Dalili kuu za kufeli kwa Rais Magufuli

Dalili kuu za kufeli kwa Rais Magufuli

Wasalamu wana JF.

Kwanza kabisa nianze kwa kujifuta machozi na kuionea huruma nchi yangu ya Tanzania kwa kufika huku ilipofika kwa sababu ya ukosefu wa umakini katika chaguzi na teuzi za viongozi. Tumekuwa ni nchi yenye mfumo mbaya na wa kijinga wa uchaguzi wa viongozi na hata mfumo ya kiuteuzi umekuwa hivyo hivyo enzi na enzi sasa. Nchi yetu imejengwa katika misingi ya kinafiki na kujipendekeza ambayo imepelekea viongozi wengi kuwa watu wasiokuwa "REAL" katika mifumo yao ya kuongoza.

Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka wa kihistoria katika nchi yetu, ni mwaka amao tuliwashuhudia wavivu, wazembe na wanafiki wakiibuka kuyasaka madaraka kwa hila na mali. Ni mwaka ambao msululu wa wasaka tonge waijitokeza kuchukua fomu za kugombania nafasi kubwa ya Urais wa nchi yetu. Mathalani ndani ya chama tawala walijitokeza wagombea 42, lakini ukiwatazama hawa 42 wengi wao walikuwa hawajui kwa nini wamechukua fomu za kuomba kuiongoza nchi yetu. Wengi walijitokeza kwa kushitukiza, mashinikizo na hata kwa tamaa ya kutaka kukwea katika kiti kikubwa kuiko vyote ndani ya nchi na kiuongozi. Hawakuwa na nia wala malengo ya muda mrefu na nchi yetu. Kiufupi walijipeleka kwa mihemko.

Katika pilika pilika hizo chama cha Mapinduzi nach kiliingia kwenye mtego wao aidha kwa makusudi au kwa kujua na kufanikisha kuwachuja wagombea hadi watano na mwishowe watatu waliofanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kura. Ukiwatazama hawa wanafainali watatu hakuna hata mmoja aliyekuwa na ndoto ya Tanzania moyoni wala mawazoni mwake, walibeba fomu kwa mashinikizo ya wakubwa wao kipindi hicho.

KWA NINI UTAWALA WA MAGUFULI UTAFELI.

1. Kwa sababu alikuwa hajajiandaa kuwa Rais kisaikolojia au kimbinu. Magufuli hakujiandaa na wala hakuwahi kujua kama kuna siku anagekuja kubeba bendera ya kwanza ya nchi hii, hata uchukuaji wake wa fomu ya kugombea Urais unasemekana alishinikwa na Rais mmoja wa zamani. Kwamba chama kilimkosa mtu hivyo bwana mkubwa akalazimishwa abebe kijiti hiki. Kitaalamu ni kwmaba kama ulikuwa hujajiandaa kukifanya kitu na ukapewa dhamana ya kukifanya na kukisimamia kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa.

Dalii ni nyingi sana za Magufuli kushindwa na kuonyesha kwamba alikuwa hajajiandaa kuwa Rais, mfano nyingi ya teuzi zake zimekosa weledi na nyingi zimeonyesha mahaba , mfano alipoingia madarakani tu aiwateua DASs, DEDs, DCs, RASs, RCs na hata Mawaziri na Mananibu wao. Kwenye teuzi zilizopo chini ya TAMISEMI kwa maana ya DCS, DEDs, na DAS, mkuu huyu alionyesh kuchemka mapema sana mana majina ya wateuliwa ylikuwa yakijirudia mara kwa mara katika teuzi tofauti tofauti, hii inaashiria kuwa mkuu hakuwa makini katika uteuzi wake au alikuwa anafanya kazi mwenyewe bila ushauri wa vyombo husika na wasaidizi wake. Hii ni daili kuu ya kushindwa.

2. Dalili ya pili ya kushindwa kwa Magufuli ni kukosekana kwa uthabiti na ubunifu kwa utawala wake. Wengi wa watawala na wateuliwa wa Rais wamekuwa siyo wabunifu, wamekuwa ni watu wa kusikiliza maagizo na kuendeshwa kwa mihemko. Mfano kitu kikiibuka Dar kesho yake utasikia kimegeuka na kuwa kampeni kwa viongozi wote nchini, kana kwamba think tank ya nchi hii iko kichwani mwa mtu mmoja Dar es salaam. Leo akiibuka mtu Dar na kusema naanza zoezi la kuzibua mitaro ,basi kila kiongozi mikoani ataifanya hiyo ni ajenda na kampeni ya nchi nzima. Hizi ni dalili za kushindwa na kukkosa umakini na ubunifu kwa viongozi.

3. Sera ya Viwanda .

Watanzania wengi haswa wa kipato cha chini walimpa kura Magufuli kwa kuwa alijinadi kuwa Tanzania aliyotaka kuiongoza ilikuwa Tanzania ya viwanda na kwamba angehakikisha katika utawala wake viwanda vingi vinpatikan kadri iwezekanavyo lakini ni miaka miili sasa nchi na wananchi wake hawajaona sera, wala dira wala mpango wowote ukianzishwa na serikali ili kuwezesha kupatika kwa nchi ya viwanda. Serikali imekuwa ni wapiga domo na nadiriki kusema kuwa Magufuli na wenzake wanatupigia domo katika ishu hii ya viwanda, hakuna uhalisia wowote. Wangekuwa ni watu makini, wenye nia ya dhati ya viwanda basi wangekuwa wameishafikisha mpango mkakati bungeni ili ujadiiwe na kupelekea kufanikisha nchi njema ya viwanda. Huwezi kusema utavipata viwanda kutoka mawinguni bila ya kuwa na mpango mkakati wa kuviwezesha kupatikana.

4. Uongozi wa visasi na chuki.

Uongozi wa Magufuli umetawaliwa na visasi na chuki kwa baadhi ya watu katika nchi hii, kwa sasa ukiwa mpinzani wa kiitikadi na watawala unakuwa umegeuka kuwa adui wao moja kwa moja. Hii siyo dalili njema hata kidogo kwa mstakabali wa taifa, leo mawazo mazuri ya kujenga kutoka kwa wapinzani wa kiitikadi hayapokelewi, wapinzani wamegeuzwa punching boxes za vyombo vya dola na usalama, hawana amani, hawako huru. Linatengenezwa bomu litakalokuja kulipuka na kuilipua Tanzania vipande vipande... oooh god forbid maana hata Rwanda ilianza hvi hivi.

5. Usalama hafiifu wa raia.

Nchi kwa sasa inalalama, wananchi hawana usalama wa maisha yao, mauwaji yasiyojulikana kila kuchapo, watu kupotea bila kuonekana na kujulikana walipo. Vyombo vya dola havina majibu ya kuridhisha juu ya matukio haya, haya yanaongeza chuki na kupunguza imani na ushirikiano wa raia kwa serikali yao. Kwa sasa ukanda wa Pwani ni ukanda hatari sana wa kuishi kwa Mtanzania yeyote mwenye hofu na maisha yake, vyombo vya usalama vikiongozwa na Polisi, TISS na wengine hawana majibu ya kutia moyo juu ya haya. Unategemea wananchi wa ukanda huo waamke wakazalishe huku hawajui kama watafika kesho? No, they can't,matokeo yake ni kuwa na wananchi wasioweza kuzalisha na kubakia kutegemea serikali yao hafifu isiyoweza kuwalinda iwape chakula na mambo mengine ya muhimu kwao.

Ninayo mengi ya kusema juu ya utawala huu wa Magufuli kwa leo hayo yanatosha, ila naomba itoshe tu kusema sioni PROGRESS yoyote tutakayopata kama nchi kutoka kwa utawala huu wa awamu ya tano.
UPENDE USIPENDE THE PRESIDENT IS DOING FINE NA ANATUPELEKA KWENYE DIRECTION NZURI. HAYO UNAYOTULETEA HAPA NI HISIA ZAKO BAADA YA BIASHARA ZA UJANJA UJANJA KUKWAMA
 
Kwenye hili la viwanda, nakubaliana na wewe, na mimi pia nimelizungumza hapa
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...

Paskali

Chronic Fault Finders.......people who habitually finds fault, complains, or objects, especially in a petty way

“Benefit Finders” focus on the positive. When you focus on the positive, the good appreciates. If you choose to focus on the negative, the good depreciates and the negative is accentuated.

Remember to see the good, the difficult, to see the potential in the seed…to be a “Benefit Finder”.
 
katika vitu sivipendi, basi mseme raisi ovyo.........mm akipatia nampongez na akikosea ni ubinadamu cha msingi wle washauri watampa nini kifanyika kama mbadala wake.

ila tujue hakuna kiongozi nakalia kiti ili atunyonye au kuiharibu nchi bali anafanya kwa mslahi ya kwetu
 
Kukosea ni ubinadamu, hilo halina mjadala.

Ila, mtu anavyozidi kuomba dhamana ya kupewa cheo kikubwa zaidi, ndivyo anavyotakiwa kupunguza uwezekano wake kukosea zadi.

Na mtu anapunguzaje uwezo wake wa kukosea kutuonyesha kwamba anaichukulia dhamana tuliyompa ya uongozi kuwa kitu muhimu na hivyo hataki kupunguza umakini wake?

Anafanya hivyo kwa kusikiliza watu kwa unyenyekevu. Usikivu huongeza maarifa,unyenyekevu unamfanya kiongozi aweze kuelewana na watu vizuri na kuongeza werevu na ushawishi.

Anafanya hivyo kwa kuwa makini katika kauli. Rasi aliye makini katika kauli anawapa wananchi confidence kwamba yupo makini hata katika mengine yanayohusu uongozi.

Anafanya hivyo kwa kuongoza kwa kuheshimu sheria na katiba. Hili ni jambo la msingi kabisa katika uongozi wa nchi, kitu ambacho rais amekula kiapo kutetea.

Anafanya hivyo kwa kuongoza kwa hekima zaidi na bila ubabe. Rais kwa kupewa urais tayari amepewa ubabe namba moja nchini, mbabe anayejijua yeye ni mbabe namba moja na mwenye akili hahitaji kupigia mstari ubabe wake,akifanya hivyo anaonekana hajiamini.Ubabe una hulka ya kupunguza hekima na kutakakufanya mambo kwa shortcut ambayo yataharibu matokeo.

Ukimsikia baba anamakakila siku "mimindiye baba nyumba hii"ujue anajisikia ana mapungufu fulani yanayomfanya atake kutangaza kwamba yeye ni baba. Baba anayejiamini hata hahitaji kusema yeye baba, familia itamtuza kama baba tu.

Anafanya hivyo kwa kuondoa jazba na kupima mambo kwa kina kabla ya uamuzi.Maamuzi ya jazba yanaweza kupigiwa makofi na raia wasio makini yanapotolewa, lakini ukiyapima kwenye mizani na matokeo ya muda mrefu yanatugharimu sana.

Anafanya hivyo kwa kuwa msikivu. Kukosa usikivu wa jumla ni kujinyima maarifa. Werevu huendana na usikivu. Rais asiye msikivu hata kama ana washauri wazuri atashindwa kuwatumia kikamilifu.Hawasikilizi. Anajiona anajua kila kitu.

Anafanya hivyo kwa kutokuwa mwepesi wa hasira bali mwepesi wa kuwaza kwa hekima. Rais ana nguvu sana na akifanya mambo kwa hasira inatugharimu kama nchi.Mtu mwenye hulka ya "mnanijua mimi?" hafai kuwa rais kwa sababu atafanya maamuzi ya hasira kwa show kinyume na hekima.

Anafanya hivyo kwa kutotengua tengua watu kila siku kama vile kubadilisha uongozi wa serikali ni sawa na kubadilisha nguo. Serikali ambayo watendaji wake wote wako katikawoga wa kutenguliwa muda wowote haiwezi kufanya kazi kwa ufanisi na ubunifu. Kila mtu anaogopa, ufanisi na ubunifu hauendani na kuogopa. Watu wanaogopa hata kuleta mawazo mapya serikalini.

Anafanya hivyo kwa kutokuwa na uadui usio na msingi na wafanyabiashara. Rais anatakiwa kukaa na wafanyabiashara na kuhakikisha anaweka mazingira mazuri ya biashara. Tunajua kuna wafanyabiashara wengi wezi na wakwepa kodi na mfumo ulikuwa umeoza, tunajua kuna haja ya kusafisha, lakini hilo halina maana kila mfanyabiashara ni mwizi na wafanyabiashara ni chanzo cha mapato tu cha serikali. Ni watu, ni raia, ni atengeneza ajira. Ni wakuza uchumi.

Anafanya hivyo kwa kupenda na kuthamini wananchi, na si kuongoza kwa kuwakomoa. Rais ambaye hajui kuongoza kiutu anaharibu nchi hata kama anafuata sheria. Sheria imewekwa kumsaidia mtu, si mtu aifuate sheria mpaka imuumize bila msingi.

Magufuli kashindwa katika yote hayo.
Unaandika maandishi ambayo viumbe wa lumumba walikatiwa mishipa ya ufahamu wa kuelewa sentensi zenye herufi kama hizo. Na kuna kitu ulisahau, ndie Rais wa kwanza kuchelewa kutangaza baraza lake la mawaziri, pia baada ya kulitangaza akatoka kifua mbele na "zakaria zote wazi" akidai amelichuja vya kutosha. Muda si mrefu Rugumi ikamvua nguo, n.k
 
Tanzania iko pale pale wanainchi wako imara na wanaipenda nchi yao.Wafanyakazi wanafanya kazi usiku na mchana kuijenga Tanzania.

Majeshi ya ulinzi na usalama yanailinda nchi yao ya Tanzania,watanzania wenyewe wake kwa waume na Mali zao usiku na mchana.

Na kwa hali hiyo Rais Magufuli anakazi nyepesi mno ya kufanya ktk kazi yake ya uraisi.
Huu unafiki nadhani hata shetani akikutana na wewe anaweza akakukimbia. Watu wanafanya kazi, wakati unambiwa BoT uchumi umeshuka, zile Tambo za TRA katangaza mapato zimepotelea wapi?

Usalama
Hapo kibiti raia (tena mbaya zaidi ni wa Ccm) wnauwawa kama kuku, unadai majeshi yanalinda?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unaandika maandishi ambayo viumbe wa lumumba walikatiwa mishipa ya ufahamu wa kuelewa sentensi zenye herufi kama hizo. Na kuna kitu ulisahau, ndie Rais wa kwanza kuchelewa kutangaza baraza lake la mawaziri, pia baada ya kulitangaza akatoka kifua mbele na "zakaria zote wazi" akidai amelichuja vya kutosha. Muda si mrefu Rugumi ikamvua nguo, n.k
Hizo teuzi na tenguzi ndiyo usiseme.

Kuna watu walikuwa wanateuliwa bila hata kuarifiwa.

Mtu anasoma gazetini kateuliwa mkuu wa wilaya.

Huyu ndiye rais makini anayesifiwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wengi tuliandika humu huyu jamaa ni JANGA KUBWA la Taifa. Kwa miezi 18 sasa ushahidi unaonyesha hatukukosea kabisa. Ngoja tusubiri miaka mitano iishe. Tanzania yetu itakuwa haitazamiki, kama tukichukulia mfano wa msuli basi msuli wote utakuwa umetapakaa kinyesi. Huwezi kuendesha nchi kwa sera MUFILISI na za kukurupuka huku akijiona yeye ndiye yeye hataki ushauri wa yoyote yule.

Hizo tsuzi na tenguzi ndiyo usiseme.

Kuna watu walikuwa wanateuliwa bila hata kuarifiwa.

Mtu anasoma gazetini kateuliwa mkuu wa wilaya.

Huyu ndiye rais makini anayesifiwa.
 
Wasalamu wana JF.

Kwanza kabisa nianze kwa kujifuta machozi na kuionea huruma nchi yangu ya Tanzania kwa kufika huku ilipofika kwa sababu ya ukosefu wa umakini katika chaguzi na teuzi za viongozi. Tumekuwa ni nchi yenye mfumo mbaya na wa kijinga wa uchaguzi wa viongozi na hata mfumo ya kiuteuzi umekuwa hivyo hivyo enzi na enzi sasa. Nchi yetu imejengwa katika misingi ya kinafiki na kujipendekeza ambayo imepelekea viongozi wengi kuwa watu wasiokuwa "REAL" katika mifumo yao ya kuongoza.

Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka wa kihistoria katika nchi yetu, ni mwaka amao tuliwashuhudia wavivu, wazembe na wanafiki wakiibuka kuyasaka madaraka kwa hila na mali. Ni mwaka ambao msululu wa wasaka tonge waijitokeza kuchukua fomu za kugombania nafasi kubwa ya Urais wa nchi yetu. Mathalani ndani ya chama tawala walijitokeza wagombea 42, lakini ukiwatazama hawa 42 wengi wao walikuwa hawajui kwa nini wamechukua fomu za kuomba kuiongoza nchi yetu. Wengi walijitokeza kwa kushitukiza, mashinikizo na hata kwa tamaa ya kutaka kukwea katika kiti kikubwa kuiko vyote ndani ya nchi na kiuongozi. Hawakuwa na nia wala malengo ya muda mrefu na nchi yetu. Kiufupi walijipeleka kwa mihemko.

Katika pilika pilika hizo chama cha Mapinduzi nach kiliingia kwenye mtego wao aidha kwa makusudi au kwa kujua na kufanikisha kuwachuja wagombea hadi watano na mwishowe watatu waliofanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kura. Ukiwatazama hawa wanafainali watatu hakuna hata mmoja aliyekuwa na ndoto ya Tanzania moyoni wala mawazoni mwake, walibeba fomu kwa mashinikizo ya wakubwa wao kipindi hicho.

KWA NINI UTAWALA WA MAGUFULI UTAFELI.

1. Kwa sababu alikuwa hajajiandaa kuwa Rais kisaikolojia au kimbinu. Magufuli hakujiandaa na wala hakuwahi kujua kama kuna siku anagekuja kubeba bendera ya kwanza ya nchi hii, hata uchukuaji wake wa fomu ya kugombea Urais unasemekana alishinikwa na Rais mmoja wa zamani. Kwamba chama kilimkosa mtu hivyo bwana mkubwa akalazimishwa abebe kijiti hiki. Kitaalamu ni kwmaba kama ulikuwa hujajiandaa kukifanya kitu na ukapewa dhamana ya kukifanya na kukisimamia kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa.

Dalii ni nyingi sana za Magufuli kushindwa na kuonyesha kwamba alikuwa hajajiandaa kuwa Rais, mfano nyingi ya teuzi zake zimekosa weledi na nyingi zimeonyesha mahaba , mfano alipoingia madarakani tu aiwateua DASs, DEDs, DCs, RASs, RCs na hata Mawaziri na Mananibu wao. Kwenye teuzi zilizopo chini ya TAMISEMI kwa maana ya DCS, DEDs, na DAS, mkuu huyu alionyesh kuchemka mapema sana mana majina ya wateuliwa ylikuwa yakijirudia mara kwa mara katika teuzi tofauti tofauti, hii inaashiria kuwa mkuu hakuwa makini katika uteuzi wake au alikuwa anafanya kazi mwenyewe bila ushauri wa vyombo husika na wasaidizi wake. Hii ni daili kuu ya kushindwa.

2. Dalili ya pili ya kushindwa kwa Magufuli ni kukosekana kwa uthabiti na ubunifu kwa utawala wake. Wengi wa watawala na wateuliwa wa Rais wamekuwa siyo wabunifu, wamekuwa ni watu wa kusikiliza maagizo na kuendeshwa kwa mihemko. Mfano kitu kikiibuka Dar kesho yake utasikia kimegeuka na kuwa kampeni kwa viongozi wote nchini, kana kwamba think tank ya nchi hii iko kichwani mwa mtu mmoja Dar es salaam. Leo akiibuka mtu Dar na kusema naanza zoezi la kuzibua mitaro ,basi kila kiongozi mikoani ataifanya hiyo ni ajenda na kampeni ya nchi nzima. Hizi ni dalili za kushindwa na kukkosa umakini na ubunifu kwa viongozi.

3. Sera ya Viwanda .

Watanzania wengi haswa wa kipato cha chini walimpa kura Magufuli kwa kuwa alijinadi kuwa Tanzania aliyotaka kuiongoza ilikuwa Tanzania ya viwanda na kwamba angehakikisha katika utawala wake viwanda vingi vinpatikan kadri iwezekanavyo lakini ni miaka miili sasa nchi na wananchi wake hawajaona sera, wala dira wala mpango wowote ukianzishwa na serikali ili kuwezesha kupatika kwa nchi ya viwanda. Serikali imekuwa ni wapiga domo na nadiriki kusema kuwa Magufuli na wenzake wanatupigia domo katika ishu hii ya viwanda, hakuna uhalisia wowote. Wangekuwa ni watu makini, wenye nia ya dhati ya viwanda basi wangekuwa wameishafikisha mpango mkakati bungeni ili ujadiiwe na kupelekea kufanikisha nchi njema ya viwanda. Huwezi kusema utavipata viwanda kutoka mawinguni bila ya kuwa na mpango mkakati wa kuviwezesha kupatikana.

4. Uongozi wa visasi na chuki.

Uongozi wa Magufuli umetawaliwa na visasi na chuki kwa baadhi ya watu katika nchi hii, kwa sasa ukiwa mpinzani wa kiitikadi na watawala unakuwa umegeuka kuwa adui wao moja kwa moja. Hii siyo dalili njema hata kidogo kwa mstakabali wa taifa, leo mawazo mazuri ya kujenga kutoka kwa wapinzani wa kiitikadi hayapokelewi, wapinzani wamegeuzwa punching boxes za vyombo vya dola na usalama, hawana amani, hawako huru. Linatengenezwa bomu litakalokuja kulipuka na kuilipua Tanzania vipande vipande... oooh god forbid maana hata Rwanda ilianza hvi hivi.

5. Usalama hafiifu wa raia.

Nchi kwa sasa inalalama, wananchi hawana usalama wa maisha yao, mauwaji yasiyojulikana kila kuchapo, watu kupotea bila kuonekana na kujulikana walipo. Vyombo vya dola havina majibu ya kuridhisha juu ya matukio haya, haya yanaongeza chuki na kupunguza imani na ushirikiano wa raia kwa serikali yao. Kwa sasa ukanda wa Pwani ni ukanda hatari sana wa kuishi kwa Mtanzania yeyote mwenye hofu na maisha yake, vyombo vya usalama vikiongozwa na Polisi, TISS na wengine hawana majibu ya kutia moyo juu ya haya. Unategemea wananchi wa ukanda huo waamke wakazalishe huku hawajui kama watafika kesho? No, they can't,matokeo yake ni kuwa na wananchi wasioweza kuzalisha na kubakia kutegemea serikali yao hafifu isiyoweza kuwalinda iwape chakula na mambo mengine ya muhimu kwao.

Ninayo mengi ya kusema juu ya utawala huu wa Magufuli kwa leo hayo yanatosha, ila naomba itoshe tu kusema sioni PROGRESS yoyote tutakayopata kama nchi kutoka kwa utawala huu wa awamu ya tano.
Nyambeya umeongea ukweli tupu ila ni vigumu sana kwa waliopo upande wa pili kukuelewa!! Na bado Serikali hii itazidi kuharibikiwa sana,Watu wasiokuelewa wataelewa wakati maji yalishafika shingoni ukweli mchungu,Serikali hii imeferi sana na itaferi sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hizo tsuzi na tenguzi ndiyo usiseme.

Kuna watu walikuwa wanateuliwa bila hata kuarifiwa.

Mtu anasoma gazetini kateuliwa mkuu wa wilaya.

Huyu ndiye rais makini anayesifiwa.
Binafsi ni mwamini mzuri tu wa kitu kinaitwa "MUDA" tuendelee kuombeana Afya njema na ufahamu wa kutosha, Ukweli utajizihirisha tu. Na naamini maandiko yako yatawafumbua macho na ufahamu, wasiwasi wangu ni pale muda utakapokuwa umewaacha.
 
Tatizo au mafanikio ya hii nchi yanaweza pia yakawa yamesababishwa na wapinzani .
Wapinzani kwa muda mrefu nao walitumika kuvuruga uwezo wa watu kufikiri na kuona nani ni kiongozi anayetufaa.
Mfano: Ni ukweli usiopingika kuwa Mh. Lowasa alikua ni kiongozi mahiri na aliyekuwa na ndoto ya kuwa rais tangu ujana wake enzi za Mwalimu.
Vita ya kufifisha ndoto zake zilianza ndani ya CCM kutokana na ukweli kuwa ndani ya CCM wengi walikuwa hawana uwezo wa kushindana na Lowasa kifedha na pia kisiasa na hata kiuwezo wa kutawala na kuongoza.
Lowasa alijaliwa uwezo wa kuongoza,kusimamia ,kutawala,kupendwa ,kuheshimiwa ,kusikilizwa,kuogopwa, kukubaliwa,kushawishi na fedha.
Kwa hali ya kawaida kila mtu aliyekuwa na ndoto ya kuwa rais ama ndani ya CCM au nje ni lazima kwanza angekua na kibarua cha kuharibu ndoto na uelekeo na kasi ya Lowasa ndipo ndoto yake itimie .

Wapinzani walijua mziki wa Lowasa,JK alijua mziki wa Lowasa uliomweka madarakani,Wale waliokua na ndoto za urais ndani ya CCM walijua mziki wake pia.

Tatizo likatokea kuwa wale waliokua wamejipanga kupata nafasi ta urais waliamua kuungana bila kujali tofauti zao na kushirikiana na wapinzani kumhujumu Lowasa.
Walifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

Michezo yote hiyo Viongozi wakongwe waluijua vizuri ndio maana waliamua kuwatosa wote na hatimaye kumpata Mh. Magufuli ambaye hakuwa na kundi lolote la hujuma kwa Lowasa wala kwa yale makundi mengine. Ndio maana hata ukimtizama mh. Magufuli utagundua kuwa hakuwa na tatizo na Lowasa.

Tujiulize siri zote walizokuwa wanazipata wapinzani bungeni na gazeti la mwanahalisi walikua wanazipata wapi?
Nani aliyekuwa anaiba siri za serikali na kuwapa wapinzani bila hata kukamatwa?
Ni kwa nini baada ya Lowasa kujiuzulu ndipo maspika wa bunge wakaanza kuwa wakali sana wa kuwabana wapinzani na wale wote waliokuwa wanajaribu kuitikisa serikali?

Hapa ndipo tunapoweza kusema kwa sauti kubwa "Mh. Rais Wewe Chapa kazi tu" Hakuna kusikiliza mtu.
Kama tutapata mafanikio basi wapinzani nao watakua wamechangia kwa kutumika kusaidia upatikanaji wa wagombea urais ndani ya CCM
Pia endapo JPM atashindwa basi wapinzani nao watakuwa wamechangia kwa kuwa walisaidia pia kupatikana kwa mgombea urais ndani ya CCM baada ya kukubali kutumuka kuwachafua baadhi ya watu.

Busara za wazee wetu walitumia mbinu ya kisiasa kwa kumpata JPM ili kufuta mizizi ya makundi ya mitandao ya kuchafuana ndani ya CCM ; amabapo walikuja na jina la JPM.
Kwa sasa amefanikiwa kuzima hiyo mitandao na hujuma za kuchafuana.

Kwa muda mrefu wapinzani wemebaki kwenye siasa za kushughulika na mtu badala yafumo.
Mfano muda mrefu wapinzani walikua wakimshughuliakia Lowasa wakasahau kudai Tume huru, wakasahau kuwa Tatizo ni bunge kumilikiwa na CCM.
Matokeo yake alipotolewa huyo Lowasa ndani ya mchakato wa CCM basi wananchi wakajua CCM kimekuwa chama safi,hivyo hata mgombea wake anafaa zaidi,na wakaichagua CCM na wabunge,madiwani wake na rais kwa sababu waliaminishwa kuwa mbaya alikua ni mtu mmoja yaani Lowasa.

Sasa bado wapinzani wanaendelea kupoteza muda kupambana na JPM ambaye ni mtu mmoja na kusahau tume huru na CCM ambayo ndio tatizo .
2025 itafika na watanzania wataletewa mgombea mwingine na atashinda kwa kishindo kwani muda wote wapinzani wametuaminisha kuwa tatizo la nchini yetu ni mtu mmoja na sio mfumo.
 
Chronic Fault Finders.......people who habitually finds fault, complains, or objects, especially in a petty way

“Benefit Finders” focus on the positive. When you focus on the positive, the good appreciates. If you choose to focus on the negative, the good depreciates and the negative is accentuated.

Remember to see the good, the difficult, to see the potential in the seed…to be a “Benefit Finder”.
Mkuu Ukweli ni Huu, thanks for this master piece!.

Naunga mkono hoja kuhusu fault finders who always focus on finding faults only hivyo they have negative vision and create negative energy ambayo mwisho wa siku it produces bad karma.

Mimi sii mmoja wa hao. Mimi niko kwenye kundi la positivity, naamini kwenye affirmatives and the powers of positive thinking.

Ndio maana ni miongoni mwa wana jf wa mwanzo mwanzo kabisa sio tuu kumkubali Magufuli, bali kuwa tipped kuwa ni Magufuli
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Wakati wa mchakato wa CCM kumtafuta mgombea, mimi nilitoa angalizo kuhusu dominant traits za wagombea wa CCM
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na Hatimaye Mgombea wa CCM!

Na baada ya Magufuli kupitishwa na CCM pia nilishauri
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

Nikaendelea kutoa lile angalizo kuhusu traits za Magufuli za Udikiteta nikiwaomba Watanzania wenzangu tutumie affirmative action ili Udikiteta huo uwe a benevolent one

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Pia nikawaeleza watu humu in a very positive way jinsi Magufuli alivyo fanana na Nyerere

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!

From there kwenye mazuri napongeza

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na Mungu, na Taifa Pia Litabarikiwa!

Hongera Rais Magufuli kwa kumruhusu Dangote achimbe Makaa ya Mawe, bado Reli na Gesi...

Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na Mungu, na Taifa Pia Litabarikiwa!

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!.

Paskali
 
Duh,wapinzani ni wengi kwa Mheshimiwa;
1. Walio kosa kuingia Ikulu ambao ni wapinzani wenye faida.
2. Walio tumbuliwa
3.Wenye vyeti feki
4.Wapiga dili
5.waingine ongezeeni.
Kwa maana hiyo michango humu Jamii forum lazima mtu uwe makini unapoisoma kuielewa mchangiaji ana maana gani!
 
Wee unafikiri ulivyoshinda kuendesha kuendesha hata familia yako ukafikiri kila mtu yuko Kama ww nunda mkubwa ww
 
Back
Top Bottom