Iitwe MlonganzilaHabari wakuu. Hili jina ni la jiji kubwa kuliko yote nchini chakushangaza ni la kiarabu wakati nchi ni ya kiafrika tena wabantu.
Kwakweli ili kulinda utambulisho wetu napendekeza jina libadirishwe liwe la kibantu kama mikoa mingine tena la kizaramo kabisa.
Haiingiii akilini kuwa na jina la kiarabu kwa mji wetu huu wa kibiashara.
Unaonekana hata hujui kwanini umeanzishwa uzi.. Unataka ujue maana ya es badala ya el au unataka jina lote libadilishwe? Sema usikikeLabda utueleze why kuna es badala ya el?? Why tupate mikanganyiko isiyo ya lazma
Salisbury- HarareLingekua Washington usinge sema libadirishwe kinacho kusumbua hapo ni roho mbaya ya ugalatia unashindwa kuangalia nini maana ya jina la dar es laaam sema sasa na ikulu ivunjwe kwa sababu imejengwa na waarabu
Waambie hao hawajui kuwa hakuna lugha ilokamilika. Ndo maana lugha hukopa maneno toka lugha ntingine. Halafu kiswahili kwa asilimia kubwa ni kibantu kwa ushahidi wa kihistoria na kiisimu. Ova.Ni kweli ila kiswahili kimetohoa hayo maneno hivo hayapo kama yalivo kwa kiarabu yanatamkwa kibantu. Dar es Salaam imabaki kiarabu kabisa tofauti na maneno ya kiswahili yenye asili ya kiarabu.
Amesahau kama mikoa ya Mbeya na Rukwa ilikuwa ikiitwa Bismarck.Ndugu yangu sio vizuri kuingiza udini kwenye hii mada. By the way wakati wa utawala wa wajerumani baadhi ya mikoa ilikua ina majina ya kijerumani ila baadae ilikuja kubadirishwa
Itabidi ubadilishe maneno mengi ya kiswahili,hata hilo neno Swahili ni kiarabu,Tabora ni kiarabu,Ilala ni kiarabu,Tabata ni kiarabu.Naomba nieleweke nia ya mada hii ni kutambulisha utamaduni wetu na lugha yetu kwenye majina ya mikoa yetu ili iakisi asili yetu. Wala sisapoti hata kutumia majina ya kiingereza kwa miji yetu.
Pia kiswahili maneno mengi ni ya kibantu kwa asilimia kubwa. Maneno mengi ya kiswahili yanafanana na lugha zetu za asili kuliko kiarabu. Hivo ninavopinga jina la Dar sipingi dini ya mtu maana hakuna uhusiano huo.
Mimi nimependekeza tuanza na huu mji maana jina lake limekua tofauti kabisa na majina ya kibantu. Na uhakika hata maneno uliyotaja kwa kiarabu hayaandikwi hivo ila yametoholewa kuwa ya Kiswahili.Itabidi ubadilishe maneno mengi ya kiswahili,hata hilo neno Swahili ni kiarabu,Tabora ni kiarabu,Ilala ni kiarabu,Tabata ni kiarabu.
Kiswahili 26% ni maneno ya kiarabu.Namba 1 2 3 4 5 6 7 8 9 ni namba za kiarabu,kutumia mkono wa kulia ni kiarabu.Na pia Luna majengo yanayotuinyizia pesa katika utalii,yameachwa na waarabu,pia tubadilishe.Majina ya watu,Meiji,mitaa itabdi tubadilishe.
Hiyo pia ni kiarabu,tena hapo ndio kiarabu kinachoitwa classic Arabic.Uarabu huwezi kuuondoa dunia,mpaka maneno mengi ya kisayansi ni ya kiarabu.Mimi nimependekeza tuanza na huu mji maana jina lake limekua tofauti kabisa na majina ya kibantu. Na uhakika hata maneno uliyotaja kwa kiarabu hayaandikwi hivo ila yametoholewa kuwa ya Kiswahili.
Hata kule spain waarabu walitawala kusini pakiitwa Al Andalus ila leo pale panaitwa Andalusia kwa kispaniola baada ya Waarabu kuondolewa. Jina Al Andulus liliondoka na waarabu wake.