Dangote ajiandaa kuongea na Rais Magufuli

Dangote ajiandaa kuongea na Rais Magufuli

Kuna wary hii habari wanaiandika kwa malengo hasi , Kama vile serikali hii ya awamu ya tano kuna kosa wamefanya, badala ya kuelezea ukweli wa Suala la dangote tokea lilipotokea , lilipo na tunakoelekea na zaidi ya hapo hakuna anayejua akija anakuja kuongea nini ?? Changamoto, vikwazo au fursa nyingine za Biashara Kama Hilo la sukari
 
Wana jamvi

SAKATA la kusimama uzalishaji kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara limechukua sura mpya baada ya mmiliki wa kiwanda hicho, Alhaji Aliko Dangote kuamua kuja nchini ili kumuona Rais John Magufuli.

Taarifa ambazo Nipashe ilithibitishiwa na kiwanda cha Dangote jana, zilieleza kuwa Dangote anakuja nchini kwa nia ya kumuona Rais Magufuli ili ashitakie mambo kadhaa ikiwamo madai ya kuwapo kwa hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara.

Kiwanda cha Dangote ambacho ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa saruji, kilisitisha uzalishaji wiki mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Harpreet Duggal, kuwa ni kuelemewa na gharama kubwa za uendeshaji.

Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana jioni kuwa ‘bosi’ wake ameamua kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500.

“Kuna mambo mengi tuliyokubaliana na Serikali kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hatuna tatizo na serikali. Imetupa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi kuanzia ardhi, mafuta ya dizeli lita milioni tatu na mengine mengi,” alisema Baruti.


Chanzo: Nipashe
 
Ni vizuri kuwepo na muwafaka si hizi porojo za mitandaoni
 
Ufisadi wa chadema utaigharimu nchi hii.


Wamebadili gia angani wanataka kumtumbua Dangote kama walivyomfanyia Lowasa na Nhc
Wewe jamaa ni mjinga sana watu wanajadili mambo ya msingi wewe unaleta ma.ta.ko ya mamako hapa?
 
Hii nchi bana, sijui nani kailoga

Hii ni LAANA ya Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere(RIP) alipowaambia CCM kuwa wakianza dhambi ya UBAGUZI hakika itawatafuna! Tunaona jinsi Wabara na Wapemba wanavyobaguliwa kwa Itikadi za kisiasa! Kuna miiko ya Viongozi iliyokuwa ndani ya Azimio la Arusha CCM walilizika na wakaamua kuwa Wapiga dili! Lakini pia aliwahi kusema kuhusu Raslimali zetu kuhusu MADINI alipowaambia wayaache mpaka TZ itapokuwa na Wataalamu wake yenyewe ili wachimbe wenyewe na siyo Wawekezaji.Lakini Viongozi wa CCM yote wameyapuuza!!!!
 
Acha Bilionea Aliko Dangote aje mwenyewe ili mbichi na mbivu zijulikane!
Nchi hii bado ina ukiritimba wa kihuni. Mijitu mizima na akili zao inaingiza porojo na longolongo kwasababu tu walishapewa SHARES kwenye Viwanda vingine vya Saruji(Cement)!

Kama JPM anataka kujua ukweli huu aombe list ya Shareholders toka Twiga Cement,Tanga Cement,Mbeya Cement,Rhino Cement n.k kama hajakuta majina ya baadhi ya Mawaziri na Vigogo wengine wa CCM wana shares kwa maelfu walizopewa ili kuwalinda wenye Viwanda hivyo!

Nitamshangaa sana Magufuli kama bado hajui kuwa issue ya Dangote ni VITA ya kibiashara kati yake na wenye Viwanda vya Cement vilivyoko nchini! Dangote Cement alianza kuzalisha Cement kwa bei nafuu kabisa ya Tshs. 8,000/= kwa mfuko wa Kilo 50 lakini hawa wengine wamekutwa wakiuza Cementi kwa Tshs. 16,000/=~ 20,000/= hivo Cementi ya Dangote imevuruga hesabu zao na hawamtaki kabisa!
Juzi tu baada ya Taarifa kwenye media kuwa kiwanda cha Dangote kimefungwa bei ya Cement ikapanda ghafla toka 11,500/= mpaka Tshs. 14,000/= na very soon itafika 16,000/= + kama JPM atazubaa!!!
Hiyo ndiyo Bongo land ya Magufuli yenye Viwanda!!!
 
Hii taarifa inasikitisha sana Suala nyeti kama hili had Rais ana Dangote waongee wkt ni ishu ya wizara usika na Uongozi wa Dangote wamgeongea na kulimaza mda ss kila kitu Rais hii nchi inasikitisha sana kwakwel.
 
Waziri Muhongo tangu ahusike na sakata la Escrow na kugoma kujiuzulu mpaka Kikwete alipo lazimkika kutengua uwaziri wake nilijua ni mtu wa maslahi tu hana jema kwa nchi hii kabisa, ni mtu mjanja sana anefanya kazi kwa bidiii lakini anahakikisha anavuta za kwake bila kujali athari itakayojitokeza kwa maamuzi yake,., ni mtu wa rushwa ndio maana alimtolea nje zito kabwe na kumuita malfi wa rushwa pale kuna mahali walikula mpaka wakashikana mikono wale kwenye sinia.
 
Naamini from the discussion mambo yataenda tofauti. Self interest kwenye mambo makubwa ya nchi yanaumiza sana Africa....this is a lesson well learned
 
.....tena akija na wimbo ulio bora ambao mfalme anataka kusikia"kiwanda cha sukari"......yaani nawahakikishia atapewa gas in next 24 hours na lolote linguine atapewa tena kwa jazba kubwa...MWijage na Muhongo wajipange.............subirini tu aje....anakuja na tune ya sukari mmekwisha na makaa yenu ya mawe.............
Hahaha ! Sukari.
 
Mfanyabiashara maarufu wa Cement duniani Bilionea Aliko Dangote amepanga kuonana na Rais John Pombe Joseph Magufuli ili aweze kumweleza kuhusu utata unaotokea kwenye uzalishaji wa Cementi katika kiwanda chake kilichoko Mtwara.

Bilionea huyo ambaye alikuwa amepanga kufungua kiwanda cha sukari na kutengeneza bandari ndogo kuna mambo ambayo haridhishwi nayo yanayofanywa na wafanyabiashara pamoja na baadhi ya wanasiasa nchini kuhujumu jitihada zake za uzalishaji.

Mfanyabiashara huyu ambaye inasemekana hulala masaa matatu tu kwa siku huenda akakutana na Rais kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

MY TAKE.
Tunaomba busara itumike ili tajiri huyu aendelee kuwekeza nchini.

======

SAKATA la kusimama uzalishaji kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara limechukua sura mpya baada ya mmiliki wa kiwanda hicho, Alhaji Aliko Dangote kuamua kuja nchini ili kumuona Rais John Magufuli.
Taarifa ambazo Nipashe ilithibitishiwa na kiwanda cha Dangote jana, zilieleza kuwa Dangote anakuja nchini kwa nia ya kumuona Rais Magufuli ili ashitakie mambo kadhaa ikiwamo madai ya kuwapo kwa hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara.

Kiwanda cha Dangote ambacho ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa saruji, kilisitisha uzalishaji wiki mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Harpreet Duggal, kuwa ni kuelemewa na gharama kubwa za uendeshaji.

Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana jioni kuwa 'bosi' wake ameamua kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500.

"Kuna mambo mengi tuliyokubaliana na Serikali kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hatuna tatizo na serikali. Imetupa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi kuanzia ardhi, mafuta ya dizeli lita milioni tatu na mengine mengi," alisema Baruti.
Saaafi sana sana!
 
Katika mtu niliyemuona wa ovyo kabisa ni waziri wetu wa vuwanda loh sikujua kama yule jamaa ni bogas kihasi hicho,we swala la muhimu kama hili unatuletea porojo???the guy he is not serious aise dah
 
Na juu ya misamaha yote ya kodi aliyopata awamu iliopita eeeeeh, haya weeee ndoto na iwe naye
 
Back
Top Bottom