mrskhoory
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 220
- 112
Basi ngoja nije PM tufahamiane zaidi.
Uchelewe uchekwe...lol
Basi ngoja nije PM tufahamiane zaidi.
unataka nitembelee mangapi ??
Jaribu Mogadishu, Nairobi, Brazzaville, Bujumbura, Addis Ababa, Maputo angaia vigezo vyote hivyo then uone Dar iko wapi. We may be we have bad city, but may not be the worst.
Kiufupi maisha ya Dar sio poa ila Dar ndio mji wa maajabu zaidi duniani kwanini nasema hivi ?
Utakuta kijana hana kazi hana chanzo cha mapato chochote ila ana smartphone ya gharama anakula vizuri na analala kama kawa na maisha yanaendelea huku tunasema mwanaume halali njaa ila anachelewa kula hata saa saba usiku tutakula tu kama hujaishi kwetu huwezi kujua.
Utamkuta kabinti hakana mbele wala nyuma kanavaa vizuri kanapendeza hakana kazi wala mwanaume wa maana usishangae wana vikundi vyao wanaazimana nguo yaani inaitwa kauka nikuvae leo anavaa huyu kesho yule asubuhi huyu mchana yule hivyo ndio wanavyoishi mimi nikiwa ni shuhuda
Mpaka leo sikijui kituo hasa cha tandika kipo wapi nikipanda gari unaweza kushtuka upo serengeti linageuza watu hawajashuka sijui wamepandia wapi cha msingi wewe sema hapo kona nishushe
Kila mtu ana ndoto za kuwa na gari ila hana malengo ya kupata fedha za kununua magari nikiwasikiliza huwa naishia kucheka nitafanyaje sasa ? Hayo ndio maisha tuliochagua kuishi
Aliyengonoka na mademu wengi huku kwetu ndio mjanja kuliko wote hapo akikaa atakupointia kila apitaye huyu tayari yule nishapita
ndio maana sijawahi kutongoza demu wa mtaa wetu amini usiamini sitaki kuja siku unasikia yule demu ana umeme kichwa kikakuuma na wewe kwenye list yake upo ninao ushahidi
Kali zaidi kila demu yupo chuo hata kama alifeli form foo hapa ndio napolipenda hili jiji wale wanaosema bora wangezaliwa ulaya nawashangaa sana maajabu yote haya bado nipakimbie dar ??
Kinachonichosha ni pale konda wa daladala anapotangaza, "Gari nyeupee, njoo ukae!" Ajabu ni kuwa pamoja na kwamba abiria wananing'inia mlangoni, watu watakanyagana kulikimbilia basi baada ya kuambiwa "njoo ukae".
Ulivyojibu ni kama mtoto kaleta ripoti kawa wa 40 kati ya watoto 45. Na akaanza kujitetea kama hivyo..
Mkuu majiji yote makubwa hapa Duniani maisha huwa ni ghali sana ukilinganisha na miji midogo,ila hilo la uchafu na foleni ya Magari linakera sana.
polisi wanavaa kama wako vitani ..always hahahaha halafu wanachofanya ni kusimamisha kuomba leseni...wamepakizana kwenye vi piki piki vibayaaaaaaaa na bunduki
Dar kweli ni moja ya maajabu na kivutio duniani!
Hata profesa wa kichina duniani anapatikana darisalam.