Wana JF,nachukua fursa hii kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia uvunjifu wa amani leo ktk jiji la DAR.
Mgambo wamefanya kazi kubwa sana,wamegawa dozi ya kufa mtu! big up mgambo.FFU ndio usiseme wamefanya kazi kubwa sana,polisi na askari kanzu nao wamefanya kazi kubwa sana leo kuhakikisha amani inarudi.Bila kusahau JWTZ nao wamefanya kazi kubwa sanan leo.
Mkuu,
Bado ni mapema sana kutoa pongezi!
Panapofuka moshi panaficha moto.
Unapowasha mkaa na kuutumia kwa shughuli kama kupika, baada ya muda moto unaisha, unaweza hata kuyamwaga majivu pembeni. Tulia saa moja, nenda kakanyage utaungua!
Siombei mabaya, na nitashukuru sana kama utulivu utaendelea.
Wasiwasi wangu na ninaamini siko peke yangu ni kuwa ile mbegu ya chuki iliyojengwa tayari imeshaota mizizi mirefu.
Kwa maana hii, zoezi la siku moja la kuonyesha nguvu mpaka kutumia JWTZ halitoshi kuing'oa mizizi ya chuki ambayo ilipandwa taratibu na kuwekwa mbolea na kumwagiwa maji na hao hao ambao leo hii wametuma majeshi.
Tatizo tulilo nalo Tanzania ni kubwa sana, na limetokana na kukosekana kwa dira ya kumwinua mwananchi.
Vijana hawana elimu ya kutosha.
Hawana ajira.
Hawana tumaini la maisha.
Hawa ndio wale wanaposikia kuna mkutano wa chama fulani, kutakuwa na T-shirt na kofia, na kutakuwa na Bongo flava, na pengine hata usafiri wa kwenda na kurudi, watatoka majumbani. Hicho kinakuwa kitu cha kufanya kupitisha siku, na pengine wataambulia hata mlo wa siku hiyo!
Hawa ndiyo wengi wao waliotoka majumbani mwao na kuanza kuchoma makanisa, na kuiba keyboards na computers. Sio wana dini wa kweli. Kitendo hicho kimewapa advebture ya siku hiyo, na wengine wameambulia vifaa wakiuza watapata pesa za kula siku mbili tatu.
Serikali imekosa sera ya msingi wa vijana hawa. Hawana tumaini la maisha.
Hawa akitokea mtu mmoja akawahamasisha kufanya lolote lile watafanya, na baadhi ya watu wanaojiita viongozi wa dini wanalijua hilo! Hawa bado wapo, na kukosa kwao matumaini bado kupo, na wale viongozi wachochezi bado wapo.
Hakuna wa kupongezwa hapa. Tunachotakiwa kufanya ni kubadili kabisa uongozi uliopo ili tulete uongozi mpya utakaotoa sera thabiti ya kumwinua mtu wa chini Tanzania. Hapo ndipo tukae na kupeana mkono wa pongezi, vinginevyo ni kufagia uchafu na kuufukia chini ya uvungu!