Dar construction expo kuwakutanisha wadau wa ujenzi

Apr 9, 2022
66
32
Watanzania na Wadau mbalimbali wa Ujenzi watakiwa kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya DAR CONSTRUCTION EXPO, ili kujifunza, nakuona Teknolojia mpya itakayopatikana katika Sekta ya Ujenzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi ambaye ndio Muandaaji wa Maonyesho hayo Bw. Deogratius John Kilawe amesema kuwa maonyesho hayo yanalengo la kuwakutanisha kwa pamoja wadau wa Sekta ya Ujenzi.

IMG-20231010-WA0762.jpg

Pia Mkurugenzi amefafanua kuwa maonyesho hayo yataambatana na kujadili njia mbalimbali zitakazosaidia kuinua Sekta hiyo pamoja na kukuza Mahusiano na kujipatia Wateja wa Bidhaa zao.

Pia amesema Maonesho haya yanatarajiwa kuwa ni ya siku Tatu kuanzia Tarehe 11- 13 Oktoba 2023 na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam.

Aidha Bw. Kilawe amesema kuwa, huu ni msimu wa 7 wa Maonesho ya Dar Constuctions Expo na yanajumuisha zaidi ya Makampuni 120 kutoka nje na ndani ya Tanzania pia yanatarajiwa kuwa yenye kuleta Tija na Mapinduzi katika sekta ya ujenzi.
 
Back
Top Bottom