DANGOTE cement imekuwa adimu

ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
2,286
2,198
Tangu DANGOTE kasitisha uzalishaji wa cement Kuna uhaba mkubwa sana wa upatikani wa cement na kutatiza shughuli za maendeleo. Cement zingine zimepanda kwa Ghafla na kufikia 12000 kwa bei ya jana hapa lindi ya twiga cement. Na leo hii cement hakuna kabisa uko mjini, ujenzi umesimama. Tumesahau kununua cement elf 15 imeshuka mpaka elf 10, 11 msiturudishe uko.

Serikali kaeni chini na huyu tajiri mmalize tofauti zenu katoa ajira nyingi kwa watanzania na cement yake imekuwa tagemeo kubwa kwa nchi yetu. Kuna figisu figisu nyingi sana kwa hiki kiwanda Nchi hii sera ya viwanda, viwanda vilivyopo vinafungwa sijui tunatoka wapi tunaelekea wapi.

Mwenye kujuwa chazo cha mgogoro mtujuze. Au ndo Yale Yale makaa ya mawe ya mbeya hayana ubora serikali inalizimisha wayatumia tu.

Wa mikoa mingine upatikani wa cement ukoje na bei.
 
Kiwanda mpk leo hii hajawekewa umeme.....alikuwa anatumia generetor ....hii Ndy nchi ya viwandaaazzzz banaaa

OVA
 
jamaaa anatumia mafuta ya kuendesha mitambo na lengo lake lilikua ni kutumia gesi ambayo haikidhi kiwango sasa lazima azime plant manake mafuta yachangia gharama kuwa kubwa za uendeshaji wa kiwanda!
cha msingi kwanza wawekeze kwenye vyanzo vya nishati vya kueleweka,mfano makaa ya mawe,umeme wa upepo na wajua inawezekana.
 
huku kwetu hatuna madukani kwa hiyo hatah bei hatujui itakuwa kiasi gani pale itakapopaatikana
 
Inasemekana jamaa kamua kukifunga kiwanda chake kimya kimya baada ya kuingia kwenye mgogoro na sirikali baada ya kukatazwa ku-import makaa ya mawe ........
 
Ukigeugeu,ukurupukaji,misifa ya kijinga,chuki za kitoto,husda za kijinga jinga,ndo hulka yetu wabongo.
 
Sasa hivi naye ataambiwa ni mpiga dili, alizoea kukwepa kodi, Ana haribu mazingira nk..
Hii nchi ni ngumu jamani.

Kazi ya kuwekeza miundo mbinu ni ya serikali. Yeye kama mwekezaji ni kuzalisha,kuajiri raia wenu na kulipa kodi stahiki.Hizo tambo anazotambiwa kuwa ni mpiga dili,mkwepa kodi na mharibu mazingira ni laana zetu zinawazunguka.Dangote ni billionea anae mwacha Trump kwa umbali wa kurusha jiwe na sio mpiga madili mliyozoea nchi hii.Nilipomsikia waziri wa biashara akiwashauri wasafirishaji wapaki malori yao hadi bandari itakapopata tena mizigo nililia machozi hata kama similiki tairi ya baikeli.Dangote alishajuta sana kuhusu huu uwekezaji mkubwa hivyo nchi ya kisanii kama hii.Mitambo anaweza kuihamisha jee majengo na ardhi aliyonunua ndio kitendawili kwake ila hana hamu.
 
sad, nawafikiria maelfu ya vijana waliokuwa wamepata tumaini kwa kuwepo kiwanda hicho pale MTR, madreva, mama lishe etc
 
Back
Top Bottom