Dar Kuna magari laki moja tu! Tatizo ni barabara

Dar Kuna magari laki moja tu! Tatizo ni barabara

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,730
Reaction score
15,388
Kama nilivyosema Tatizo la Tanzania hasa Dar ni barabara ndogo. Hapa Houston, TX tuna magari milioni mbili (2 million) na hatuna jam kama ya Dar

2cyiqg5.jpg

From IPP website

The President explained that the project funded by the World Bank and the government of Tanzania, was intended to reduce traffic jams and ease transport in the city set to become more serious in the future.

He said the number of vehicles in Dar es Salaam was expected to reach 500,000 by 2030 from the current slightly over 100,000 and that if comprehensive measures were not taken to improve transport infrastructure, traffic jams would worsen.
 
Kumbe wakati Kikwete anatamba kuwa watajenga barabara za juu kwa juu alikuwa akijua kuwa kuna wafadhili? Huu ni ugonjwa mbaya sana kwani tunapokuwa tunapanga mipango ya maendeleo kwa kutegemea misaada tunakuwa tunajinyang'anya uhuru wetu kabisa. Missada ni mizuri iwapo inaongezea kwenye mipango yetu lakini tusipange mipango yetu, tena kwa mbwembwe za moto sana, huku tukitegemea misaada. ndiyo maana miaka ya hivi karibuni tulinyimwa misaada hadi bajeti ya serikali ikakwama.

I hate this B/S called CCM kabisa.

Tanzanites zetu zote karibia zinakwisha pale Arusha; Alamsi nayo imekauaka pale Mwadui, na dhahabu nazo kule Musoma na Tarime karibia zinakwisha tunabakiwa mapango tu huku nchi haina kitu. Hakuna tofauti kabisa na maisha ya kiuchumi tuliyokuwa nayo wakati wa mkoloni kwani raslimali zote za nchi zilikuwa zinawafadia wakoloni tu.
 
CCM haihitaji ufandili wa fedha, inahitaji ufadhili wa AKILI na MAWAZO...
 
Ilikuwa ahadi ya siku nyingi sana kumbe iliyotolewa na Eddy

attachment.php

Barabara.JPG​
 
Kikatuni nacho kinachemka. Barabara ya Sekenke ilishajengwa. Ya zamani ilishafungwa kule milimani ikajengwa nyingine pembeni, na ajali pale zimepungua. Sasa sijui Sekenke gani kinaiongelea hiki kipanya.
 
.............nadhani ilikuwa katuni ya mwaka 2007 baada ya Lowasa kusema kuwa ndege ya uchumi imeanza kupaa kabla hajashushiwa kipigo cha Richmond. BTHW: Nimepitia barabara nyingi za Tanzania zilizojengwa katika awamu hii nikagundua kuwa asilimia 80 ziko chini ya ubora na zitabomoka hata kabla ya miaka mitano.
 
Tupe ushahidi. otherwise, utakuwa umeleta story za udaku humu
 
tanzania ni sikio la kufa .........halisikii dawa. weshakaa viongozi wa kila aina, lakini hali ni ile ile na muelekeo wa kutoka ccm katika kipindi cha miaka mitano mijayo hakipo.

huko vyama vya upinzani nako kelele zile zile za ufisadi na rushwa..............nahofia kuwa mabadiliko kwa tanzania ni ndoto.
 
Afrika yote kusini mwa jangwa la Sahara ukiondoa Afrika Kusini (ambako kuna Wazungu wengi) iko hivyo. Nenda Cameroun...nenda Burkina Faso....nenda Mali...nenda Zambia..nenda Lesotho...hakuna tofauti kubwa sana. Wote ni ulimwengu wa tatu. Kote kuna ufisadi uliokithiri. Kote kuna ujinga wa hali ya juu.

Kwa hiyo si Tanzania tu iliyo sikio la kufa. Nasema....sisemi....lakini mnajua ninachosema.....
 
Back
Top Bottom