DAR: Jeshi la Polisi Kanda Maalum kuwachukulia hatua kundi la kisanii la Orijino Komedi

Hivi zile movie za Wazungu huwa wanatumiaje sare za kijeshi au polisi? au unakuta wanatumia vifaa vya kijeshi kabisa hadi ikulu, pentagoni au makao makuu ya CIA yanaonekana kabisa
wanatumiaje aisee
Movies nyingi za kijeshi na CIA zinakuwa zinafadhiliwa na Pentagon na CIA. Hii ni kusaidia kuuza image yao nje na ndani ya nchi.
 
Maskini Tanzania!Ndio maana wasanii wetu wa bongo movie wakiwa wanaigiza kama polisi huwa wanavaa "minguo"ya ajabu ajabu isiyo na uhalisia wa jeshi la polisi.Wao ilimradi tu rangi iwe kama ya mfuko wa cement,kumbe wanaogopa "beat".Sanaa yetu ya uigizaji ina miaka 100 mbele kufikia wenzetu walipofika.
 
Naona kauli mbinu ya Tanzania ya MARUFUKU inakuja juu kuliko ile ya Tanzania ya VIWANDA.
Sioni sababu ya jeshi la polisi kulivalia njuga jambo hili wakati vituoni kwao usiku wa manane ukipata tatizo hawatukaribishi na vituo vidogo vya mitaani vinafungwa saa kumi na moja ati nao wanaogopa.
 
Hivi zile movie za Wazungu huwa wanatumiaje sare za kijeshi au polisi? au unakuta wanatumia vifaa vya kijeshi kabisa hadi ikulu, pentagoni au makao makuu ya CIA yanaonekana kabisa
wanatumiaje aisee
swali lako na avatar yako are equal in magnitude but oposite in direction.
 
Polisi wafanye kazi zenye tija. Huko kanda ya kaskazini mashule yanachomwa moto na kutuweka roho juu kuhusu usalama wa wanetu mashuleni, kupoteza nguvu zao kushughulikia sare zilizovaliwa na the comedy ni kukosa kazi na dira!
 
Hivi wakuu kwa kawaida vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hua wana uniform na combati!! Sasa kwenye combati pale juu kwenye mkono wa kushoto hua panakuwa na kamba!!hivi wakuu zile kamba hua zinakuwa niza nini!!ni hilo tuu wakuu!!
 
Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Kufuatia kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.

Imetolewa na:

Advera John Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.



Baadhi ya wasanii wa Orijino Komedi wakiwa na MC Pilipili katika harusi ya mwenzao Masanja Mkandamizaji juzi Jumapili.

Wasamehewe jameni
 
Wafungwe miaka 7 jela kila mmoja na viboko kumi na viwili vya makalio...sita siku ya kuingia na sita siku ya kutoka wakawaoneshe wapenzi wao kuwa kuuza sura TBC sio maana yake na wewe ni mtukufu
 
Mnabwabwaja kuwaponda polisi kwa kuzingatia Sheria?!!! watanzania akili zetu ni kama mbayu mbayu.

Sheria ipo kabisa ambayo inazuia yeyote asiye askari kutumia/kuvaa sare/vifaa vya kijeshi pasipo kibali. Sasa Police wanaposimamia law compliance, kosa la Police ni lipi hapo?!!!

Mbona kwenye kumiliki silaha watu wanafuata taratibu zote za kisheria? ila kwenye Sare za kijeshi mnataka watu wajivalie tu eeh? Kuongoza watanzania ni shughuli pevu aisee.

Sio kila kinachofanyika marekani basi na hapa Tanzania eti kifanyike tu! Marekani Sheria yao inaruhusu, hapa Tanzania Sheria bado haijaruhusu. Pia mazingira ya Marekani (developed countries) sio sawa na mazingira ya nchi maskini kama Tanzania ambapo matukio ya kihalifu (mfano wizi na ujambazi) bado yanatutoa jasho!

Mnaacha kupaza sauti za ku-advocate for LAW REFORM kuhusu suala hilo ili Sheria irekebishwe, nyie mmekalia kuponda police eti wanatafuta kiki, mara ooh eti wakafanye vitu vingine vya maana, nyie watu vipi? mnatumia nini kufikiri?

Mara nyingi tu, hasa hapa Dar, tumeshuhudia matukio kadhaa ya Traffic feki na mapolice feki kusimama barabarani na kukamata RAIA, sasa hali itakuwaje watu wajivalie tu sare za kijeshi hovyo hovyo?

Watanzania tufike mahali tuwe na 'reasoning'. Tuacheni kufikiri na kuhoji kwa kutumia mihemko ya kisiasa. Tuwe tunatoa hoja with free mind.

Mtu unayeng'ang'ania kufananisha mazingira ya Marekani (nchi ambayo imefika hapo ilipo leo after more than 100 years) na mazingira ya Tanzania (nchi ambayo ina 50 years after Uhuru), nakuona punguani wa head.

Ofcoz ni vizuri kuiga best practices kutoka kwenye nchi zilizoendelea, lakini SIO kwa kuvunja Sheria zetu za nchi.

Tupazeni sauti kudai law reforms ili kuendana na kasi ya maendeleo ya karne hii. Na sio kupayuka tu kuwaponda law enforcers wakati wanatimiza majukumu yao.

Hao The Orijino Komedi wamevunja Sheria. Inabidi wawajibishwe accordingly.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom