Mcharo son
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 6,280
- 5,258
unaambiwa dar ndo tunaongoza kwa foleni worldwide
jioni wakati wa kutoka maofisini. matrafiki wanazuia magari yasiingie mjini ili kuwapisha hawa wenye magari wanaotoka maofisini mjini hususan POSta wasipate shida. Kazi kwenu nyie wafanyakazi msiokuwa na magari binafsi mnaotegemea usafiri wa umma daladala. mtalazimika kutembea kuyafuata mabasi kule yalipozuiliwa au kusubiri mpaka wenzenu wapite na magari yao ndio mkanyagane kupanda basi. MFANO HALISI BARABARA YA KILWA MAENEO YA BANDALI PITA PALE SAA9 kuingia mjini. utazuiwa mpaka saa11. abilia wa posta itawabidi watembee mpaka bandari kupanda basi zilizo foleni kuingia mjini ili waje wageuze na basi kukwepa kugombania na kupata siti. Nauli ni mara 2. (lini utapata na weye gari katika hali hii)
mwisho wa siku maisha yanaendelea hakuna wa kulalamika. kwa nini daladala zinazuiwa kipindi hiko kwani ndio zingebeba wafanyakazi wasiokuwa na kipato cha kununua magari.
UKIPITA MSAFARA NDIO mwisho wa yote hilo foleni litakaloachwa. CCM mbele kwa mbele??? how
viongozi gani wa ccm atajitokeza kuwakanya maaskali waliobuni miundo mbinu ya kuwapendelea wakubwa au wenye pesa.
WOTE TUNAJENGA NCHI KWA NINI WAKATI WA KURUDI MAKWETU WANAPENDELEWA WALE WENYE KIPATO waliomudu kununua gari zao. HATA sie tulioshonana kwenye basi. joto. hewa nzito. mwenzio akipumua mnavumiliana hewa hiyo hiyo harafu dereva wa basi akijaribu kupita njia ya mkato isio na foleni kuwawahisha ATAKAMATWA. MTASHUSHWA MTEMBEE KWA MGUU AU MSUBILI LINGINE. Kwa nini mabasi haya yaliobeba watu WENGI yasipewe kipaumbele kwenye foleni. HASIRA YANGU nitaionyesha OCTOBA 25