Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
Huwa nawashangaa vijana wa zamani utasikia siku hizi vijana hawana maadili, wanaongea hivi, wanaimba hivi, wanavaa sivyo etcEnzi Hairudi.
Nelson,Enzi Hairudi.
Umenikumbusha jambo kubwa sana mzee wangu. Hii Portelo ndio soda ya kwanza kutengenezwa hapa nchini na kiwanda cha Abdurasul and Sons LTD kilichokua pale opposite na jengo la telephone House nadhani ni mtaa qa Bridge uleWauza soda za Portelo kutoka kiwanda cha Abdulrasul wanazunguka uwanjani
Umenikumbusha jambo kubwa sana mzee wangu. Hii Portelo ndio soda ya kwanza kutengenezwa hapa nchini na kiwanda cha Abdurasul and Sons LTD kilichokua pale opposite na jengo la telephone House nadhani ni mtaa qa Bridge ule
Siku moja mwaka 1996 mmojawapo ya mtoto wa Abdurasul akiiitwa Turabal( amefariki miaka takriban kumi iliyopita naye akiwa mtu mzima sana) alikabiliwa na mwanaharakati za Uzawa zilizoasisiwa na Mchungaji Christopher Mtikila, jamaa wa Kingoni na akamwambia wewe Gabacholi(Muhindi) rudi kwenu India
Basi Mzee Turab kama tulivyokua tunamwita alianza kumueleza yule mwanaharakati wa sera za uzawa kua yeye Babu yake akiitwa Sachupira alikuja Tanganyika(Kilwa) mwaka 1841 kwa Jahazi akitokea Zanzibar akiwa ni survivor wa ajali ya baharini iliyouwa wazazi wake yeye akiwa mtoto wa kubebwa
Baadae walezi wake wakahamia Dar na ndipo alipokulia hadi akaoa na kumzaa Abdurasul ambae ni Baba yao kina MarehemuTurabali, Mustafa, Shuli na wengine nimewasahau
Mzee Turab akamwambia yule jamaa wa Kingoni kwamba kipindi hicho bado Wangoni hawajaja kabisa Tanganyika wapo hukoo South Afrika wakipewa msukosuko na Mfalme Shaka Zulu hadi kwenye miaka ya 1880s. Akamalizia kwa kumuuliza kati ya yeye(Turab Abdurasul) na hiyo Mngoni nani kati yao ni Mtanzania zaidi!?

Hahahaa pamoja sana mkuuhii nimeipenda bure Kabisa
Ni umri wa mtu huo kabisa mkuu1887-1840 miaka 47
Youtube haipoWengi wetu tumekulia Dar es Salaam na tumeuona unazi wa Simba na Yanga ulivyokuwa.
Nakumbuka siku kama ya leo ambayo sasa tunaita Dar es Salaam Derby ukipenda Kariakoo Derby ilivyokuwa.
Nakumbuka pale mnadani Mafia na Msimbazi vile vitezo vilivyokuwa vinamwaga moshi wa ubani toka asubuhi.
Wakati ule Yanga wako Sukuma na Sunderland yaani Simba wako Congo.
Vilabu viko jirani kwa mwendo na mbio zetu za kitoto dakika kumi zilitosha kufika Yanga kuangalia kuna nini na ukarejea Sunderland kutazama hali ya hewa. Uwanja ulikuwa Ilala Stadium.
Watangazaji wa TBC wana kijibanda kidogo juu tuu ya jukwaa la watazamaji.
Dar es Salaam ilikuwa ndogo sana.
Milango ya kuingia uwanjani midogo sana inaruhusu kuingia mtu mmoja mmoja na wachanaji tiketi unawaona hapo.
Wauza soda za Portelo kutoka kiwanda cha Abdulrasul wanazunguka uwanjani na Cocacola pia walikuwa wanashusha makreti kwa makreti ya mbao nyuma ya uwanja.
Kuna vijana wakiuza soda hizo kwa kamisheni. Nakumbuka gari la soda za Cocacola la Mzee Maukwe.
Navikumbuka vyumba vya wachezaji...vyumba vidogo sana.
Minazi mingi ilikuwa imezunguka uwanja na kuna waliopanda minazi hii kuangalia mpira.
Hali imebadilika sana.
Kuna maendeleo makubwa katika soka.
Unazi pia umechukua sura tofauti kabisa.
Leo sihitaji kupiga zile mbio kwenda club au kupita mnadani kupata, "mood," ya "game."
Simu yangu janja inanitosha kabisa kusikiliza na kuona watani wanavyotupiana makombora na kwa kweli inaongeza ladha ya mchezo.
Hakika tumetoka mbali toka enzi za akina Mnuwili, Ugundo (Dr. William), Ayub Kiguru, Bin Dossi, Jumanne Kisukari...Allah awarehemu...viongozi kama Shebe, Kitwana Ibrahim...muhimu sana TFA itengeneze Ukumbi wa Historia ya Mpira na historia ya Wanazi wa Simba na Yanga.
Hii ni historia ya pekee kabisa.
Leo tuko kwenye "electronic tickets," na mpira uko kwenye TV na hii imetuletea wapenzi wa soka wa kwenye makochi majumbani, Uingereza wanawaita, "arm chair supporters," na wanajaribu kuwatoa vitini kuwaleta uwanjani.
Club zinataka kuongeza ''gate collection.''
Vilabu hivi Simba na Yanga vina historia kubwa sawasawa na mji wake wa Dar es Salaam.
Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.
View attachment 1024269
Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.