Dar iko shwari! Storm is over now!

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
Wana JF,nachukua fursa hii kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia uvunjifu wa amani leo ktk jiji la DAR.
Mgambo wamefanya kazi kubwa sana,wamegawa dozi ya kufa mtu! big up mgambo.FFU ndio usiseme wamefanya kazi kubwa sana,polisi na askari kanzu nao wamefanya kazi kubwa sana leo kuhakikisha amani inarudi.Bila kusahau JWTZ nao wamefanya kazi kubwa sanan leo.
 
Sio kuwakamata wote waliohusi ni kuwakamata waislamu wote waliohusika, maana waliohusika ni waislamu na wahuni wa mitaani ambao bila waislamu wasingeingia kwnye huo mkumbo
 
Tuombe Mungu amani irejee, vita haina macho. Bomu au risasi havichagui Mkristu au Muislam.
 
Wana JF,nachukua fursa hii kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia uvunjifu wa amani leo ktk jiji la DAR.
Mgambo wamefanya kazi kubwa sana,wamegawa dozi ya kufa mtu! big up mgambo.FFU ndio usiseme wamefanya kazi kubwa sana,polisi na askari kanzu nao wamefanya kazi kubwa sana leo kuhakikisha amani inarudi.Bila kusahau JWTZ nao wamefanya kazi kubwa sanan leo.

Mkuu,
Bado ni mapema sana kutoa pongezi!
Panapofuka moshi panaficha moto.
Unapowasha mkaa na kuutumia kwa shughuli kama kupika, baada ya muda moto unaisha, unaweza hata kuyamwaga majivu pembeni. Tulia saa moja, nenda kakanyage utaungua!
Siombei mabaya, na nitashukuru sana kama utulivu utaendelea.
Wasiwasi wangu na ninaamini siko peke yangu ni kuwa ile mbegu ya chuki iliyojengwa tayari imeshaota mizizi mirefu.
Kwa maana hii, zoezi la siku moja la kuonyesha nguvu mpaka kutumia JWTZ halitoshi kuing'oa mizizi ya chuki ambayo ilipandwa taratibu na kuwekwa mbolea na kumwagiwa maji na hao hao ambao leo hii wametuma majeshi.

Tatizo tulilo nalo Tanzania ni kubwa sana, na limetokana na kukosekana kwa dira ya kumwinua mwananchi.

Vijana hawana elimu ya kutosha.
Hawana ajira.
Hawana tumaini la maisha.
Hawa ndio wale wanaposikia kuna mkutano wa chama fulani, kutakuwa na T-shirt na kofia, na kutakuwa na Bongo flava, na pengine hata usafiri wa kwenda na kurudi, watatoka majumbani. Hicho kinakuwa kitu cha kufanya kupitisha siku, na pengine wataambulia hata mlo wa siku hiyo!

Hawa ndiyo wengi wao waliotoka majumbani mwao na kuanza kuchoma makanisa, na kuiba keyboards na computers. Sio wana dini wa kweli. Kitendo hicho kimewapa advebture ya siku hiyo, na wengine wameambulia vifaa wakiuza watapata pesa za kula siku mbili tatu.

Serikali imekosa sera ya msingi wa vijana hawa. Hawana tumaini la maisha.

Hawa akitokea mtu mmoja akawahamasisha kufanya lolote lile watafanya, na baadhi ya watu wanaojiita viongozi wa dini wanalijua hilo! Hawa bado wapo, na kukosa kwao matumaini bado kupo, na wale viongozi wachochezi bado wapo.

Hakuna wa kupongezwa hapa. Tunachotakiwa kufanya ni kubadili kabisa uongozi uliopo ili tulete uongozi mpya utakaotoa sera thabiti ya kumwinua mtu wa chini Tanzania. Hapo ndipo tukae na kupeana mkono wa pongezi, vinginevyo ni kufagia uchafu na kuufukia chini ya uvungu!
 
Pamoja na hayo kuweni makini, punguwani hata akichapwa anaweza kushawishiwa na wajanja afanye kufuru usiku, halafu usikilizie kesho!!
Ila big up kwa vijana ama kikosi cha kazi, na pengine niwaase wasifikiri kazi wamemaliza wakalala makwao, bali wahakikishe usalama wa raia na mali zao.
 
Wana JF,nachukua fursa hii kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia uvunjifu wa amani leo ktk jiji la DAR.
Mgambo wamefanya kazi kubwa sana,wamegawa dozi ya kufa mtu! big up mgambo.FFU ndio usiseme wamefanya kazi kubwa sana,polisi na askari kanzu nao wamefanya kazi kubwa sana leo kuhakikisha amani inarudi.Bila kusahau JWTZ nao wamefanya kazi kubwa sanan leo.
unapongeza wakati bado hujamaliza kuvuka mto?tafakari.
 
Mkuu,
Bado ni mapema sana kutoa pongezi!
Panapofuka moshi panaficha moto.
Unapowasha mkaa na kuutumia kwa shughuli kama kupika, baada ya muda moto unaisha, unaweza hata kuyamwaga majivu pembeni. Tulia saa moja, nenda kakanyage utaungua!
Siombei mabaya, na nitashukuru sana kama utulivu utaendelea.
Wasiwasi wangu na ninaamini siko peke yangu ni kuwa ile mbegu ya chuki iliyojengwa tayari imeshaota mizizi mirefu.
Kwa maana hii, zoezi la siku moja la kuonyesha nguvu mpaka kutumia JWTZ halitoshi kuing'oa mizizi ya chuki ambayo ilipandwa taratibu na kuwekwa mbolea na kumwagiwa maji na hao hao ambao leo hii wametuma majeshi.

Tatizo tulilo nalo Tanzania ni kubwa sana, na limetokana na kukosekana kwa dira ya kumwinua mwananchi.

Vijana hawana elimu ya kutosha.
Hawana ajira.
Hawana tumaini la maisha.
Hawa ndio wale wanaposikia kuna mkutano wa chama fulani, kutakuwa na T-shirt na kofia, na kutakuwa na Bongo flava, na pengine hata usafiri wa kwenda na kurudi, watatoka majumbani. Hicho kinakuwa kitu cha kufanya kupitisha siku, na pengine wataambulia hata mlo wa siku hiyo!

Hawa ndiyo wengi wao waliotoka majumbani mwao na kuanza kuchoma makanisa, na kuiba keyboards na computers. Sio wana dini wa kweli. Kitendo hicho kimewapa advebture ya siku hiyo, na wengine wameambulia vifaa wakiuza watapata pesa za kula siku mbili tatu.

Serikali imekosa sera ya msingi wa vijana hawa. Hawana tumaini la maisha.

Hawa akitokea mtu mmoja akawahamasisha kufanya lolote lile watafanya, na baadhi ya watu wanaojiita viongozi wa dini wanalijua hilo! Hawa bado wapo, na kukosa kwao matumaini bado kupo, na wale viongozi wachochezi bado wapo.

Hakuna wa kupongezwa hapa. Tunachotakiwa kufanya ni kubadili kabisa uongozi uliopo ili tulete uongozi mpya utakaotoa sera thabiti ya kumwinua mtu wa chini Tanzania. Hapo ndipo tukae na kupeana mkono wa pongezi, vinginevyo ni kufagia uchafu na kuufukia chini ya uvungu!

umenena mkuu,naamini waliondamana leo sio waislam tu lazima kuna wakristu na wapagani.ambao wanaamini watapata chochote kupitia vurugu hizi.!
 
Wana JF,nachukua fursa hii kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia uvunjifu wa amani leo ktk jiji la DAR.
Mgambo wamefanya kazi kubwa sana,wamegawa dozi ya kufa mtu! big up mgambo.FFU ndio usiseme wamefanya kazi kubwa sana,polisi na askari kanzu nao wamefanya kazi kubwa sana leo kuhakikisha amani inarudi.Bila kusahau JWTZ nao wamefanya kazi kubwa sanan leo.

"The storm is over, i can see clearly Now.!'' iyo ni beti ya wimbo wa gwiji wa Musiki wa Marekani R.Kelly kama inavyobainisha katika Head ya uzi wako.
Mkuu.., Lakini mimi naona kama Nguvu nyingi imetumika,nikiangalia kwa haraka haraka vyombo vyote Muhimu vimetumika kuanzia Askari kanzu, polisi wa kawaida, FFU hadi wapiganaji wetu ( jwtz) kudhibiti kundi dogo la wahuni kama wengi wanavyowaita katika vurugu hizo.

Mimi nadhani kuwe na long term solution katika kumaliza vurugu hizo kwa serikali kuwangalia the root coz na siyo the sympton katika kushughulikia tatizo hilo...vipo vyombo kadhaa vya habari hapa Nchini ambavyo kwa makusudi vinachochea katika kuleta hamasa za kuvuruga Amani na utulivu wa jamii ya watanzania.., Serikali kupitia wizara ya Habari ina mamlaka ya kufuta au kufungia chombo chochote kinacho hatarisha amani kwa kuleta au kutangaza habari za uchochezi....,lakini bado tuu tunaona hali inakuwa mbaya na ndio matokeo yake aya.
 
Kiongozi wa uamsho zanzibar ameipa serikali masaa kueleza bossi wao alipo vinginevyo watajua la kufanya hili nalo limekaaje wadau?
 
Back
Top Bottom