Dar: Halima Mdee, Bulaya, Jesca Kishoa, Meya Jacob,Henry Kilewo na wengine wafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kufanya fujo gereza la Segerea

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,445
2,000
Meya Boniface Jacob ni mmoja kati watu 15 waliofikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi hii leo‬.

‪Bado haijajulikana wanashtakiwa kwa kosa gani‬.

Wametoka Kituo cha Polisi Stakishari

IMG_0378.jpg


======
UPDATE:

Kwenye hati ya mashtaka inaonekana kesi itakuwa washtakiwa 29.

Wabunge watatu wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini) na Jesca Kishoa (Viti Maalumu) nao wameunganishwa kwenye kesi pamoja na Meya Jacob

-----
HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe na wenzake 14, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya vurugu katika gereza la Segerea.
Kwenye kundi hilo, wapo wajumbe wanne wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na wanachama 10 wa chama hicho.
Mbali na Mdee, wengine ni Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Jesca Kishoa, Mbunge Viti Maalumu; Boniface Jacob, Meya wa Ubungo na Henry Kilewo, mjumbe wa kamati hiyo, wamefikishwa mahakamani hapo leo tarehe 23 Machi 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema katika ukurasa wake wa Twitter, watuhumiwa hao walitakiwa kuripoti polisi leo, lakini wamepelekwa mahakamani.

Mdee na wenzake wanatuhumiwa kufanya fujo katika Gereza la Segerea, walipokwenda kumtoa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, aliyekuwa anatumikia kifungo cha miezi mitano gerezani hapo.

Kwa mujibu wa Chadema, hadi sasa watuhumiwa hao hawajapandishwa kizimbani.

======
UPDATE:

Hati ya Mashtaka

BE9EBADC-87FE-4635-A091-7EC927E876FE.jpeg

7CF69F46-C885-44D6-869D-FC04BF12AC22.jpeg

34494E31-E3D1-4245-9AC4-7BA4B650A562.jpeg

1800EC93-CF7E-43D4-B736-027BE87F01EC.jpeg

FC743F9A-3625-435C-BABB-E6098BC1DF62.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom