Dangote ajiandaa kuongea na Rais Magufuli

Dangote ajiandaa kuongea na Rais Magufuli

.....tena akija na wimbo ulio bora ambao mfalme anataka kusikia"kiwanda cha sukari"......yaani nawahakikishia atapewa gas in next 24 hours na lolote linguine atapewa tena kwa jazba kubwa...MWijage na Muhongo wajipange.............subirini tu aje....anakuja na tune ya sukari mmekwisha na makaa yenu ya mawe.............
Mkuu kama ni kweli baba rizmoko na embe wana hisa basi itakuwa washampiiiiiiiiika Dangote vya kutosha si wanamjua JP,M in and out akifika ataongea mambo mataaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam kwa JP,M na mwisho Mhong na Mwijg wataonekana watu wa hovyo kabisaaaa! na from there itakuwa issue ya Dangote inaanzia Ikulu then wengine wanaambiwa watekeleze! naona kwa mbaaali chenkapa alivyofura na atakavyofura baada ya J,PM kutoa maamuzi ya mwisho ndipo atakapojua hela haina uraic mstaaf na kama namuona vile baba riz anavyocheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeka!
Muhng na Mwjg wajiandae kisaiklojia kunywa matapishi yao na wala wasikasirike maana kazi walizikubali wenyewe!
 
Yule mama alikuwa anababaika kidogo nafikiri hajazoea kuongea na media.Kuna sehemu alisema Dangote anasafiri sana lakini kabla ya mwisho wa mwaka huu anaweza kuonana na Magufuli.
Unajua mama anaujua ukweli woooooooooooooote shida aliyokuwa anapata ni kwamba anataka kutumikia mabwana zaidi ya 1! anamsifia sana Dangote, anaisifia sana serikali! sasa hapo akawa anajaribu kuwa makini asiukosee upande wowote na hiyo ni poa maana mwisho wa siku anapata ugali wake hafanyi kazi bure pale! by the way yupo kazin ni kama akina Lizabon na wengine humu JFs
 
Bila shaka JK atakuwa kwenye icho kikao ili kuweka mambo sawa na kuondoa lugha gongana
 
Watanzania tusiwe wanasiasa katika kila ishu aitatufikisha popote pale sasa rais ndio fund mitambo wa kiwanda cha dangote
 
Mfanyabiashara maarufu wa Cement duniani Bilionea Aliko Dangote amepanga kuonana na Rais John Pombe Joseph Magufuli ili aweze kumweleza kuhusu utata unaotokea kwenye uzalishaji wa Cementi katika kiwanda chake kilichoko Mtwara.

Bilionea huyo ambaye alikuwa amepanga kufungua kiwanda cha sukari na kutengeneza bandari ndogo kuna mambo ambayo haridhishwi nayo yanayofanywa na wafanyabiashara pamoja na baadhi ya wanasiasa nchini kuhujumu jitihada zake za uzalishaji.

Mfanyabiashara huyu ambaye inasemekana hulala masaa matatu tu kwa siku huenda akakutana na Rais kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

MY TAKE.
Tunaomba busara itumike ili tajiri huyu aendelee kuwekeza nchini.

======

SAKATA la kusimama uzalishaji kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara limechukua sura mpya baada ya mmiliki wa kiwanda hicho, Alhaji Aliko Dangote kuamua kuja nchini ili kumuona Rais John Magufuli.
Taarifa ambazo Nipashe ilithibitishiwa na kiwanda cha Dangote jana, zilieleza kuwa Dangote anakuja nchini kwa nia ya kumuona Rais Magufuli ili ashitakie mambo kadhaa ikiwamo madai ya kuwapo kwa hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara.

Kiwanda cha Dangote ambacho ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa saruji, kilisitisha uzalishaji wiki mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Harpreet Duggal, kuwa ni kuelemewa na gharama kubwa za uendeshaji.

Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana jioni kuwa 'bosi' wake ameamua kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500.

"Kuna mambo mengi tuliyokubaliana na Serikali kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hatuna tatizo na serikali. Imetupa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi kuanzia ardhi, mafuta ya dizeli lita milioni tatu na mengine mengi," alisema Baruti.
Kama analala masaa 3 tu kwa siku basi afya yake c nzur. Joke kidogo
 
Ufisadi wa chadema utaigharimu nchi hii.


Wamebadili gia angani wanataka kumtumbua Dangote kama walivyomfanyia Lowasa na Nhc

utakuwa unakalia kigogo kwa nyuma.
 
Mwezi mzima Dangote Dangote mpaka tumechoka sasa.

Hii habari lazima ijadiliwe sana maana inahusu maisha ya watu.Kuna watu watapoteza ajira ambayo inawalinda wao na familia zao.Vilevile Cement inaweza kupanda bei lakini baya zaidi ni kuharibu taswira ya Tanzania kimataifa hasa kwenye kuvutia wawekezaji.
 
Kwa figisu Tanzania tuko vizuri, watu wanawaza maslahi yao tu kuanzia wanasiasa,wafanyabiashara, wafanyakazi hadi wananchi wa kawaida.!
Na hiyo ndio tabia yetu watanzania, unapomzungumzia mtanzania halisi basi ndo huyo uliyemuelezea hapo mkuu.
*Tanzania kilichobaki ni kujivunia
-lugha ya kiswahili
-mlima kilimanjaro
 
Hii habari lazima ijadiliwe sana maana inahusu maisha ya watu.Kuna watu watapoteza ajira ambayo inawalinda wao na familia zao.Vilevile Cement inaweza kupanda bei lakini baya zaidi ni kuharibu taswira ya Tanzania kimataifa hasa kwenye kuvutia wawekezaji.
Umefafanua vizuri kiongozi.
 
Ukweli huu hapa.. Mh. Rais wetu sikiliza hii sound clip..!!

Maoni yangu: Dangote apewe ruhusa ya kuagiza makaa ya mawe kokote anakotaka.. plse plsee makaa ya mawe yanayochimbwa kwa sasa hayatoshelezi kiwanda cha Dangote, tuache siasa

 

Attachments

Sababu ni msauzi hataki kusikia kitu cement ya dangote kwa sababu dangote alitaka kuuza mfuko 7000 ingesababisha makaburu kufunga viwanda vyao vya cement tz na EAC na SADC
 
Ufisadi wa chadema utaigharimu nchi hii.


Wamebadili gia angani wanataka kumtumbua Dangote kama walivyomfanyia Lowasa na Nhc
Naomba JF ikutangaze kuwa wewe ni mwehu bora wa mwaka 2016.
Mbona unachanganya mambo kiasi hiki? Au ni pombe unakunywa isiyopimwa?
Jamaa kapagawa kweli yaani hata haelewi nini tunajadili.Inawezekana kanyang'anywa Jimbo na CHADEMA sasa anaiota kila dakika.

Mnahangaika bure na hili dude linaloitwa "Lupyee"....

Siyo binadamu huyu.......
 
Back
Top Bottom