mapato ya soko la mitumba ashanti au?Dsm wanajua haki zao hawawezi kuingizwa mkenge wa kijinga kama wengine wa huko mikoani. Jimbo kama la Ilala linachangia 80% ya mapato ya serikali ya kila mwezi, sasa unafikiri wa kuja anaweza kulishika hilo jimbo? Hata CHADEMA japokuwa makao makuu yao yapo hapa dar waliogopa kuliingia hilo jimbo
mtakalia wakuja wakuja.... Haya wakunyumba wanawaingiza mjini sisi wakuja haohao wanatusaidia... Go Mnyika go... Go wakuja go!
I care about maendeleo hata yakiletwa na wakuja nayakumbatia!
Wana JF
Kwa mtazamo wangu naona watu wa mikoani wamejitambua muda mrefu na hata kuchagua wabunge kutoka vyama vya upinzani tokea mabunge yaliyopita(ukiacha kawe na ubungo 2010),ukiangalia msukumo uliopo arusha,mara,mbeya ,kigoma,songea,kagera,mwanza nk utaliona hilo.Je ni kwanini wana dar hawana mwamko sana wa kimapinduzi na ukizingatia wajanja wengi wapo hapo?
Nawasilisha ukumbini
80% unaumwa wewe! kwani viwanda Dar vipo wap?Dsm wanajua haki zao hawawezi kuingizwa mkenge wa kijinga kama wengine wa huko mikoani. Jimbo kama la Ilala linachangia 80% ya mapato ya serikali ya kila mwezi, sasa unafikiri wa kuja anaweza kulishika hilo jimbo? Hata CHADEMA japokuwa makao makuu yao yapo hapa dar waliogopa kuliingia hilo jimbo
Mawazo ya kijinga au hujui maana ya 80%.Dsm wanajua haki zao hawawezi kuingizwa mkenge wa kijinga kama wengine wa huko mikoani. Jimbo kama la Ilala linachangia 80% ya mapato ya serikali ya kila mwezi, sasa unafikiri wa kuja anaweza kulishika hilo jimbo? Hata CHADEMA japokuwa makao makuu yao yapo hapa dar waliogopa kuliingia hilo jimbo
Wana JF
Kwa mtazamo wangu naona watu wa mikoani wamejitambua muda mrefu na hata kuchagua wabunge kutoka vyama vya upinzani tokea mabunge yaliyopita(ukiacha kawe na ubungo 2010),ukiangalia msukumo uliopo arusha,mara,mbeya ,kigoma,songea,kagera,mwanza nk utaliona hilo.Je ni kwanini wana dar hawana mwamko sana wa kimapinduzi na ukizingatia wajanja wengi wapo hapo?
Nawasilisha ukumbini
hivi dodoma, singida,arumeru,monduli,simanjiro kuna uswahili?
Slogan yao
Kusoma hatujasoma,
Nguvu hatuna,
Pesa hatuna,
Kazi hatuna,
Hata majungu na fitna tushindwe?
Alituletea Nyerere, sasa tutahakikisha hawashiki, especially Ilala, Kinondoni Temeke. Kwingine huko ni nje ya Dar.
Madogo wa juzi hao hawajui kama temeke,kigamboni zilikua upinzani wao wanaona kama chadema ndio imeanza kuchukua majimbo dar!Si kweli Kuwa Dar-es-salaam hawana mwamko kama kumbukumbu zako zinafanya kazi, majimbo ya Kigamboni na Temeke yalikuwa ya mwanzo ktk miaka ya 90 kutoa wabunge toka vyama vya CUF na NCCR.mageuzi(Lyatonga Mrema)! huku majimbo mengine yalileta vurugu mpaka uchaguzi kurudiwa mara 2 mwaka 1995!
Dar ni jiji la kwanza bara kuwa na harakati za ukombozi pale wananchama wa CUF walipokuwa mstari wa mbele kuonesha ungangari mbele ya CCM na kusababisha hata Polisi kuuwa waandamanaji wa CUF mwaka 2001 sambamba na Visiwani! lakini la kusikitisha wenzao wa vyama vingine kama CDM waliwasusia kichinichini na kueneza propaganda kuwa CUF ni chama cha kidini na kuwavunja moyo wana CUF na kuiacha DAR iwe na upinzani mmoja tu CUF!
Sasa kwa kweli sijui CDM wakati huo labda walikuwa na muafaka wa siri na CCM ndio maana uchaguzi wa 2000 CUF walipoteza jimbo la kigamboni huku jimbo kama la Temeke likiwa na taharuki na uchakachuwaji!
Kwa hiyo ndugu yangu usiwalaumu wakazi wa Dar bure, kwani walikuwa mstari wa mbele kutaka kuleta mabadiliko lakini wameangushwa na ubinafsi wa baadhi ya vyama vya siasa!