvi clarified that no institution can change the land use plan apart from the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development.

  "Even if the Municipal council were to decide to change the use of particular plots, such change can not be implemented until it is approved by the ministry itself."

  "In have ordered the Municipal executive director to provide the list of all open plots which have been sold, so that PCCB can investigate and take disciplinary measures against all the culprits," he said.

  He said he has started with Kinondoni Municipality, but the process will continue in the other municipalities.
  The Dar es Salaam Special Zone Commander Suleiman Kova confirmed the arrest of Magesa and that investigation into the allegations against him had began.

  During his tour of Dar es Salaam last month, President Jakaya Kikwete was irked by land officers who were reported to be involved in selling open spaces.

  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Lakini bidae wataachiwa tu
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kama kawaida.
   
 4. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi na ile plot pale kwenye kona kali iliyokuwa na mbuyu mkubwa ukitokea njia ya msasani KKKT - CCBRT - kuelekea Masaki pana uzio mzuri tu wa magogo ndio penyewe? Maana ghfla pamewekwa uzio kama mahali maalumu pa watoto kucheze...japo pamekaa kiuuzwaji uzwaji!

  By the way ule mbuyu haukuanguka wenyewe nini? Ndio ilikuwa kuelekea uuzaji? Wera Wera! Tanzania...doh tutabanana hapa hapa! Haendi mtu mbali mpaka maeneo yote ya wazi yaishe.
   
 5. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0


  And equally so : Lukuvi arrested Magesa Magesa under political pressure!

  Obladi Oblada ... Life Goes ON
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kiutendaji mi naona ni move nzuri tu, actually muda huu ndio njia pekee ya kupunguza kasi ya mafisadi...Ishu ni kwamba je vyombo vinavyohusika vitamwadhibu accordingly, au atatembeza rupia?
   
 7. A

  Alpha JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  GOOD NEWS!!!

  but meaningless unless he is successfully prosecuted and severely punished.
   
 8. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mimi siku hizi sina imani sana na maamuzi ya serikali hasa linapokuja suala la kushughukia ufisadi! kama magesa anasema aliuza under political pressure atueleze ni politician gani aliye m pressurize hadi akapauza hapo, na tuna imani gani kuwa huyo politician hata m presurize Lukuvi kumuachia Magesa? kuelekea uchaguzi tamthilia nyingi tu zitaanza luningani na tusubiri tuone!
   
 9. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Lukuvi anafahamu kinachoendelea, wanasiasa ni wazuri sana wa kucheza karata
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kama kawaida yetu, kukurupuka baadaye anaachiwa with apologies of course
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Ni plot halali ya Marehemu Mzee Wilfrem Mwakitwange.....
   
 12. M

  MJM JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hata ikienda mahakamani bado kesi itakwisha kwa political pressure. Life goes on. Ndiyo maana kila mtu anataka kuwa mwanasiasa ili asiwe na pressure ila aipeleke kwa watu na maisha yajipange safi. Tanzania Tanzania nakuponda kwa moyo wote..........
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hii imekaa kama sehemu ya kampeni za CCM. Kwanini Lukuvi hakuchukua hatua hii kabla ya JK kutembelea mkoa na kulizungumzia swala hili hili la kuuza maeneo ya wazi? Ina maana Lukuvi alikwisha jua hiyo political pressure inatoka wapi, akaiogopa ndiyo maana akamwita raisi kutembelea mkoa ili kulainisha hiyo political pressure??? CCM ni chafu, inanuka siasa zilizooza, inanuka ufisadi. Hakuna dawa nyingine zaidi ya kuiondoa madarakani ili ipate muda wa kujisafisha.
   
 14. G

  Godwine JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  vipi na nyumba za serikali walizopeana watarudisha au na mshikaji naye alichukua, hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 15. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  LizSenior. Kile ni kiwanja cha marehemu Mwakitwange aliekuwa mbunge awamu ya kwanza na mmiliki wa Rungwe Oceanic ila kina mgogoro wa kifamilia.
   
 16. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Uozo upo mwingi na sana sana hizi ni mbio za kuelekea uchaguzi mkuu, kuna zile Nyumba zilizokuwa zimejengwa Masaki, rita Mlaki alipokuwa Naibu waziri Ardhi alisimamia mpaka zikabomolewa, Mhandisi wa wilaya akasimamishwa na kushtakiwa cha kushangaza mpaka leohakuna kinachoendelea,

  Mtawapeleka mahakamani na hakuna kitakachofanyika, ni ngumu saana kusimamia sheria kwa nchi maskini kama Tanzania, ambapo wenye uwezo wananguvu kuwazidi watawala
   
 17. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mambo ya nchi hii yanakatisha tamaa sana. Katika hali ya kawaida na watu makini alichofanya Lukuvi anapaswa kupongezwa, tatizo who knows kama ni kung'arisha nyota kuelekea uchaguzi mkuu hili ndio tatizo.

  Jambo hili alilolifanya anastahili pongezi kama uamuzi huu una umakini ndani yake na kwamba yeye binafsi afuatilie suala hili na kuhakikisha ushahidi unafuatiliwa kwa wakati na unapatikana vinginevyo inaweza kuwa ni changa la macho kwa wabongo na pengine hii ni danganya toto kama atakuwa ana mpango wa kutangaza nia somewhere.
   
 18. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ardhi wilaya pameoza. tatitizo sio uuzwaji wa
  "open space" tu bali hata kwenye kushughulikia
  viwanja vilivotengwa kwa ujenzi nako ni taabu tupu.

  hongera lukuvi
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,677
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  Huu ni mwaka wa uchaguzi isiwe ni geresha toto tu kwa wapiga kura kisha baada ya ya uchaguzi anaachiwa huru kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha. Matatizo ya kiwanja kimoja kuuzwa kwa mtu zaidi ya mmoja hayakuanza leo bongo ni ya miaka nenda ,miaka rudi. Tusubiri tuone hatima ya hii kesi itakuwaje
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,677
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  Wengine 22 wanaswa kwa ufisadi wa ardhi


  Saturday, 19 June 2010 08:16
  *Lukuvi akamata watano Temeke pekee
  *TAKUKURU Dar yaanza kazi rasmi
  *Ofisi za Temeke, K'ndoni, Ilala zafungwa
  Na Benjamin Masese
  Majira

  SAKATA la ufisadi wa uuzwaji wa viwanja vya wazi jijini Dar es Salaam iliyosabisha watumishi 16 wa Manispaa ya Kinondoni kukamatwa, limechukua sura mpya baada ya watumishi wengine 22 wakiwemo watano kutoka Manispaa ya Temeke kutiwa mbaroni. Kukamatwa kwa watumishi hao 22 kunafanya idadi ya watuhumiwa wa sakata hilo kufikia 38.

  Aawali Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Magesa Magesa, na watumishi wengine 15 wa Idara yake walikamatwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka za kuuza maeneo ya wazi huku taarifa za awali zikionesha kuwa mtandao huo wa kifisadi wa ardhi umeenea katika Manispaa zote tatu.
  Akizungumza na waandishi wa jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Wiliam Lukuvi, alisema watumishi hao walipatikana na tuhuma za kuandaa kwa siri nyaraka za upimaji viwanja na kuviuza, kutoa kibali cha umilikaji kinyume ch asheria.

  Alisema watumishi hao walikutwa wakiwa wamejitayarishia hati 52 ambazo tayari walikuwa wamekwishauza kwa watu bila fedha hizo kuziwasilisha kwa Mkurugenzi bila kumhusisha kama kiongozi wao mkuu katika utendaji kazi zao.

  Bw. Lukuvi alisema kutokana na hali hiyo aliamua kuwaondoa nje na kuwaweka chini ya ulinzi na kufunga ofisi hizo ili kulinda nyaraka hizo muhimu kabla ya kufichwa na wahusika.

  Alisema watumishi hao walikutwa na nyaraka mbalimbali batili walizoziandaa kuhusu uuzwaji wa viwanja zaidi ya 20,000 katika manispaa hiyo bila kumshirikisha Mkurugenzi wao.


  Alisema kutokana na mkanganyiko huo aliamua kufunga ofisi tatu zote zinazohusika kutunza nyaraka za mikataba ya ardhi na kukabidhi funguo kwa Mkurugenzi ambapo watumishi hao walikabidhiwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa mahojiano zaidi.

  Alisema kutokana na mtandao huo kuonekana kusambaa katika Manispaa zote za Dar es Salaam alifikia hatua ya kufanya ziara za kushtukiza katika Manispaa ya Ilala na kufunga ofisi za Ardhi kwa ukaguzi zaidi.

  Katika hatua inayoonesha ufisadi huo ni mkubwa na una mtandao mpana zaidi alisema tayari amepata taarifa kwamba ofisi za jiji zinazohusika na utunzaji wa nyaraka za ardhi na ramani nayo imehusika hivyo ameagiza ifungwe kwa muda.


  "Hivi sasa ofisi zote za idara ya Ardhi katika katika Manispaa tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala nimezifunga kutokana na kuonekana kujihusisha na uuzwaji wa viwanja vya wazi kinyamela, pia watumishi watano na bosi wao nimewakamata na kuwakabidhi TAKUKURU,"alisema Bw.Lukuvi.


  Alisema ameunda tume ya watu saba kutoka wizara ya Ardhi, TAKUKURU Polisi na wengine kutoka ofisini kwake kuanza ukaguzi wa nyaraka zote ndani ya siku ishirini na moja na kukabidhi taarifa rasmi ifikapo Julai 9, mwaka huu.


  Alisema tume hiyo ilianza kazi jana (juzi) katika ofisi za Kinondoni hadi Juni 26, Juni 27 hadi Julai 2 watakuwa Ilala na Julai 3-5 watakuwa Temeke huku Julai 6-8 zikitengwa kwa ajili ya kufanya majumuisho na Julai 9 watawasilisha ripoti yao kamili kwake.


  Alisema iwapo watumishi hao watabainika kuwa na makosa watafikishwa katika vyombo vya sheria na ikibidi utaratibu wa kuwafuta kazi utafanyika haraka. Kwa upande wa wafanyakazi wa Kinondoni Bw. Lukuvi alisema hawataruhusiwa kufanya kazi tena katika ofisi zao.

  Akizungumzia mahojiano kati ya polisi na watumishi 16 wa Kinondoni yalioanza juzi alisema katika mahojiano hayo idadi ya wahusika iiliongezeka hadi kufikia 33. Alisema hivi sasa mmiliki wa Kampuni ya Tanzania Building Weight aliyeuziwa viwanja namba 1274 na 1275 amefikishwa katika vyombo vya sheria kwa mahojiano zaidi.


  Alitoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam wenye malalamiko makubwa ya ardhi kuandika barua na kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Manispaa husika ili ifanyiwe kazi ndani ya siku za uchunguzi wa tume aliyounda.
   
Loading...