Dangote ajiandaa kuongea na Rais Magufuli

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,685
Mfanyabiashara maarufu wa Cement duniani Bilionea Aliko Dangote amepanga kuonana na Rais John Pombe Joseph Magufuli ili aweze kumweleza kuhusu utata unaotokea kwenye uzalishaji wa Cementi katika kiwanda chake kilichoko Mtwara.

Bilionea huyo ambaye alikuwa amepanga kufungua kiwanda cha sukari na kutengeneza bandari ndogo kuna mambo ambayo haridhishwi nayo yanayofanywa na wafanyabiashara pamoja na baadhi ya wanasiasa nchini kuhujumu jitihada zake za uzalishaji.

Mfanyabiashara huyu ambaye inasemekana hulala masaa matatu tu kwa siku huenda akakutana na Rais kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

MY TAKE.
Tunaomba busara itumike ili tajiri huyu aendelee kuwekeza nchini.

======

SAKATA la kusimama uzalishaji kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara limechukua sura mpya baada ya mmiliki wa kiwanda hicho, Alhaji Aliko Dangote kuamua kuja nchini ili kumuona Rais John Magufuli.
Taarifa ambazo Nipashe ilithibitishiwa na kiwanda cha Dangote jana, zilieleza kuwa Dangote anakuja nchini kwa nia ya kumuona Rais Magufuli ili ashitakie mambo kadhaa ikiwamo madai ya kuwapo kwa hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara.

Kiwanda cha Dangote ambacho ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa saruji, kilisitisha uzalishaji wiki mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Harpreet Duggal, kuwa ni kuelemewa na gharama kubwa za uendeshaji.

Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana jioni kuwa 'bosi' wake ameamua kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500.

"Kuna mambo mengi tuliyokubaliana na Serikali kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hatuna tatizo na serikali. Imetupa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi kuanzia ardhi, mafuta ya dizeli lita milioni tatu na mengine mengi," alisema Baruti.
 
Labda atamsikiliza sio hao akina mwijage ambao kila siku mtu anabadilisha kauli
 
yule mama aliyekuwa anahojiwa hajajibu swali lililoulizwa 'kama mnastock ya kutosha sasa ni kwanin cement inapanda bei?'
 
Mfanyabiashara maarufu wa Cement duniani Bilionea Aliko Dangote amepanga kuonana na Rais John Pombe Joseph Magufuli ili aweze kumweleza kuhusu utata unaotokea kwenye uzalishaji wa Cementi katika kiwanda chake kilichoko Mtwara.
Bilionea huyo ambaye alikuwa amepanga kufungua kiwanda cha sukari na kutengeneza bandari ndogo kuna mambo ambayo haridhishwi nayo yanayofanywa na wafanyabiashara pamoja na baadhi ya wanasiasa nchini kuhujumu jitihada zake za uzalishaji.
Mfanyabiashara huyu ambaye inasemekana hulala masaa matatu tu kwa siku huenda akakutana na Rais kabla ya mwisho wa mwaka huu.
SOURCE.NIPASHE/CLOUDS TV.

MY TAKE.Tunaomba busara itumike ili tajiri huyu aendelee kuwekeza nchini.

Unaikumbuka hii kauli "siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa! ndicho kinachotokea kuna watu wanabweeeeeeka sasa yeye anakuja kutalk na big boss ni hii yote ni sabab ana pesa. Pesa inaongea ndugu pesa inaweza fanya vitu vingi ambavyo inaonekana haviwezekani!
 
Ufisadi wa chadema utaigharimu nchi hii.

Wamebadili gia angani wanataka kumtumbua Dangote kama walivyomfanyia Lowasa na Nhc

Wakati watu wanaongea mambo ya maana bora ukae kimya.Ina maana CHADEMA wana nguvu kuliko Serikali?Acha kudhalilisha serikali.
 
Unaikumbuka hii kauli "siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa! ndicho kinachotokea kuna watu wanabweeeeeeka sasa yeye anakuja kutalk na big boss ni hii yote ni sabab ana pesa. Pesa inaongea ndugu pesa inaweza fanya vitu vingi ambavyo inaonekana haviwezekani!

Ni kweli kabisa.Afadhali wakutane wenye maamuzi ya mwisho maana hawa wengine hawaeleweki.
 
Naomba JF ikutangaze kuwa wewe ni mwehu bora wa mwaka 2016.
Mbona unachanganya mambo kiasi hiki? Au ni pombe unakunywa isiyopimwa?

Jamaa kapagawa kweli yaani hata haelewi nini tunajadili.Inawezekana kanyang'anywa Jimbo na CHADEMA sasa anaiota kila dakika.
 
  • "Mkuu wa kaya hajawahi kuwa seriuos kwenye mambo seriuos na amekuwa seriuos kwa mambo yasiyo serious"
 
Ila watanzania jamaniii....yaani jamaa ulivoandika Uzi wako utafikiri Dangote ndio kakwambia. Yule mama mwenyewe hana uhakika ni lini.

Yule mama alikuwa anababaika kidogo nafikiri hajazoea kuongea na media.Kuna sehemu alisema Dangote anasafiri sana lakini kabla ya mwisho wa mwaka huu anaweza kuonana na Magufuli.
 
.....tena akija na wimbo ulio bora ambao mfalme anataka kusikia"kiwanda cha sukari"......yaani nawahakikishia atapewa gas in next 24 hours na lolote linguine atapewa tena kwa jazba kubwa...MWijage na Muhongo wajipange.............subirini tu aje....anakuja na tune ya sukari mmekwisha na makaa yenu ya mawe.............
 
Back
Top Bottom