Dar es Salaam - Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia

Segerea tumefanya uboya wa kitoto sana, mgombea wa chadema alikuwa kama yule mwanamke kahaba alielalia mtotoke na kuiba wa mwenzake, walipoenda kwa Mfalme Suleiman akataka apasuliwe kati kwa kati wagawane! Shame on her!
 
Sehemu wanazoongoza CUF tayari tofauti hipo inaonekana, serikali za mitaa ya CUF yote Dar hakuna kutoka pesa mwananchi kwa huduma yoyote, hata baruwa ni bure, nakuhakikishia sehemu wakishaichukuwa sahau kurudi ccm, hawa jamaa nawakubari kwa utendaji wa hizi local government.

Hata Zanzibar wapeni tu ushindi wao utakuja kukumbuka maneno yangu mambo yatakavyokuwa super Zanzibar.

Ni kweli mkuu Matola, Watanzania sijui nani katuloga! nashangaa Mtwara ccm kupata kura nyingi vile.
 
Last edited by a moderator:
mwaka 2010, nikiwa kimara mwisho nilimpigia MNYIKA akapita; Katikati hapo nikahamia Mbeya mjini kimaisha kwa muda, mwaka huu 2015 nimempigia SUGU nae kapita...haaa..yani raha tupu KURA yangu!!

SASA January narejea Dar, Ubungo yupo Kubenea....najisikiaje raha....narudi nikiwa na amani ya kutosha kwenda kuongozwa na halimashauri chini ya UKAWA, jamani Dar raha; laikini hata ningebaki Mbeya..bado raha sababu SUGU nae amekabidhiwa halimashauri ya jiji.....so maendeleo lazima!!! nashauri mwaka 2020 tujichange zaidi tuchukue halimashauri nyingi,,,ndio itakuwa mwanzo wa kuchukua nchi hapo mbeleni kidogo....iwapo mwaka huu CCM itapenya!!
 
Baadhi ya wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, wamevamia kituo cha kuhesabia kura za jimbo hilo kilichopo katika Shule ya Msingi Maji Matitu na kuchoma masanduku 10 ya kuhesabia kura.Tukio hilo lilitokea jana saa 11:00 jioni baada ya wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa Chama cha Wananchi (CUF) kutawanywa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakidaiwa kutaka kuingia ndani ya kituo hicho.Baada ya wafuasi hao kutawanywa na mabomu, inadaiwa kuwa baadhi yao walizunguka nyuma ya kituo hicho cha kuhesabia kura kilichopo ndani yashule hiyo na kuingia moja kwa moja ndani ya darasa linalotumika kuhifadhia kura kisha wakachoma masanduku yapatayo 10.Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa kilitokana na matokeo hayo kucheleweshwa kutangazwa kwa siku ya tatu sasa. source Times Fm
 
Timu Magufuli tupo hapa, tunawakilisha mwanzo mwisho.

Rais Magufuli hakika wewe ni chaguo la wengi.

Mwenyezi Mungu akubariki, Amin
 
Timu Magufuli tupo hapa, tunawakilisha mwanzo mwisho.

Rais Magufuli hakika wewe ni chaguo la wengi.

Mwenyezi Mungu akubariki, Amin


​Mungu. Yupi Mkuu? Mungu Anachangamana na Ulaghai? Labda Mungu Moto Ule Uliokuwa Kwenye Mabango Yake.
 
Mtwara si wanaishi mazombie then wanawake ndio kikwazo cha kutoitoa fisiem madarakani.


Mkuu si hivyo;

Mtwara kusema ukweli wanataka mabadiliko isipokuwa kilio tulichonacho majimbo mengine na katika katokeo ya urais ndivyo iivyo mikoa ya kusini.

Kule ni uchakachuaji. MSiwe na shaka tutakkutana mahakamani na vielelezo
 
...Hivi Chadema mwaka 2010 walikua na wabunge wangapi wa kuchaguliwa majimboni?
 
Timu Magufuli tupo hapa, tunawakilisha mwanzo mwisho.

Rais Magufuli hakika wewe ni chaguo la wengi.

Mwenyezi Mungu akubariki, Amin

Unatapika humu ukirudi Nyumbani Umeme hakuna....SUKARI ELF 2...MCHELE ELF 2,....SEMBE 1200 kwaakili kama hizi Sitashangaa CCM kuwekeza kwenye ujinga kwasababu inalipa sana
 
Mkuu si hivyo;

Mtwara kusema ukweli wanataka mabadiliko isipokuwa kilio tulichonacho majimbo mengine na katika katokeo ya urais ndivyo iivyo mikoa ya kusini.

Kule ni uchakachuaji. MSiwe na shaka tutakkutana mahakamani na vielelezo

Inaweza kuwa kweli lkn hilo lakwenda Mahakamani Fikitia vzr Sheria zetu Matokeo yakishatangazwa Basi hakuna pakwenda...Dawa kama ushahidi wakutosha upo Laigwanan akinukishe tuheshimiane kama KENYA
 
Back
Top Bottom