Dar: Halima Mdee, Bulaya, Jesca Kishoa, Meya Jacob,Henry Kilewo na wengine wafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kufanya fujo gereza la Segerea

Mbona ndugu yako polepole alienda tena na makamera kabisa. Alienda kufanya nini?

Nilikuwa natafuta jibu lake kuhusu hili swali lako, uso wake kidogo umeumbwa na soni, roho yake imemsuta kulijibu hili..

Ila daah, kweli yule bwana ni mkaidi..
WhatsApp Image 2020-03-22 at 19.29.30.jpeg
 
Watu ambao wamo kwenye hatari kubwa ni ester bulaya na mdee, najua hao kama watakutwa na hatia, basi watakula mvua zakutosha, maana mahakama inatabia yakuangalia historia ya mtuhumiwa ukizingatia wametoka kuitukana mahakama juzi juzi tu.

Yangu macho, Ni muda wa wanasheria kupiga pesa ndani ya chadema! Uwiiiii.
 
Ingetumika busara tu kwenye jambo hili, ila kwa vila kila mtu kajaliwa 'busara' zake basi na iwe hivi!
 
maxresdefault-1-620x308.jpg

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe na wenzake 14, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya vurugu katika gereza la Segerea.
Kwenye kundi hilo, wapo wajumbe wanne wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na wanachama 10 wa chama hicho.
Bmali na Mdee, wengine ni Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Jesca Kishoa, Mbunge Viti Maalumu; Boniface Jacob, Meya wa Ubungo na Henry Kilewo, mjumbe wa kamati hiyo, wamefikishwa mahakamani hapo leo tarehe 23 Machi 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema katika ukurasa wake wa Twitter, watuhumiwa hao walitakiwa kuripoti polisi leo, lakini wamepelekwa mahakamani.

Mdee na wenzake wanatuhumiwa kufanya fujo katika Gereza la Segerea, walipokwenda kumtoa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, aliyekuwa anatumikia kifungo cha miezi mitano gerezani hapo.

Kwa mujibu wa Chadema, hadi sasa watuhumiwa hao hawajapandishwa kizimbani.
 
"Uvumilivu wetu siyo UWOGA, sasa imetosha" Freeman Mbowe aliongea kwa kujiamini sana
Sisi kama vijana tunaendelea kujiandaa
#nohatenofear
#tumehuruyauchaguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom