Dar es Salaam ndio jiji lenye maajabu zaidi duniani

Dar es Salaam ndio jiji lenye maajabu zaidi duniani

MO11

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
19,670
Reaction score
41,847
Kiufupi maisha ya Dar sio poa ila Dar ndio mji wa maajabu zaidi duniani kwanini nasema hivi ?

Utakuta kijana hana kazi hana chanzo cha mapato chochote ila ana smartphone ya gharama anakula vizuri na analala kama kawa na maisha yanaendelea huku tunasema mwanaume halali njaa ila anachelewa kula hata saa saba usiku tutakula tu kama hujaishi kwetu huwezi kujua.

Utamkuta kabinti hakana mbele wala nyuma kanavaa vizuri kanapendeza hakana kazi wala mwanaume wa maana usishangae wana vikundi vyao wanaazimana nguo yaani inaitwa kauka nikuvae leo anavaa huyu kesho yule asubuhi huyu mchana yule hivyo ndio wanavyoishi mimi nikiwa ni shuhuda

Mpaka leo sikijui kituo hasa cha tandika kipo wapi nikipanda gari unaweza kushtuka upo serengeti linageuza watu hawajashuka sijui wamepandia wapi cha msingi wewe sema hapo kona nishushe

Kila mtu ana ndoto za kuwa na gari ila hana malengo ya kupata fedha za kununua magari nikiwasikiliza huwa naishia kucheka nitafanyaje sasa ? Hayo ndio maisha tuliochagua kuishi

Aliyengonoka na mademu wengi huku kwetu ndio mjanja kuliko wote hapo akikaa atakupointia kila apitaye huyu tayari yule nishapita
ndio maana sijawahi kutongoza demu wa mtaa wetu amini usiamini sitaki kuja siku unasikia yule demu ana umeme kichwa kikakuuma na wewe kwenye list yake upo ninao ushahidi

Kali zaidi kila demu yupo chuo hata kama alifeli form foo hapa ndio napolipenda hili jiji wale wanaosema bora wangezaliwa ulaya nawashangaa sana maajabu yote haya bado nipakimbie dar ??
 
Uko sawa mkuu,dar ni jiji la ajabu duniani,mie nimetembelea majiji mengi,dar ndo kibo cha yote,na nairobi pia.
 
Da kwenye daladala kila mtu kanuna ukimwambia sogea tu unaambulia mvua ya maneno,ngoja nikomae na kukata mkaa nije nipate hata kapasso!
 
Kiufupi maisha ya Dar sio poa ila Dar ndio mji wa maajabu zaidi duniani kwanini nasema hivi ?
??

Sawa kabisa, katika kuongezea nafikiri pia hili ni moja ya majiji yanayoshangaza mno, utakuata mfanyakazi wa serikali, kipatoo chake cha chini au kati, lakini kajenga majumba 3 hata 4 kwa mshahara na marupurupu yasiozidi hata laki tano! Bado utasikia ana shamba, magari matatu, na kajenga mkoani alipotoka! Unajiuliza huyu hela katoa wapi na huko anapofanya kazi ina maana hawayaoni haya yote na kumchukulia hatua kali za kisheria ikiwezekana kumfilisi kabisa..
Ni jiji la ajabu ambapo sifa ni kuwa mwizi ofisini, unaonekana kama "role model"!
Ni jiji la ajabu sana hasa ukizingatia utaona polisi wengi wako kwenye pikipiki wamevalia kama wanaenda vitani, lakini utashangaa mbona kama kazi yao kubwa ni kusimamisha bajaj, bodaboda, daladala na carriers! Sasa Sijui trafiki polisi wafanye kazi gani!
Ni jiji la ajabu mno kuona trafiki polisi kazi yao kubwa ni kusimamisha magari na kuomba leseni za udereva na za gari, hii kazi inatakiwa iwe inafanywa na TRA, kwamba huwezi kupata bima kama huna motor vehicle licence iliolipiwa, na pia basi wawe na vyombo maalum barabarani vya kusoma namba ambazo zitaweza kuwaeleza kama hizo gari zina vibali vyote..
Kwa kweli hili jiji hata mie linanishangaza, ukienda kula kwenye migahawa au bar, vyakula na vinywaji vina bei tofauti, mhudumu ana bei yake, counter kuna bei yake na ukienda jikoni kabisa kuna bei yake!
Lazima hata wageni watakuwa wanaburudika na vioja vyetu, taa barabarani hazifuatwi kisa magari machache, honi za magari zinapigwa kama mziki, watu tunashindana kuweka sauti za juu kabisa za mziki kwenye daladala, madukani, mtaani, majumbani, bodaboda, bajaj n.k.
Ni jiji pekee lenye matangazo mengi mno na yaliyosheni ya waganga wa kienyeji, hasa wanaotibu mambo ya mapenzi, utajiri, akili na ngiri!
Hili jiji sitalikimbia sababu napokuwa barabarani huwa nacheka mwenyewe kila wakati kwa jinsi lilivyopambwa na na magari yenye engine kubwa (mashangingi)hali tukijuwa hii nchi ni maskini, haya mashangingi kuyahudumia ni ghali mno sasa huwa nastaajabu nikiona wafanyakazi wa TRA, Hazina, BOT, TPDC na mengine mengi tu wakiyaendesha, najiuliza na kutaka kuamini kuwa basi mishahara na marupurupu serikalini yatakuwa ni mamilioni kwa mwezi!
Vioja huwa haviishi, hasa unaposikia Muhimbili kuna watu wanajipatia ajira kwa kuuza damu zao tu! Hii sijaona au kusikia sehemu zingine duniani!
Kama hamlipendi hili jiji la DAR shauri yenu ila mimi niko addicted nalo...
 
mie mweee kila siku nikitembea barabari lazima uone chupi za watu mweee kule kwetu hata mwaka chupi huoni maungoni mwa ntuu
 
Kiufupi maisha ya Dar sio poa ila Dar ndio mji wa maajabu zaidi duniani kwanini nasema hivi ?

Utakuta kijana hana kazi hana chanzo cha mapato chochote ila ana smartphone ya gharama anakula vizuri na analala kama kawa na maisha yanaendelea huku tunasema mwanaume halali njaa ila anachelewa kula hata saa saba usiku tutakula tu kama hujaishi kwetu huwezi kujua.

Utamkuta kabinti hakana mbele wala nyuma kanavaa vizuri kanapendeza hakana kazi wala mwanaume wa maana usishangae wana vikundi vyao wanaazimana nguo yaani inaitwa kauka nikuvae leo anavaa huyu kesho yule asubuhi huyu mchana yule hivyo ndio wanavyoishi mimi nikiwa ni shuhuda

Mpaka leo sikijui kituo hasa cha tandika kipo wapi nikipanda gari unaweza kushtuka upo serengeti linageuza watu hawajashuka sijui wamepandia wapi cha msingi wewe sema hapo kona nishushe

Kila mtu ana ndoto za kuwa na gari ila hana malengo ya kupata fedha za kununua magari nikiwasikiliza huwa naishia kucheka nitafanyaje sasa ? Hayo ndio maisha tuliochagua kuishi

Aliyengonoka na mademu wengi huku kwetu ndio mjanja kuliko wote hapo akikaa atakupointia kila apitaye huyu tayari yule nishapita
ndio maana sijawahi kutongoza demu wa mtaa wetu amini usiamini sitaki kuja siku unasikia yule demu ana umeme kichwa kikakuuma na wewe kwenye list yake upo ninao ushahidi

Kali zaidi kila demu yupo chuo hata kama alifeli form foo hapa ndio napolipenda hili jiji wale wanaosema bora wangezaliwa ulaya nawashangaa sana maajabu yote haya bado nipakimbie dar ??

ubaya hadhi ya vyuo omeshuka hata madrsa ni chuo
awe udereva chuo. ni tabu tu
 
Kinachonichosha ni pale konda wa daladala anapotangaza, "Gari nyeupee, njoo ukae!" Ajabu ni kuwa pamoja na kwamba abiria wananing'inia mlangoni, watu watakanyagana kulikimbilia basi baada ya kuambiwa "njoo ukae".
 
Dar es salaam ndio jiji pekee duniani ambalo takataka zinatupwa katikati ya jiji...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom