Dar inawapotezea watu muda

Bado hatufanani asee ndo mana ata mtu kutoka huko NY akija apo dar atafainanisha dar na kijiji flan cha huko marekani. Ukisema dar ni rahisi kutoka kmaisha utakuwa muongo mana ata hao wenye maisha yao waulize wamehustle kwa mda gan adi kufikia walipo sasa watakwambia ni safari ndefu sana. Na ndo mana dar malaya ni wengi sana na mashoga ni wengi sana pia...hawa wote walikuwa fresh km wew lakin mji uliwachapa hasa wakaona kurud nyumban how come na jiji halina shortcuts bora 'wagawe vya kugawa' na ndio huko huko mwanaume maisha yamemshinda anaona bora aolewe na mwanamke...'damn'. Dar mda mwing unapotea kweny mausafiri na kufanya kaz kwa ajili ya tumbo, vinguo, kodi, kupata mchongo tu adi ujuane na mzushi flan. Ndani ya mwaka mkoan mtu unaweza pata mchongo mzuri na fasta ukaanza kupandisha msingi lakin dar mwaka mzima unahangaika kupata watu wa kuwashobokea ili wakupe mchongo wa maana. Asee endeleen tu kusifia kuwa dar kuna magari na nyumba kali sisi tutakuja kununua ramani tujenge zetu huku mkoani
 
Kuna jamaa mkoa alikuwa na kajumba ka moja mkoa na Frem moja ya grocery plus Pikipiki sanlg nilikuwa namuona pedesheeeee,nilivokuja kuona wenye nazo nimecheka sana ile nyumba nikiiona Leo naona kama mabanda ya kufugia Kuku sema Haina ventilation za kutosha na tuvyumba tudogo
 
Afadhali ongezeko la watu lipungue.
 
Enheee...sasa uyo ni bora zaid kuliko wew ambaye upo dar alafu umepanga au unakaa kwa shemej yko
 
Hakika mkuu tatizo dar unapata kiasi unatumia zaidi yaani kama unapta 100 unatumia 95 inabaki 5 ndo kwa ajili ya maendeleo na bado kuna anasa kibao zinakusubiri,,lazima uzeeke huna kitu labda ukitaka kufanikiwa unatakiwa utumie nguvu kubwa na maarifa ya hali ya juu usisahau na kujituma zaidi....ila Mikoani mzunguko wa pesa mdogo ila ukiweza kuingiza elfu 20 kwa siku ukijipanga ndani ya miaka kadhaa utakuwa mbali
 
Majitu ya Dar bhana!
Yaani tajiri namba moja inakuhusu nini wewe unayeishi Gongo la Mboto?
Viwanja vikali wakati unalala sebuleni kwa shemeji yako inakusaidia nin?
Mikoa hatuwasalimii shemeji zetu.....wanaume wa Dar wanagongea sigara kwa shemeji zao!
Kwahio huko mikoani wote matajiri? Takwimu zimeonesha Dar ndio kuna nafuu ya maisha na huko mikoani hali ni mbaya sana.
 
Hii takwimu yako umeipataje? Kwamba tunatumia 95% ya pato letu....
 
Mawazo ya mtu. muoga muoga....
 
Hapo kwenye kutokulala vzr nakuunga mkono, nilikuwa naamka saa 10 alfajir kwenda kazini ili niwahi foleni na nilikuwa narudi home saa 4 usiku na hata ninachokipata sikioni hela yote inaishia kwenye matumizi ya kawaida nijasanuka
Hio ni wewe na mipangilio yako. Mimi naondoka saa mbili asubuhi saa tatu kasoro niko kibaruani. Kurudi hivyo hivyo 45mins tu.
 
Enheee...sasa uyo ni bora zaid kuliko wew ambaye upo dar alafu umepanga au unakaa kwa shemej yko
Sometimes reasoning kama hizi Huwa naziona za kijinga.Hivi Kwa mtu anayetafuta maisha kupanga ni tatizo? Wangapi wana nyumba zao lakini wao wenyewe wamepanga? Twende Kwa hiyo ya Shemeji hivi hao mashemeji wapo Dar au Kolomije? Kama wao wapo Dar kwanini wamefanikiwa.Kama wewe umeshindwa kuishi mjini usilazimishe Kila mtu ashindwe.
 
Kwahio huko mikoani wote matajiri? Takwimu zimeonesha Dar ndio kuna nafuu ya maisha na huko mikoani hali ni mbaya sana.
Dar watu wenye akili na uthubutu wanafanikiwa haraka mno,ila wenye tamaa na uvivu plus ubrothermen tutabaki kuilaani Dar
 
Kwenye kuzeeka umedanganya.Kuna Mzee mmoja anauza Kokoto tu hapa Dar akikuonyesha age mate wake Kijijini utashangaa.Age mate wake Kijijini wamechoka balaaaaaa wanaitwa mababu jamaa jamaa anadunda tu kitaa kama yupo kwenye late 30s kumbe yupo 50s huko
 
Kwenye kuzeeka umedanganya.Kuna Mzee mmoja anauza Kokoto tu hapa Dar akikuonyesha age mate wake Kijijini utashangaa.Age mate wake Kijijini wamechoka balaaaaaa wanaitwa mababu jamaa jamaa anadunda tu kitaa kama yupo kwenye late 30s kumbe yupo 50s huko
"Nimesema lazima uzeeke huna kitu" yaani mpaka unafika uzee usipokuwa makini huna hata pakuweka ubavu sijamaanisha kuwa utazeeka kwa shida ya kutafuta dar maana pesa zipo kila sehemu tatizo dar kila kitu cha kununua na gharama kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…