Dar es Salaam: Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka nane

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu, Stambuli Yusufu (35) kifungo cha maisha jela baada ya kumkuta na hatia ya kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike wa miaka nane.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo anayesoma darasa la nne kati ya mwaka 2017 na 2018.
Imeelezwa kuwa baada ya kitendo hicho alikuwa akimpatia Sh1,000 hadi 2,000, kumtaka asiseme kwa mtu yeyote.

Akisoma hukumu hiyo leo Jumanne Januari 28, 2020 hakimu mkazi, Jimson Mwankenja amesema kifungo cha maisha jela kitaanza kuhesabiwa baada ya mshtakiwa kumlipa Sh2 milioni mtoto huyo.

Amesema ikiwa atashindwa kulipa fidia hiyo, atachapwa viboko 12 na kuanza kutumikia kifungo hicho.

Hakimu Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya kuzingatia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka, utetezi wa mshtakiwa na uzito wa kosa hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Sheria nyingine bhana.

Ikiwa atashindwa kulipa milioni 2 basi atachapwa fimbo 12 na kuanza kutumikia kifungo.

Kwahiyo inaonekana hiyo milioni 2 haina ulazima wa kutoa, ilipaswa alipe kwa njia yoyote ile kabla hajaanza kutumikia hukumu.
 
daaah.! kumbe viboko 12 vina thamani ya 2m, bc ndo mana walimu walikuwa wanatuchapa hovyo kumbe wanalipwa huko majuu.
 
kwan ile kauli ya adhabu haipo inayosema
"Atafungwa kifungo cha maisha au atalipa pesa milioni kadhaa au atafanya vyote kwa pamoja" hio kaul hapo haitumik nn mana viboko dozen duu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom