Dalili kuu za kufeli kwa Rais Magufuli

Wasalamu wana JF.

Kwanza kabisa nianze kwa kujifuta machozi na kuionea huruma nchi yangu ya Tanzania kwa kufika huku ilipofika kwa sababu ya ukosefu wa umakini katika chaguzi na teuzi za viongozi. Tumekuwa ni nchi yenye mfumo mbaya na wa kijinga wa uchaguzi wa viongozi na hata mfumo ya kiuteuzi umekuwa hivyo hivyo enzi na enzi sasa. Nchi yetu imejengwa katika misingi ya kinafiki na kujipendekeza ambayo imepelekea viongozi wengi kuwa watu wasiokuwa "REAL" katika mifumo yao ya kuongoza.

Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka wa kihistoria katika nchi yetu, ni mwaka amao tuliwashuhudia wavivu, wazembe na wanafiki wakiibuka kuyasaka madaraka kwa hila na mali. Ni mwaka ambao msululu wa wasaka tonge waijitokeza kuchukua fomu za kugombania nafasi kubwa ya Urais wa nchi yetu. Mathalani ndani ya chama tawala walijitokeza wagombea 42, lakini ukiwatazama hawa 42 wengi wao walikuwa hawajui kwa nini wamechukua fomu za kuomba kuiongoza nchi yetu. Wengi walijitokeza kwa kushitukiza, mashinikizo na hata kwa tamaa ya kutaka kukwea katika kiti kikubwa kuiko vyote ndani ya nchi na kiuongozi. Hawakuwa na nia wala malengo ya muda mrefu na nchi yetu. Kiufupi walijipeleka kwa mihemko.

Katika pilika pilika hizo chama cha Mapinduzi nach kiliingia kwenye mtego wao aidha kwa makusudi au kwa kujua na kufanikisha kuwachuja wagombea hadi watano na mwishowe watatu waliofanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kura. Ukiwatazama hawa wanafainali watatu hakuna hata mmoja aliyekuwa na ndoto ya Tanzania moyoni wala mawazoni mwake, walibeba fomu kwa mashinikizo ya wakubwa wao kipindi hicho.

KWA NINI UTAWALA WA MAGUFULI UTAFELI.

1. Kwa sababu alikuwa hajajiandaa kuwa Rais kisaikolojia au kimbinu. Magufuli hakujiandaa na wala hakuwahi kujua kama kuna siku anagekuja kubeba bendera ya kwanza ya nchi hii, hata uchukuaji wake wa fomu ya kugombea Urais unasemekana alishinikwa na Rais mmoja wa zamani. Kwamba chama kilimkosa mtu hivyo bwana mkubwa akalazimishwa abebe kijiti hiki. Kitaalamu ni kwmaba kama ulikuwa hujajiandaa kukifanya kitu na ukapewa dhamana ya kukifanya na kukisimamia kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa.

Dalii ni nyingi sana za Magufuli kushindwa na kuonyesha kwamba alikuwa hajajiandaa kuwa Rais, mfano nyingi ya teuzi zake zimekosa weledi na nyingi zimeonyesha mahaba , mfano alipoingia madarakani tu aiwateua DASs, DEDs, DCs, RASs, RCs na hata Mawaziri na Mananibu wao. Kwenye teuzi zilizopo chini ya TAMISEMI kwa maana ya DCS, DEDs, na DAS, mkuu huyu alionyesh kuchemka mapema sana mana majina ya wateuliwa ylikuwa yakijirudia mara kwa mara katika teuzi tofauti tofauti, hii inaashiria kuwa mkuu hakuwa makini katika uteuzi wake au alikuwa anafanya kazi mwenyewe bila ushauri wa vyombo husika na wasaidizi wake. Hii ni daili kuu ya kushindwa.

2. Dalili ya pili ya kushindwa kwa Magufuli ni kukosekana kwa uthabiti na ubunifu kwa utawala wake. Wengi wa watawala na wateuliwa wa Rais wamekuwa siyo wabunifu, wamekuwa ni watu wa kusikiliza maagizo na kuendeshwa kwa mihemko. Mfano kitu kikiibuka Dar kesho yake utasikia kimegeuka na kuwa kampeni kwa viongozi wote nchini, kana kwamba think tank ya nchi hii iko kichwani mwa mtu mmoja Dar es salaam. Leo akiibuka mtu Dar na kusema naanza zoezi la kuzibua mitaro ,basi kila kiongozi mikoani ataifanya hiyo ni ajenda na kampeni ya nchi nzima. Hizi ni dalili za kushindwa na kukkosa umakini na ubunifu kwa viongozi.

3. Sera ya Viwanda .

Watanzania wengi haswa wa kipato cha chini walimpa kura Magufuli kwa kuwa alijinadi kuwa Tanzania aliyotaka kuiongoza ilikuwa Tanzania ya viwanda na kwamba angehakikisha katika utawala wake viwanda vingi vinpatikan kadri iwezekanavyo lakini ni miaka miili sasa nchi na wananchi wake hawajaona sera, wala dira wala mpango wowote ukianzishwa na serikali ili kuwezesha kupatika kwa nchi ya viwanda. Serikali imekuwa ni wapiga domo na nadiriki kusema kuwa Magufuli na wenzake wanatupigia domo katika ishu hii ya viwanda, hakuna uhalisia wowote. Wangekuwa ni watu makini, wenye nia ya dhati ya viwanda basi wangekuwa wameishafikisha mpango mkakati bungeni ili ujadiiwe na kupelekea kufanikisha nchi njema ya viwanda. Huwezi kusema utavipata viwanda kutoka mawinguni bila ya kuwa na mpango mkakati wa kuviwezesha kupatikana.

4. Uongozi wa visasi na chuki.

Uongozi wa Magufuli umetawaliwa na visasi na chuki kwa baadhi ya watu katika nchi hii, kwa sasa ukiwa mpinzani wa kiitikadi na watawala unakuwa umegeuka kuwa adui wao moja kwa moja. Hii siyo dalili njema hata kidogo kwa mstakabali wa taifa, leo mawazo mazuri ya kujenga kutoka kwa wapinzani wa kiitikadi hayapokelewi, wapinzani wamegeuzwa punching boxes za vyombo vya dola na usalama, hawana amani, hawako huru. Linatengenezwa bomu litakalokuja kulipuka na kuilipua Tanzania vipande vipande... oooh god forbid maana hata Rwanda ilianza hvi hivi.

5. Usalama hafiifu wa raia.

Nchi kwa sasa inalalama, wananchi hawana usalama wa maisha yao, mauwaji yasiyojulikana kila kuchapo, watu kupotea bila kuonekana na kujulikana walipo. Vyombo vya dola havina majibu ya kuridhisha juu ya matukio haya, haya yanaongeza chuki na kupunguza imani na ushirikiano wa raia kwa serikali yao. Kwa sasa ukanda wa Pwani ni ukanda hatari sana wa kuishi kwa Mtanzania yeyote mwenye hofu na maisha yake, vyombo vya usalama vikiongozwa na Polisi, TISS na wengine hawana majibu ya kutia moyo juu ya haya. Unategemea wananchi wa ukanda huo waamke wakazalishe huku hawajui kama watafika kesho? No, they can't,matokeo yake ni kuwa na wananchi wasioweza kuzalisha na kubakia kutegemea serikali yao hafifu isiyoweza kuwalinda iwape chakula na mambo mengine ya muhimu kwao.

Ninayo mengi ya kusema juu ya utawala huu wa Magufuli kwa leo hayo yanatosha, ila naomba itoshe tu kusema sioni PROGRESS yoyote tutakayopata kama nchi kutoka kwa utawala huu wa awamu ya tano.

wewe ni mmoja wa ma Great Thinkers , umesema bila upendeleo hakika asiyeona kuwa haya unayosema ni kweli na sahihi ajipime akili labda sio mzima ki fikra, Asanste kwa kutumia ubongo wako kufikiri vitu sahihi
 
Wasalamu wana JF.

3. Sera ya Viwanda .

Watanzania wengi haswa wa kipato cha chini walimpa kura Magufuli kwa kuwa alijinadi kuwa Tanzania aliyotaka kuiongoza ilikuwa Tanzania ya viwanda na kwamba angehakikisha katika utawala wake viwanda vingi vinpatikan kadri iwezekanavyo lakini ni miaka miili sasa nchi na wananchi wake hawajaona sera, wala dira wala mpango wowote ukianzishwa na serikali ili kuwezesha kupatika kwa nchi ya viwanda. Serikali imekuwa ni wapiga domo na nadiriki kusema kuwa Magufuli na wenzake wanatupigia domo katika ishu hii ya viwanda, hakuna uhalisia wowote. Wangekuwa ni watu makini, wenye nia ya dhati ya viwanda basi wangekuwa wameishafikisha mpango mkakati bungeni ili ujadiiwe na kupelekea kufanikisha nchi njema ya viwanda. Huwezi kusema utavipata viwanda kutoka mawinguni bila ya kuwa na mpango mkakati wa kuviwezesha kupatikana.

Kwenye hili la viwanda, nakubaliana na wewe, na mimi pia nimelizungumza hapa
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na mission wala vision ya ni nini vipaumbele vyetu, Tanzania ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndiPo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio. Nchi inakabiliwa na sitofahamu nyingi, kuna kiongozi amefoji vyeti, kuna kiongozi amefanya tukio la uvamizi wa media, kuna waziri anatimiza wajibu wake kwa waledi, anatumbuliwa, na kutishiwa bastola, halafu mkuu wetu wa nchi anakwenda kufanya igizo ziara ya kushtukiza bandarini! .

Ushauri on What to Do. A Way Forward
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na wakala, lazima ziwe na mission na vision statement, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas maonesho na kuita media kusema tutafanya hiki au kile!.

Mfano tunapo hubiri kuhusu Tanzania ya viwanda, where is the blue print ya Tanzania ya viwanda?, zenye smart objectives zenye malengo ya short term, medium term na long term strategies?. Ili tuwe na Tanzania ya viwanda tunahitaji land, where is the land set out kwa Tanzania ya Viwanda?. Tunahitaji labor, jee tumeishajua tutajenga viwanda gani ili hiyo mainpower na labor force kuvihudumia hivyo viwanda itayarishwe?. Tunahitaji capital ya kuanzisha hivyo viwanda, kuna strategies gani kuwawezesha Watanzania kuimiliki Tanzania ya Wiwanda, au tunataka kujenga Tanzania ya viwanda lakini viwanda ni vya wageni, vya Mchina, Mhindi na Mzungu?, na Mtanzania kuja kuwa ni kibarua tuu kwenye hiyo,Tanzania ya Viwanda kama ilivyo kwenye Uchumi wa Gesi?. Tanzania ya viwanda itahitaji malighafi ya viwanda, uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo the biggest industries za Tanzania ya Viwanda zinapaswa kuwa ni agro processing industries, jee tuna mikakati gani ya kuinua sekta ya kilimo, kutoa malighafi ya viwanda?, au tunajenga Tanzania ya viwanda kama viwanda vya Bhakressa, vinatengeneza jiuces na unga wa ngano, lakini malighafi zote zinatoka nje!, hadi pulp ya mango juice tuna import, huku maembe ya Lushoto yakiozea mitini!. Tangu tumeanza kuhubiri wimbo wa Tanzania ya Viwanda, tuko wapi, tumefanikisha nini? , tumekwama wapi and what is a way forward? .

Badala ya kuwahimiza ma bullies,impersonators na forgerists kuchapa kazi, tupewe matokeo ya hizo kazi zinazochwapwa, watu wanataka matokeo, na sio tuu kupokea maagizo na vitendo vya kuona sifa kutokelezea tuu kwenye TV, na kuandikwa magazetini, tujikite kwenye utendaji unaozingatia matokeo, na sifa zisiwe katika kutoa maagizo, bali katika matokeo ya utekelezaji.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Paskali
 
Kwenye kampeni alisema atafuta makodi kodi mengi mengi yanayomnyonya mtanzania
Lakin kodi ndio zimekuwa nyingi kama utitiri
 
Huna uwezo wa kufanya analysis na kujenga hoja zenye mantiki!. Nakushauri kajisaidie haja kubwa na ndogo kisha ukalale usije jisaidia haja hizo kitandani
 
Hawa baraza la vichaa hawaishiwi vituko kila siku ni kumtabilia kushindwa rais na siku zinakwenda tu
 
Tanzania iko pale pale wanainchi wako imara na wanaipenda nchi yao.Wafanyakazi wanafanya kazi usiku na mchana kuijenga Tanzania.

Majeshi ya ulinzi na usalama yanailinda nchi yao ya Tanzania,watanzania wenyewe wake kwa waume na Mali zao usiku na mchana.

Na kwa hali hiyo Rais Magufuli anakazi nyepesi mno ya kufanya ktk kazi yake ya uraisi.
 
UTAMWONGEZEA MUDA BASHA WAKO AKULE MSAMBWANDA BAADA YA MIAKA 10 HUNA ADABU, pia mti kupigwa mawe sio lazima uwe na matunda unaweza kuwa na BUNDI hivyo usikariri
 
Mkuu viwanda havijengwi kwa kukejeli raisi,wala si kazi ya serikali kujenga viwanda.
Ni wajibu wa mimi nawewe kujenga viwanda.
Hivi Cocacola au Big G,Au Boeing,au Vics dawa ya mafua ilijengwa na serikali za nchi husika?
Mkuu usipoteze nguvu zako kuisemea serikali bali wewe utaifanyia nchi yako nini? Anzia hapo na ujipime mchango wako kitaifa hata kifamilia.
Haya mambo ya kulelewa kama mayai ni shida hadi kwenye fikra zetu.
Hivi wewe unataka kula bila kunawa hadi lini.
Hacha kukejeli watu bila kuweka nguvu stahili.
 
Wasalamu wana JF.

Kwanza kabisa nianze kwa kujifuta machozi na kuionea huruma nchi yangu ya Tanzania kwa kufika huku ilipofika kwa sababu ya ukosefu wa umakini katika chaguzi na teuzi za viongozi. Tumekuwa ni nchi yenye mfumo mbaya na wa kijinga wa uchaguzi wa viongozi na hata mfumo ya kiuteuzi umekuwa hivyo hivyo enzi na enzi sasa. Nchi yetu imejengwa katika misingi ya kinafiki na kujipendekeza ambayo imepelekea viongozi wengi kuwa watu wasiokuwa "REAL" katika mifumo yao ya kuongoza.

Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka wa kihistoria katika nchi yetu, ni mwaka amao tuliwashuhudia wavivu, wazembe na wanafiki wakiibuka kuyasaka madaraka kwa hila na mali. Ni mwaka ambao msululu wa wasaka tonge waijitokeza kuchukua fomu za kugombania nafasi kubwa ya Urais wa nchi yetu. Mathalani ndani ya chama tawala walijitokeza wagombea 42, lakini ukiwatazama hawa 42 wengi wao walikuwa hawajui kwa nini wamechukua fomu za kuomba kuiongoza nchi yetu. Wengi walijitokeza kwa kushitukiza, mashinikizo na hata kwa tamaa ya kutaka kukwea katika kiti kikubwa kuiko vyote ndani ya nchi na kiuongozi. Hawakuwa na nia wala malengo ya muda mrefu na nchi yetu. Kiufupi walijipeleka kwa mihemko.

Katika pilika pilika hizo chama cha Mapinduzi nach kiliingia kwenye mtego wao aidha kwa makusudi au kwa kujua na kufanikisha kuwachuja wagombea hadi watano na mwishowe watatu waliofanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kura. Ukiwatazama hawa wanafainali watatu hakuna hata mmoja aliyekuwa na ndoto ya Tanzania moyoni wala mawazoni mwake, walibeba fomu kwa mashinikizo ya wakubwa wao kipindi hicho.

KWA NINI UTAWALA WA MAGUFULI UTAFELI.

1. Kwa sababu alikuwa hajajiandaa kuwa Rais kisaikolojia au kimbinu. Magufuli hakujiandaa na wala hakuwahi kujua kama kuna siku anagekuja kubeba bendera ya kwanza ya nchi hii, hata uchukuaji wake wa fomu ya kugombea Urais unasemekana alishinikwa na Rais mmoja wa zamani. Kwamba chama kilimkosa mtu hivyo bwana mkubwa akalazimishwa abebe kijiti hiki. Kitaalamu ni kwmaba kama ulikuwa hujajiandaa kukifanya kitu na ukapewa dhamana ya kukifanya na kukisimamia kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa.

Dalii ni nyingi sana za Magufuli kushindwa na kuonyesha kwamba alikuwa hajajiandaa kuwa Rais, mfano nyingi ya teuzi zake zimekosa weledi na nyingi zimeonyesha mahaba , mfano alipoingia madarakani tu aiwateua DASs, DEDs, DCs, RASs, RCs na hata Mawaziri na Mananibu wao. Kwenye teuzi zilizopo chini ya TAMISEMI kwa maana ya DCS, DEDs, na DAS, mkuu huyu alionyesh kuchemka mapema sana mana majina ya wateuliwa ylikuwa yakijirudia mara kwa mara katika teuzi tofauti tofauti, hii inaashiria kuwa mkuu hakuwa makini katika uteuzi wake au alikuwa anafanya kazi mwenyewe bila ushauri wa vyombo husika na wasaidizi wake. Hii ni daili kuu ya kushindwa.

2. Dalili ya pili ya kushindwa kwa Magufuli ni kukosekana kwa uthabiti na ubunifu kwa utawala wake. Wengi wa watawala na wateuliwa wa Rais wamekuwa siyo wabunifu, wamekuwa ni watu wa kusikiliza maagizo na kuendeshwa kwa mihemko. Mfano kitu kikiibuka Dar kesho yake utasikia kimegeuka na kuwa kampeni kwa viongozi wote nchini, kana kwamba think tank ya nchi hii iko kichwani mwa mtu mmoja Dar es salaam. Leo akiibuka mtu Dar na kusema naanza zoezi la kuzibua mitaro ,basi kila kiongozi mikoani ataifanya hiyo ni ajenda na kampeni ya nchi nzima. Hizi ni dalili za kushindwa na kukkosa umakini na ubunifu kwa viongozi.

3. Sera ya Viwanda .

Watanzania wengi haswa wa kipato cha chini walimpa kura Magufuli kwa kuwa alijinadi kuwa Tanzania aliyotaka kuiongoza ilikuwa Tanzania ya viwanda na kwamba angehakikisha katika utawala wake viwanda vingi vinpatikan kadri iwezekanavyo lakini ni miaka miili sasa nchi na wananchi wake hawajaona sera, wala dira wala mpango wowote ukianzishwa na serikali ili kuwezesha kupatika kwa nchi ya viwanda. Serikali imekuwa ni wapiga domo na nadiriki kusema kuwa Magufuli na wenzake wanatupigia domo katika ishu hii ya viwanda, hakuna uhalisia wowote. Wangekuwa ni watu makini, wenye nia ya dhati ya viwanda basi wangekuwa wameishafikisha mpango mkakati bungeni ili ujadiiwe na kupelekea kufanikisha nchi njema ya viwanda. Huwezi kusema utavipata viwanda kutoka mawinguni bila ya kuwa na mpango mkakati wa kuviwezesha kupatikana.

4. Uongozi wa visasi na chuki.

Uongozi wa Magufuli umetawaliwa na visasi na chuki kwa baadhi ya watu katika nchi hii, kwa sasa ukiwa mpinzani wa kiitikadi na watawala unakuwa umegeuka kuwa adui wao moja kwa moja. Hii siyo dalili njema hata kidogo kwa mstakabali wa taifa, leo mawazo mazuri ya kujenga kutoka kwa wapinzani wa kiitikadi hayapokelewi, wapinzani wamegeuzwa punching boxes za vyombo vya dola na usalama, hawana amani, hawako huru. Linatengenezwa bomu litakalokuja kulipuka na kuilipua Tanzania vipande vipande... oooh god forbid maana hata Rwanda ilianza hvi hivi.

5. Usalama hafiifu wa raia.

Nchi kwa sasa inalalama, wananchi hawana usalama wa maisha yao, mauwaji yasiyojulikana kila kuchapo, watu kupotea bila kuonekana na kujulikana walipo. Vyombo vya dola havina majibu ya kuridhisha juu ya matukio haya, haya yanaongeza chuki na kupunguza imani na ushirikiano wa raia kwa serikali yao. Kwa sasa ukanda wa Pwani ni ukanda hatari sana wa kuishi kwa Mtanzania yeyote mwenye hofu na maisha yake, vyombo vya usalama vikiongozwa na Polisi, TISS na wengine hawana majibu ya kutia moyo juu ya haya. Unategemea wananchi wa ukanda huo waamke wakazalishe huku hawajui kama watafika kesho? No, they can't,matokeo yake ni kuwa na wananchi wasioweza kuzalisha na kubakia kutegemea serikali yao hafifu isiyoweza kuwalinda iwape chakula na mambo mengine ya muhimu kwao.

Ninayo mengi ya kusema juu ya utawala huu wa Magufuli kwa leo hayo yanatosha, ila naomba itoshe tu kusema sioni PROGRESS yoyote tutakayopata kama nchi kutoka kwa utawala huu wa awamu ya tano.
sorry..we mchaga?
 
Sio kosa la muanzisha uzi kwani ni maoni na mawazo yake kwa namna anavyojaribu kuyawasilisha.
 
Wasalamu wana JF.
...
kana kwamba think tank ya nchi hii iko kichwani mwa mtu mmoja Dar es salaam.
...

Dalili zinaonyesha kuwa hali ni hiyo. Na kama kuna Think Tank tofauti na hiyo basi iko dhaifu sana (ya mfano wa ile inayotumika kutengeneza sera za chama tawala) NA/AU wahusika wanaipuuza.
 
Kwenye hili la viwanda, nakubaliana na wewe, na mimi pia nimelizungumza hapa
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...

Paskali

Naamini ili Systems(Mifumo) mizuri ipate kuwepo na kutumika, inabidi Viongozi wakuu wa nchi, hasa Raisi;

1. Waelewe maana na faida ya kuwepo kwa mifumo hiyo, na wawe na nia ya dhati yakufanya iwepo na kusimamia utekelezaji wake.
2. Watambue kuwa wanahijati (nchi inahitaji) kuwa na Think Tank ya kitaifa imara na endelevu.
N.K.

Mifumo hiyo ni muhimu ikawa (pamoja na vitu vingine) na UWAZI (transparency), UWAJIBIKAJI(accountability) na ijengwe katika dhana ya "Amini lakini Thibitisha" (trust but verify).

Kwa bahati mbaya (kwa maoni yangu), dalili zinaonyesha kuwa uongozi wa nchi uliopo madarakani unaamini kuwa mifumo/mfumo iliyopo inafaa kutumika kutuletea "maendeleo ya kweli", lakini tatizo lipo katika utekelezaji/usimamizi, na hivyo wamejikita katika kurekebisha utekelezaji/usimamizi.
 
Back
Top Bottom