Dar es Salaam here I come naomba mnipokee waugwana!

Asalam alaikum wanajamvi, Namshukuru Mungu kwa kuiona siku mpya nikiwa na siha na afya njema. Baada ya kufika Tanga kuwaona jamaa na marafiki na sio kurenuu konsensa kama alivyosema "drphone" hatimae leo nipo njia moja narudi zangu Dar es Salaam.

Nimefungashiwa na wenyeji wangu pakacha la embe viringe, nazi, ndizi za bokoboko,halwa, vitoria,heltho ya lita 5 na vingine vingi. Japo kuwa waenyeji wangu wa jf huku Tanga hawakunipa ushirikiano na mapokezi ya kutosha zawadi iliyo moyoni mwangu narudi nayo Dar es Salaam, shukran za dhati kwa shosti, caramel na michelle kwa mlijitoa kimasomaso kwa karibu ya mdomo japo hamkujua umuhimu wa kampani yenu. Sina budi kuwashukuru kwani hilo si dogo pia.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru The Finest, Kiraka, Baba ubaya, babalao, Miss Judith, Mwenzetu, Babukkijana, MTM, Dreamliner, RayB, Chupaku, Mallaba, Moudymtoi, Miss Pirate, Mpevu, Son of Alaska, na bila kumsahau Shemu, pamoja na wote mliosoma ile post ya "Tanga Mpooooo??? Mmeifanya safari yangu imekuwa ya maana mnenipa kampani ya nguvu sana. Ahsanteni sana tupo pamoja. Walionipa salam zao nimezifikisha na wanasema wamefurahi sana ila watafurahi zaidi kama mtawatembelea siku moja.

Mkuu Ikimita, nimefika Chumbageni kama ulivyoniomba nimemtafuta Rehema nimempata nikampatia ujumbe wako amesema "kapata dereva ajuae gari yake yaenda mbio" sijafahamu ana amamanisha nini lakini sidhani kama atarudi tena kwako. Tanga Raha na ni raha kweli kweli, tanga hakuna foleni kama Dar narudi huku nikifikiria foleni zetu za luku, bank, barabarani na maofisini natamani Dar ingekuwa kama Tanga!

Namalizia kwa kusema naomba mapokezi wandugu ikiwezekana Invisble awe mkuu wa mapokezi na ikibidi kikundi cha matarumbeta kiwepo na si vibaya kama kutakuwa nakikundi cha ngoma za asili especial mdundiko maana huku nilipokelewa na mdumange na waenyeji wangu. Shukran sana na nategemea mapokezi yatafana.

UNAKUJA NYUMBANI AU UGENINI??

Karibu Basi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom