Uchaguzi 2020 Dar es Salaam imepatwa na nini? Mbona mpo tuli?

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Kama mji mkuu Tanzania kwa hadhi na historia, jiji la Dar ndio lango la mambo yote, yawe mazuri au mabaya.

Ni kweli Dar ni bandari salama ila sio kwa kupoa huku kwenye vuguvugu hili la mabadiliko.

Sijaona zile vibe za 2010 kipindi cha Dr. Slaa Vs Kikwete. Sijaona vibe za 2015 kipindi cha Mh Edward Lowasa Vs Dr. JPM

Jiji na viunga vyake vyote ilikua mshikemshike nguo kukauka nikuvae, ila this time, watu wako busy na issue zao tu.

Sijui ni hasira zimewajaa mzee wa kaya alivyoziba mirija kwa miaka 5?

Please, tunapoelekea week 4 za mwisho, tunataka kuona mchango wa jiji kubwa katika harakati za kuwa na taifa lenye muelekeo wa kisera na kimifumo ya taasisi za kiutawala, na maendeleo.
 
Nataka mabadiliko wameshakula Sana hii nchi waache yu na wengine wale hata km tutapigwa Tena nafuu kuliwa kuliwa na wale wale wanapeana maisha wao kwa wao maarufu...pum.bav kbs CCM mmetuvunjia heshima vijana kwa kutunyima ajira na huku tumesoma kwa mamilioni ni heri tungefanya biashara mapema
 
Mkuu una hasira?
Vipi 5:0 Nini?
 
Tuko busy na mambo yetu, ni uboya kupoteza muda kumpa mtu ulaji, mwaka 2015 saa 12 niko kwenye foleni kumpa ulaji mbunge wangu, hajui na hatajua nilishinda juani kwa ajili yake,akawa anatupita barabarani hata salam hatoi, sitarudia tena kupoteza muda kufanywa ngazi ya mtu
 
Jiji na viunga vyake vyote ilikua mshikemshike nguo kukauka nikuvae, ila this time, watu wako busy na issue zao tu.
Kwani hukuona ilivyokuwa huko Kawe mshike mshike ulivyokuwa kati ya mmiliki mapepo na huyo bibi? Bibi alipigwa knock out. Huko kwenye majimbo mengine nako walipigwa knock out mapema na hivyo ligi ilishamalizika mapema.
 
Screenshot_20200929-204922.jpg
 
Back
Top Bottom