Mdee na Wenzake wawasili mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri lao

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Wabunge wa viti maalum akiwemo Halima Mdee na wenzake leo Ijumaa wamefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuhudhuria kesi waliyoifungua mahakamani hapo ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mdee na wenzake wamevuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 27, 2020 kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Mbali na Mdee, wengine ni Grace Tendega, Esther Matiko, Ester Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa na Nusrat Hanje.

Shauri hilo bado halijaanza kusikilizwa ambapo mawakili wote wa upande wa Chadema na wa akina Mdee wameitwa kwa Jaji Cyprian Mkeha kwa ajili ya taarifa kwa ufupi.

Hali ilivyo katika Mahakama hiyo kuwa wanachama wamejitokeza kwa wingi kwa pande zote mbili kwa akina Mdee na Chadema wakiwa wako kwenye vikundi mbalimbali

Kwa upande wa wanachama wa Chadema wamejitokeza wengi huku wengine wamevaa sare za chama.

Wakili wa Chadema, Peter Kibatala aliwasilisha ombi mbele ya Jaji Mkeha kuwa atoe hati ya wito kwa wabunge hao ili waje kuwahoji mahakamani hapo kuhusiana na viapo vyao.

Jaji Mkeha alikubaliana na ombi hilo na kueleza hati za wito zitolewe kwa waleta maombi saba (Mdee na wenzake) kwa ajili ya kuhojiwa.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: SHAURI LA HALIMA MDEE NA WENZAKE LAAHIRISHWA


Usikilizwaji wa Shauri la Halima Mdee na Wenzake katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam la kupinga kuvuliwa Uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeahirishwa hadi Septemba 2

Katika shauri hilo, wanasiasa hao wameiomba Mahakama kupitia upya Mchakato wa kuvuliwa Uanachama na pia itazame hoja walizoziwasilisha na kuwabakiza na Ubunge wao.
 
Hii kesi ni ya wazi ama siri? kama ni wazi haya tupeni updates basi vip goma limeshaanza ??
 
Yaani hii nchi ita laaniwa hadi Yesu arudi. Wanyonge tunaibiwa hela kwa tozo ili wengine wakae bungeni na kulipiwa gharama za mawakili sie tuna teseka kwa ajili ya Ccm kulinda maslahi yao.

Yaani una lipwa mshahara kupitia bank umesha lipa kodi zote, una toa mshahara benki unakatwa tozo.

Unaweka pesa uliyo toa benki ili umtumie mama yako ina katwa tozo.. Ili Halima alipwe mshahara ambao hauna kodi.

Viongozi wa serikali ya Ccm nawaambieni, mtafika Mbunguni mmechoka sana. Take it from me
 
Kufikia 2025 inabaki almost miezi 30, hapo shauri likienda mwendo wa kinyonga manake Hawa Waheshimiwa wataendela kuwa Wabunge hadi 2025.

Wacha waendelee kulamba Asali
 
Back
Top Bottom