Vifaa vyote vya Freeman Mbowe vilivyokamatwa jana na NHC vitauzwa baada ya siku 14 Ili kufidia deni

Mondoros

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
629
472

VIFAA vilivyokamatwa jana vya klabu ya usiku ya Bilicanas na ofisi ya gazeti la Tanzania Daima, vyote vinavyomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, vitapigwa mnada na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) siku 14 kuanzia jana, endapo atashindwa kulipa Sh. bilioni 1.2 za deni la pango la miaka 20.

Mbowe alikuwa mpangaji katika jengo la NHC lililopo makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Vyombo hivyo vilikamatwa jana na kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Mbowe kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi miwili ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia.

Meneja wa Kitengo cha Kukusanya Madeni kutoka NHC, Japhet Mwanasenga aliyekuwa akisimamia ukamataji wa vyombo hivyo, alisema Mbowe ana muda wa wiki mbili kuanzia jana kulipa deni la Sh. bilioni 1.172 vinginevyo vitapigwa mnada.

Vifaa vilivyokamatwa ni pamoja na kompyuta, meza na viti.

Alisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kumuondoa mteja wao, ikiwamo notisi na kwamba vifaa hivyo vitashikiliwa kwa muda huo wa wiki mbili.

“Tunashikilia vyombo kwa muda wa wiki mbili na iwapo atashindwa kulipa vitapigwa mnada na dalali, (mdaiwa) akishindwa kulipa anapangishwa mwingine,” alisema.

Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa majengo yake hivyo mteja ambaye anadaiwa ajiandae kuondolewa wakati wowote na kwamba zoezi la jana ni mwanzo tu.

Baadhi ya watu wamelihusisha tukio la kuondolewa Mbowe katika ofisi hizo na masuala ya kisiasa.Lakini Mwanasenga alisema uamuzi wa kumuondoa ofisi hizo hauna uhusiano na masuala ya kisiasa.

Alisema wapangaji wa jengo hilo wapo wengi pamoja na wadaiwa na kwamba baada ya mchakato huo kuanza mdaiwa yeyote atakayeshindwa kulipa kodi ataondolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari katikati ya wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanaa pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema. Notisi hiyo ilikuwa inaisha juzi.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadiawa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma.

"Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma," alisema Mchechu, hivyo "fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo."

Alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ujenzi wa nyumba za watumishi 300 hadi 500 mkoani Dodoma. Alisema ujenzi huo unatarajia kuanza mara moja na utachukua miezi 12.Kwa mujibu wa Mchechu, Sh. bilioni 60 za ujenzi wa nyumba hizo zitatokana na fedha za ndani.

Alisema shirika hilo limenunua ekari 240 eneo la Iyumbu, ekari saba Chamwino, nne Bahi na Chemba ekari nne pia ikiwa ni kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano kuhamia Dodoma.Alisema fedha nyingine zitapatikana baada ya nyumba 97 za shirika hilo zilizopo Medeli mjini Dodoma kuuzwa.
 
Kelele nyingi kumbe wakwepa kodi wakubwa.

Mabadiliko mabadiliko kumbe wao ndio wa kwanza kuwaibia wananchi!!!!!

Shame on you Chadema
 
Nasubiri kuona Wizara kama ya Mambo ya Nje inatolewa vifaa na vyombo nje...loading.

Hapo tutathibitisha hakuna siasa. Ila pia kwa nini uende kupambana na wa 1 billion alhali kuna mdeni hapo wa 2 billions???!!!

Tanzania eeeeh!!!
 
Kelele nyingi kumbe wakwepa kodi wakubwa.

Mabadiliko mabadiliko kumbe wao ndio wa kwanza kuwaibia wananchi!!!!!

Shame on you Chadema
Hahahhaaaaa! Kumbe akinya bata ndio kaharisha ila akinya kuku hakuna shida eeeeh! Kama taasisi za umma kibao tu zinadaiwa tena zinaliowa ruzuku na serikali na hazilipi pango. Unashagaa huyo mtu binafsi? Wa lumumba bhana.
 
Tayari tatizo la ajira limeongezeka. Watu wengi waliokuwa wameajiriwa au kutegemea maisha kupitia biashara za Mbowe wataathirika kwa kukosa kazi. Lakini mbona taasisi na mashirika ya serikali wameachwa pamoja na kuwa wanadaiwa zaidi ya Mbowe?!
 
Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadiawa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.
Hili la Mbowe linaweza kueleweka kirahisi (mkwepaji kama wakwepaji wengine au kuna mgogoro wa kibiashara).

Lakini hili la taasisi za serikali linahitaji maelezo ya kina. Kila mwaka inapitishwa bajeti naamini ikiwa ni pamoja na pesa za kulipia pango, je zilikuwa zinakwenda wapi? Tena hiyo Wizara ya Ujenzi, ilikuwa ni wizara ya Mheshimiwa Sana. Kunahitajika maelezo ya kina kutoka kwa serikali.
 
VIFAA vilivyokamatwa jana vya klabu ya usiku ya Bilicanas na ofisi ya gazeti la Tanzania Daima, vyote vinavyomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, vitapigwa mnada na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) siku 14 kuanzia jana, endapo atashindwa kulipa Sh. bilioni 1.2 za deni la pango la miaka 20.

Mbowe alikuwa mpangaji katika jengo la NHC lililopo makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Vyombo hivyo vilikamatwa jana na kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Mbowe kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi miwili ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia.

Meneja wa Kitengo cha Kukusanya Madeni kutoka NHC, Japhet Mwanasenga aliyekuwa akisimamia ukamataji wa vyombo hivyo, alisema Mbowe ana muda wa wiki mbili kuanzia jana kulipa deni la Sh. bilioni 1.172 vinginevyo vitapigwa mnada.

Vifaa vilivyokamatwa ni pamoja na kompyuta, meza na viti.

Alisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kumuondoa mteja wao, ikiwamo notisi na kwamba vifaa hivyo vitashikiliwa kwa muda huo wa wiki mbili.

“Tunashikilia vyombo kwa muda wa wiki mbili na iwapo atashindwa kulipa vitapigwa mnada na dalali, (mdaiwa) akishindwa kulipa anapangishwa mwingine,” alisema.

Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa majengo yake hivyo mteja ambaye anadaiwa ajiandae kuondolewa wakati wowote na kwamba zoezi la jana ni mwanzo tu.

Baadhi ya watu wamelihusisha tukio la kuondolewa Mbowe katika ofisi hizo na masuala ya kisiasa.

Lakini Mwanasenga alisema uamuzi wa kumuondoa ofisi hizo hauna uhusiano na masuala ya kisiasa.

Alisema wapangaji wa jengo hilo wapo wengi pamoja na wadaiwa na kwamba baada ya mchakato huo kuanza mdaiwa yeyote atakayeshindwa kulipa kodi ataondolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari katikati ya wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanaa pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema. Notisi hiyo ilikuwa inaisha juzi.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadiawa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma.

"Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma," alisema Mchechu, hivyo "fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo."

Alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ujenzi wa nyumba za watumishi 300 hadi 500 mkoani Dodoma.

Alisema ujenzi huo unatarajia kuanza mara moja na utachukua miezi 12.

Kwa mujibu wa Mchechu, Sh. bilioni 60 za ujenzi wa nyumba hizo zitatokana na fedha za ndani.

Alisema shirika hilo limenunua ekari 240 eneo la Iyumbu, ekari saba Chamwino, nne Bahi na Chemba ekari nne pia ikiwa ni kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano kuhamia Dodoma.

Alisema fedha nyingine zitapatikana baada ya nyumba 97 za shirika hilo zilizopo Medeli mjini Dodoma kuuzwa.
SAWA
ila isiwe ni kwa sababu ni mpinzani, tunataka tuone vilevile anauza vile vya wizara mbalimbali, na vya chama tawala maana nao wanadaiwa madeni sugu.
 
Kweli hivyo vimeza na viti vitafikisha 1.2b wanazomdai!? Ngoja tusubiri kuona kama sio siasa.

Hivyo vimeza na viti kuwekwa nje ni shinikizo ili walipe. Kama wakishindwa jengo litapangishwa mpangaji mwingine na kesi ya madai itafunguliwa kwa deni litakalobaki. Lakini hizo ni pesa za mboga kwa EL!
 
Hili la Mbowe linaweza kueleweka kirahisi (mkwepaji kama wakwepaji wengine au kuna mgogoro wa kibiashara).

Lakini hili la taasisi za serikali linahitaji maelezo ya kina. Kila mwaka inapitishwa bajeti naamini ikiwa ni pamoja na pesa za kulipia pango, je zilikuwa zinakwenda wapi? Tena hiyo Wizara ya Ujenzi, ilikuwa ni wizara ya Mheshimiwa Sana. Kunahitajika maelezo ya kina kutoka kwa serikali.

Waliopita walikuwa hawakusanyi kodi. Sasa serikali hii italipa madeni yote.
 
Hivyo vimeza na viti kuwekwa nje ni shinikizo ili walipe. Kama wakishindwa jengo litapangishwa mpangaji mwingine na kesi ya madai itafunguliwa kwa deni litakalobaki. Lakini hizo ni pesa za mboga kwa EL!
Umesoma Maelezo yaliyotolewa na shirika la Nyumba?
Maelezo ya kwako na ya kwao unataka tuamini yapi?
 
Back
Top Bottom