Dar: Bilionea Davis Mosha mikononi mwa Polisi kwa kuwashambulia Maofisa wa Uhamiaji; aachiwa kwa dhamana

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
221
431
Hapa maofisa walikwenda kwenye apartment zake baada ya kupata taarifa muhimu.

VIDEO:



-----Update-----

Pagan Amum anasema,
Baada ya video kutrend iliyoonyesha Mfanyabiashara Davis Mosha akiwapiga maafisa Uhamiaji mpaka muda huu naandika Davis Mosha yuko chini ya mikononi mwa polisi...

Hongera sana jeshi la polisi. Hawa wafanyabiashara wenye ela walizoea serikali zingine ila sio hii..

========

Msemaji wa idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda amesema Mosha amewashambulia askari hao na kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika katika jengo la Delina lililopo Sinza Mori, jijini hapa.

"Askari walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja walionyeshwa ofisi za meneja,” amesema Mtanda.

“Wakati wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na kuanza kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang'anya askari mmoja simu yake.”

Amesema alichofanya Mosha ni kinyume cha sheria ya uhamiaji namba 54 kifungu cha 45 kipengele 1 F, kinachozungumzia kumzuia ofisa wa uhamiaji kufanya kazi yake ya ukaguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema tayari wamepokea taarifa ya tukio hilo, wanafanya uchunguzi kwa hatua za kisheria.

"Tunachunguza ili kujua kilichotokea ni nini, baada ya hapo ndio hatua nyingine zitafuata,” amesema Murilo.

======

UPDATES:

Ameachiwa kwa dhamana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom