DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamemchagua Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Sillo kuwa Naibu Spika wa Bunge. Sillo amechaguliwa leo Novemba 13, 2025 kwa kupata kura zote za ndio (371) zilizopigwa na wabunge huku akiwa mgombea pekee aliyegombea nafasi hiyo. Tayari Sillo ameapishwa kushika wadhifa huo huku akiahidi ushirikiano kwa wabunge wote.
Kabla ya wadhifa huo, Sillo amewahi kushika nafasi mbalimbali kama Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti.
Kabla ya wadhifa huo, Sillo amewahi kushika nafasi mbalimbali kama Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti.