Dalili kuu za kufeli kwa Rais Magufuli

Siwezi kusema kwa hakika kama Rais Magufuli atashindwa. Siwezi pia kujiaminisha kuwa atafanikiwa. Yote mawili (kushindwa au kufaulu) yanahitaji muda uamue. Hata hivyo, kama muda utaamua kuwa ameshindwa kuliongoza Taifa kwa mafanikio katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kidplomasia nk. kundi la kwanza la kulaumiwa itakuwa ni wana chama wa CCM, wabunge wa CCM, na viongozi wa ngazi mbalimbali katika chama. Hawa wana wajibu wa moja kwa moja kumshauri M/kiti wao ambaye pia ndiyo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati wa TANU, kulikuwa na ahadi 10 za mwana TANU, moja ya ahadi hizo ilisomeka "Nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko." Viongozi waliambiwa ukweli, walishauriwa na wao walipima na kufanyia kazi ushauri waliopewa. Nachelea kusema, japo ahadi hizo za TANU, hazina tena nafasi katika CCM mpya ya Rais Magufuli, tunacho kishuhudia ni kinyume cha ahadi hiyo! Kundi la pili linalopaswa kulaumiwa endapo Rais Magufuli atashindwa ni Wananchi wa kawaida wasio na uthubutu wa kuhoji na kukosoa huku wakipendekeza nini kifanyike. Wanao kosoa siyo maadui, hawana nia mbaya na Taifa lao Tanzania, wasichukuliwe kuwa ni wahaini kwa kuwa na mawazo mbadala/kinzani yasiyopendwa kusikilizwa na watawala. Tuwasikilize, tusipo kubaliana nao, tuwapinge kwa hoja zenye mashiko. Wakitoa ushauri mzuri, tuwashukuru na kuufanyia kazi. Kwa kufanya hivyo, naamini, kama Taifa tutsaonga mbele. Hatuta tumia muda mwingi kulumbana hata kwa mambo ya msingi. Tutaheshimiana na kuijenga Nchi kwa pamoja! Tutaifikia Tanzania mpya kila Mwananchi akitimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na viongozi wetu.
 
Toa haya maneno "dalili kuu za" uzi utapendeza sana.

Haiwezekani mnakuwa na Rais ambaye mpaka leo anajua kuwa "kata" ni maneno mawili.
 
Kuendesha nchi mama familiar in hatari. Sasa hivi anahangaika kudhibiti Binge wakati ni mhimili mwingine
 
Mtasubiri sana hashindwi mtu na akimaliza 10 tunamuongezea.
Umejiita Maharo,hiyo ni password ya akili yako inavyofanya kazi kinyume,na huu ni mwendelezo wa unafiki,kwani nyie hamuoni mapato yalivyoshuka,hana ubunifu,mnamuogopa kwani nyie ni walinzi wa geti lake?
Anafuata Mbinu za Kagame,Kagame is just a Fake one,nyie mmechagua role modal fake,akili fake,Msitegemeee mavuno wakati mnapanda mbegu za chuki,Bot wanafanya kazi kama sio wataalamu wa uchumi,Hivi enyi wagaratia nani kawaroga.
 
Wasalamu wana JF.

Kwanza kabisa nianze kwa kujifuta machozi na kuionea huruma nchi yangu ya Tanzania kwa kufika huku ilipofika kwa sababu ya ukosefu wa umakini katika chaguzi na teuzi za viongozi. Tumekuwa ni nchi yenye mfumo mbaya na wa kijinga wa uchaguzi wa viongozi na hata mfumo ya kiuteuzi umekuwa hivyo hivyo enzi na enzi sasa. Nchi yetu imejengwa katika misingi ya kinafiki na kujipendekeza ambayo imepelekea viongozi wengi kuwa watu wasiokuwa "REAL" katika mifumo yao ya kuongoza.


Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka wa kihistoria katika nchi yetu, ni mwaka amao tuliwashuhudia wavivu, wazembe na wanafiki wakiibuka kuyasaka madaraka kwa hila na mali. Ni mwaka ambao msululu wa wasaka tonge waijitokeza kuchukua fomu za kugombania nafasi kubwa ya Urais wa nchi yetu. Mathalani ndani ya chama tawala walijitokeza wagombea 42, lakini ukiwatazama hawa 42 wengi wao walikuwa hawajui kwa nini wamechukua fomu za kuomba kuiongoza nchi yetu. Wengi walijitokeza kwa kushitukiza, mashinikizo na hata kwa tamaa ya kutaka kukwea katika kiti kikubwa kuiko vyote ndani ya nchi na kiuongozi. Hawakuwa na nia wala malengo ya muda mrefu na nchi yetu. Kiufupi walijipeleka kwa mihemko.



Katika pilika pilika hizo chama cha Mapinduzi nach kiliingia kwenye mtego wao aidha kwa makusudi au kwa kujua na kufanikisha kuwachuja wagombea hadi watano na mwishowe watatu waliofanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kura. Ukiwatazama hawa wanafainali watatu hakuna hata mmoja aliyekuwa na ndoto ya Tanzania moyoni wala mawazoni mwake, walibeba fomu kwa mashinikizo ya wakubwa wao kipindi hicho.


KWA NINI UTAWALA WA MAGUFULI UTAFELI.


1. Kwa sababu alikuwa hajajiandaa kuwa Rais kisaikolojia au kimbinu. Magufuli hakujiandaa na wala hakuwahi kujua kama kuna siku anagekuja kubeba bendera ya kwanza ya nchi hii, hata uchukuaji wake wa fomu ya kugombea Urais unasemekana alishinikwa na Rais mmoja wa zamani. Kwamba chama kilimkosa mtu hivyo bwana mkubwa akalazimishwa abebe kijiti hiki. Kitaalamu ni kwmaba kama ulikuwa hujajiandaa kukifanya kitu na ukapewa dhamana ya kukifanya na kukisimamia kuna uwezekano mkubwa sana wa kushindwa.


Dalii ni nyingi sana za Magufuli kushindwa na kuonyesha kwamba alikuwa hajajiandaa kuwa Rais, mfano nyingi ya teuzi zake zimekosa weledi na nyingi zimeonyesha mahaba , mfano alipoingia madarakani tu aiwateua DASs, DEDs, DCs, RASs, RCs na hata Mawaziri na Mananibu wao. Kwenye teuzi zilizopo chini ya TAMISEMI kwa maana ya DCS, DEDs, na DAS, mkuu huyu alionyesh kuchemka mapema sana mana majina ya wateuliwa ylikuwa yakijirudia mara kwa mara katika teuzi tofauti tofauti, hii inaashiria kuwa mkuu hakuwa makini katika uteuzi wake au alikuwa anafanya kazi mwenyewe bila ushauri wa vyombo husika na wasaidizi wake. Hii ni daili kuu ya kushindwa.



2. Dalili ya pili ya kushindwa kwa Magufuli ni kukosekana kwa uthabiti na ubunifu kwa utawala wake. Wengi wa watawala na wateuliwa wa Rais wamekuwa siyo wabunifu, wamekuwa ni watu wa kusikiliza maagizo na kuendeshwa kwa mihemko. Mfano kitu kikiibuka Dar kesho yake utasikia kimegeuka na kuwa kampeni kwa viongozi wote nchini, kana kwamba think tank ya nchi hii iko kichwani mwa mtu mmoja Dar es salaam. Leo akiibuka mtu Dar na kusema naanza zoezi la kuzibua mitaro ,basi kila kiongozi mikoani ataifanya hiyo ni ajenda na kampeni ya nchi nzima. Hizi ni dalili za kushindwa na kukkosa umakini na ubunifu kwa viongozi.



3. Sera ya Viwanda .

Watanzania wengi haswa wa kipato cha chini walimpa kura Magufuli kwa kuwa alijinadi kuwa Tanzania aliyotaka kuiongoza ilikuwa Tanzania ya viwanda na kwamba angehakikisha katika utawala wake viwanda vingi vinpatikan kadri iwezekanavyo lakini ni miaka miili sasa nchi na wananchi wake hawajaona sera, wala dira wala mpango wowote ukianzishwa na serikali ili kuwezesha kupatika kwa nchi ya viwanda. Serikali imekuwa ni wapiga domo na nadiriki kusema kuwa Magufuli na wenzake wanatupigia domo katika ishu hii ya viwanda, hakuna uhalisia wowote. Wangekuwa ni watu makini, wenye nia ya dhati ya viwanda basi wangekuwa wameishafikisha mpango mkakati bungeni ili ujadiiwe na kupelekea kufanikisha nchi njema ya viwanda. Huwezi kusema utavipata viwanda kutoka mawinguni bila ya kuwa na mpango mkakati wa kuviwezesha kupatikana.



4. Uongozi wa visasi na chuki.


Uongozi wa Magufuli umetawaliwa na visasi na chuki kwa baadhi ya watu katika nchi hii, kwa sasa ukiwa mpinzani wa kiitikadi na watawala unakuwa umegeuka kuwa adui wao moja kwa moja. Hii siyo dalili njema hata kidogo kwa mstakabali wa taifa, leo mawazo mazuri ya kujenga kutoka kwa wapinzani wa kiitikadi hayapokelewi, wapinzani wamegeuzwa punching boxes za vyombo vya dola na usalama, hawana amani, hawako huru. Linatengenezwa bomu litakalokuja kulipuka na kuilipua Tanzania vipande vipande... oooh god forbid maana hata Rwanda ilianza hvi hivi.



5. Usalama hafiifu wa raia.

Nchi kwa sasa inalalama, wananchi hawana usalama wa maisha yao, mauwaji yasiyojulikana kila kuchapo, watu kupotea bila kuonekana na kujulikana walipo. Vyombo vya dola havina majibu ya kuridhisha juu ya matukio haya, haya yanaongeza chuki na kupunguza imani na ushirikiano wa raia kwa serikali yao. Kwa sasa ukanda wa Pwani ni ukanda hatari sana wa kuishi kwa Mtanzania yeyote mwenye hofu na maisha yake, vyombo vya usalama vikiongozwa na Polisi, TISS na wengine hawana majibu ya kutia moyo juu ya haya. Unategemea wananchi wa ukanda huo waamke wakazalishe huku hawajui kama watafika kesho? No, they can't,matokeo yake ni kuwa na wananchi wasioweza kuzalisha na kubakia kutegemea serikali yao hafifu isiyoweza kuwalinda iwape chakula na mambo mengine ya muhimu kwao.


Ninayo mengi ya kusema juu ya utawala huu wa Magufuli kwa leo hayo yanatosha, ila naomba itoshe tu kusema sioni PROGRESS yoyote tutakayopata kama nchi kutoka kwa utawala huu wa awamu ya tano.

Hakuna hata punje ya mchele katika pumba ulizoandika hapa. Unatupotezea muda wetu bure.
 
Naamini ili Systems(Mifumo) mizuri ipate kuwepo na kutumika, inabidi Viongozi wakuu wa nchi, hasa Raisi;

1. Waelewe maana na faida ya kuwepo kwa mifumo hiyo, na wawe na nia ya dhati yakufanya iwepo na kusimamia utekelezaji wake.
2. Watambue kuwa wanahijati (nchi inahitaji) kuwa na Think Tank ya kitaifa imara na endelevu.
N.K.

Mifumo hiyo ni muhimu ikawa (pamoja na vitu vingine) na UWAZI (transparency), UWAJIBIKAJI(accountability) na ijengwe katika dhana ya "Amini lakini Thibitisha" (trust but verify).

Kwa bahati mbaya (kwa maoni yangu), dalili zinaonyesha kuwa uongozi wa nchi uliopo madarakani unaamini kuwa mifumo/mfumo iliyopo inafaa kutumika kutuletea "maendeleo ya kweli", lakini tatizo lipo katika utekelezaji/usimamizi, na hivyo wamejikita katika kurekebisha utekelezaji/usimamizi.
Mkuu selemala, thanks for this!, huwezi amini, hii post yako ndio naisoma leo!.
P
 
Back
Top Bottom