DAR: Jengo la NHC zilipo ofisi za Tanzania Daima na Billicanas laanza kubomolewa

GeeM

JF-Expert Member
Apr 11, 2014
1,897
1,327


NHC imeanza kulibomoa jengo la Bilicanas lililoko katikati ya jiji baada ya kuwapa notisi ya masaa 24 wapangaji wake kulihama na kuondoa vitu.

Source: Channel 10

Mytake:
Kama ni sababu za kisiasa hili jambo halijakaa vyema hata kidogo.
 
Salam!

Jengo lililokuwa limepangishwa na Mh Freeman Mbowe limeanza kuvunjwa leo na wamiliki wa jengo hilo, Shirika la nyumba la Taifa NHC.

Ikumbukwe kwamba, jengo hilo ndilo palikuwa na club maarufu jijini Dsm na Africa Mashariki, Bilicanas Club.

Inasadikika Mbowe anadaiwa pango kiasi kikubwa cha pesa.

Source:Channel 10
 
Roho mbaya bwana ,hii ni dunia kuna siku tutakutana mbinguni tukiwa wafu wote wakati huo hatuwezi hata kuwatukana na kushambulia wengine na kuwalipa visasa maisha ni zaidi ya visasi na chuki

[HASHTAG]#ndoto[/HASHTAG] ya lema
 
Jengo la Club Bilicanas lililokuwa limepangishwa na Mh Mbowe toka NHC,Shirika la nyumba la Taifa, limeanza kuvunjwa leo baada ya wapangaji kupewa notisi ya saa 24.

NHC wanadai kwamba, jengo hilo lilikuwa linakaliwa kqa Mkopo wa mamilioni ya shilingi.

Chanzo:Chanel 10
 
Back
Top Bottom