Dalili kuwa mtoto wako anatumika kingono

nkumbuka nikiwa kama 4-5 yrs hivi nilishaanza kulalana na binti mmoja hivi anaitwa mariam alikua chumba cha jirani,,tulikua tunavizia mama zetu wakitoka kwenda sokoni au clinic na mchezo ulikua mtamu hasa,,,,,baadae tulijahama na hatujaonana ten 27+ yrs now na hata simkumbuki sura tena ila alikua mtam sana
Wewe haukuwa unadhalilishwa kijinsia. Ulikuwa unafanya mchezo mbaya ambao adhabu yake ni kucharazwa ulie hadi sauti ikauke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pitia ujumbe huuu...hatari fire
Screenshot_20190318-043347.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni pigo linaloendelea kutafuna kizazi kinachochipukia sasa na madhara yake yatakua kilio kikubwa huko tuendako maana kwa sasa hili swala halijatazamwa kwa jicho la pili na kutafuta ufumbuzi wa mapema. Eee baba nusuru watoto wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1048145
WATOTO WANATUMIKA KINGONO!
Inaumiza lakini ndio uhalisia! sio kitu kinapendeza machoni wala akili lakini ndio ukweli!

Watoto wetu hawako salama!

Hawako salama sio kwa watu tunaoamini sio salama.

Watoto hawako salama kwa watu tunaoamini wako salama!



Kuna vitu tu lazima kama jamii tuambiane na tuinue sauti kuvizungumza!

Unyanyasaji kingono miongoni mwa watoto ni jambo ambalo lipo, linafanyika, linatendeka under our very noses!

Ni vile tu hatuamini na tunafikiri wapo salama! ni vile tu tunaamini sio kitu kinaweza kutokea kwa wanetu! ni vile tu tunaamini wapo watoto aina fulani wa kufanyiwa hayo!



Sio kweli!

Sio kweli!

Sio kweli!


Leo hebu tushirikishane dalili ambazo zinaweza kuwa taarifa kuwa mtoto anatumika kingono.



Unyanyasaji kingono umekuwa ni sehemu ya historia za maisha ya baadhi yetu.



Matukio yote unayokumbuka ulifanyiwa ukiwa mdogo ambayo leo ukiwa mtu mzima

unaweza kuyahusisha na matukio ya kingono na hukusema ndiyo hayo yanaweza kuwa yanamtokea mtoto sasa na hasemi.



nyingine ni

  1. Mtoto anapata shida kukaa au kutembea (2 - 10yrs)
  2. Anaogopa kupita kiasi baadhi ya watu, mahali au vitu (0-5yrs)
  3. Anapenda kujishika sehemu za siri kiasi cha kujisahau mpk kulala akiwa anajishika.
  4. Anakaa chooni muda mrefu au kuhitaji kujisaidia mara kwa mara.(0-5yrs)
  5. Anaweweseka usiku (0-5yrs)
  6. Anakataa/kusumbua kula au kutapika bila ugonjwa mahsusi. (0-5yrs)
  7. Analia sana (0-3yrs )
  8. Anaona aibu na kujitenga (umri wote)
  9. Anashindwa kuzuia haja kubwa (4-7yrs)
  10. Anakuwa mkimya isivyo kawaida (umri wa balehe)
  11. Anashuka kielimu (6-17)
  12. Anakuwa na kiburi, maamuzi ya kukinzana na maagizo( umri wa balehe)
  13. Mimba (11-17)
  14. Majaribio ya kujiua (8- 17)
  15. Anakimbia nyumbani mara kwa mara (8-17)
  16. Msongo wa mawazo (8-17)
  17. Anakataa kushiriki shughuli za nyumbani, za shule, za kiroho. (7-17)




Ongeza zingine na tushauriane cha kufanya!

Hali sio nzuri!

Sio nzuri kabisa!

cc sema tanzania
Asante kwa elimu hii muhimu kwa walezi - ^ CS
 
Back
Top Bottom